Monday, October 29, 2012

Kumzuru Rasul'Allah (s.a.w) na Ku-tawassal kupitia kaburi lake.


Kuzuru Kaburi La Rasul'Allah (S.A.W) na Ku-tawasal kupitia kaburi la Mtume Swalallahu aleihi wa salaam
Kuzuri kaburi la Mtume s.a.w ni katika manduubaat zilotiliwa mkazo zaidi, bali kwa baadhi ya maulamaa ni karibu na wajibu, bali kwa madhehebu ya dhwahiriya ( moja katika madhehebu ya fiqhi ) ni wajib..
ndio tunamuona Imam Nawawi katika almajmuua anasema: واعلم ان زيارة قبر النبي صلى الله عليه وسلم من أهم القربات وانجح المساعي ..., فإذا انصرف الحجاج والمعتمرون من مكة استحب لهم استحبابا مؤكدا ان يتوجهوا لزيارته صلى الله عليه وسلم وينوي الزائر من الزيارة التقرب وشد الرحل والصلاة فيه
Na imam ibnu Qudaamah asema katika almughni : وإذا فرغ من الحج استحب له زيارة قبر النبي صلى الله عليه وسلم وقبر صاحبيه

Friday, October 19, 2012

Kizee na muoka mikate


Kisa cha Kizee na Muoka mikate

Kizee, baada ya salatul Ishaa akajikusanya akitaraji kupata rukhsa kulala pale msikitini, kwani yeye si mwenyeji wa huo mji...anapitia tu. Bahati mbaya mchunga msikiti akamkatalia kizee huyo kulala ndani. 

Kizee akabembeleza bila mafanikio, akatoka nje na kuandaa matandiko alale pale nje tu ya msikiti, lakini haikutosha kwa yule mchunga msikiti, bado akamfukuza hat
a hapo...tena kwa kumburuza.

Pembeni kukawa na duka la muoka mikate, alipoona hivyo akamhurumia kizee yule na kumkaribisha ndani kumpatia hifadhi usiku huo. Ndani ya duka kizee yule kabla kupitiwa usingizi akaona mwenyeji wake (muoka mikate) akifanya istighfar kwa wingi sana...kipindi chote, huku akiendelea na shughuli zake. Kizee akamuuliza kama ameona nini faida/matokeo kutokana na tabia yake hiyo ya kufanya istighfar wakati wote mara nyingi hivyo? Muoka mikate akamjibu kuwa KILA jambo aliloomba kwa Allah limejibiwa (kukubaliwa) isipokuwa tu jambo moja. Kizee akamuuliza, ni jambo lipi ambalo haukujibiwa? Muoka mikate akasema nimemuomba Allah muda mrefu aniwezeshe kukutana na Mwanazuoni mkubwa maarufu, Imam Ahmad Ibn Hanbal.

Na hapo ndipo kizee akajitambulisha kwa kusema si tu kuwa Allah amekusikia dua yako bali pia ameniburuza mpaka mlangoni kwako.

Imam Ahmad pamoja na umaarufu wa jina na sifa nyingi si wengi walimjua kwa sura walioishi miji ya mbali naye. Na hakupenda makuu, hakutaka kujitambulisha alipofika hapo mjini ambapo hakumjua mtu yeyote kwani angefanya hivyo kila mtu angetaka kumkaribisha nyumbani kwake.