Sunday, July 6, 2014

Lengo na faida za MAULIDI ● kwa ufupi - Albeidh

taraweh na idi-allamah ustadh muhammad


SWAUM KWA MTAZAMO WA WANAVYUONI WA TAZKIYAH

  بسم الله و  الحمد لله .
 Tungependa kuangaziya Ibada ya Funga(Swaum) kwa mtazamo na fikra za Wanavyuoni wa Tazkiyah/Taswawwuf.

Kama wanavyuoni wa Fiqhi,Wanavyuoni wa Tazkiyah/Taswawwufwanakubaliana kuwa funga ya Ramadhani ni lazima na kadhalika ya kafara,deni n.k. na kuna za sunnah kama za Siku sita za Shawwal,Kila jumatatu na alhamisi n.k. kwao wao saum ina vigawanyo.Asema Imam Abu Hamid Muhammad bin Muhammad bin Muhammad Al-Ghazali رحمه الله  katika kitabu chake IHYA ULUM DIN "Saumu ni daraja tatu, saumu ya watu wote nayo ni kutokamana na vyenye kufuturisha. saumu ya khaswa nayo ni kuzuiliya viungo visifanye madhambi na saumu ya khaswa wa khaswa nayo ni kulekeza moyo kwa Allah pekee"
wakasema tena "watu wa kawaida hufunga kwa kuwacha mufattwiraat lakini walio juu kwa daraja hufunga kwa kuwacha shahawaat(matamanio ya nafsi) na muharramaat(yaliyoharamishwa)"


Ulamaa wa Tazkiyah, mbali na Fadhwaail mbali mbali za Swaum zilizotajwa na faida za ki-afya wanataja kuwa swaum ina faida za ki-moyo nyingi.

Imam Abdullah bin Alwy bin Muhammad Al-Haddad رحمه الله  katika itabu chake maarufu 'annaswaihu diniyah' asema "saumu ndiyo nguzo ya mazoezi ya nafsi na msingi wa mujahadah"

Saum kwao ni mmoja katika misingi ya kuenda kwa Allah. .    تقليل الكلام والمنام و الطعا م




و الله أعلم