Kuzuru Kaburi La Rasul'Allah (S.A.W) na Ku-tawasal kupitia kaburi la Mtume Swalallahu aleihi wa salaam
Kuzuri kaburi la Mtume s.a.w ni katika manduubaat zilotiliwa mkazo zaidi, bali kwa baadhi ya maulamaa ni karibu na wajibu, bali kwa madhehebu ya dhwahiriya ( moja katika madhehebu ya fiqhi ) ni wajib..
ndio tunamuona Imam Nawawi katika almajmuua anasema: واعلم ان زيارة قبر النبي صلى الله عليه وسلم من أهم القربات وانجح المساعي ..., فإذا انصرف الحجاج والمعتمرون من مكة استحب لهم استحبابا مؤكدا ان يتوجهوا لزيارته صلى الله عليه وسلم وينوي الزائر من الزيارة التقرب وشد الرحل والصلاة فيه

Na imam ibnu Qudaamah asema katika almughni : وإذا فرغ من الحج استحب له زيارة قبر النبي صلى الله عليه وسلم وقبر صاحبيه
Na huu ndio mfumo wa mafuqahaa.. kwa dalili kutoka kwa qur'an na sunna na ijmaaa.
Swali linaulizwa Na jee ,mbona twaambiwa si wajibu kufanya Ziyara kwa Mtume na yasemwa si katika nguzo za Hijja au Umrah?Na je tukifika kaburini kwa Mtume nini tuseme?au tuombe dua vipi?Na wapo wengine hushangazwa na watu wanaokwenda Hajj kupeleka Salaam kwa Mtume swalallahu aleihi wa Salaam na imefikia kudai kuwa ni shirk, Je hili suala liko vipi?

Kwanza kabisa tukubaliane kuwa ndiyo kumzuru Mtume swalallahu aleihi wa salaam si katika nguzo za Hajj au Umrah bali ni mustahab kuzuru kabla ama baada ya Hajj na Umrah na ni sunnah kusafiri na kuzuru Kaburi la Mtume(salalahu alaih wasalam) wakati wowote
Swali jingine linauliza je jambo likiwa مستحب(mustahab) inawajibikia watu kuwakataza wengine kulifanya jambo hilo?
Jawabu ni kuwa haiwajibiki kukataza watu kufanya jambo la Mustahab na hawa wanaokataza watu kusafiri kuzuru kaburi la Mtume(salalahu alaih wasalam) wametoka katika ijmaa na Imam Ibn Tayimiyyah ndiye aliyeanzisha fikra hii na hiyo ilikuwa ni IJTIHADI yake mwenyewe ambayo inapishana kwa marefu na mapana na Salaf Swaleh na bila shaka amekosea hapo kwa kukhalifu Ijmaa na kama alivyosema Mtume s.a.w mwenye kufanya IJTIHADI na akakosea ana ujira 1 shidakubwa iliyopo ni hao walofuata kosa lake hilo na kulifanya ndio mfumo wa dini na hivyo wamekuwa wamekhalifu ijmaa ya ummah yaani Ahlul Sunnah wal Jamaa na wamepishana sana na Salaf Swaleh.
"Amesema, swala na salamu zimwalie pamoja na Aali zake: "Man zara qabri wajabat lahu shafa`ati ikimaanisha 'Mwenye kunijia mimi kwaa ziara tu, hakuna haja nyingine iliyomvuta isipokuwa kunizuru mimi, basi huwa ni haki juu ya Mwenyezi Mungu, Aliye-tukuka, kuwa mimi niwe muombezi wake siku ya kiyama.' Na 'hakuna yeyote yule katika Ummah wangu ambaye ana wasaa, na licha ya hayo asinizuru basi huyo hana udhuru,' na 'yule mwenye kuniswalia kwenye kaburi langu, basi Mwenyezi Mungu humwakilisha Malaika mwenye kunifikishi mimi swala hiyo, na yeye hutoshelezwa kwenye mambo ya dunia yake na Akhera yake, na mimi huwa ndiye muombezi wake siku ya Kiyama au shahidi wake.'( Imesimuliwa na al-Daraqutni, al-Dulabi, al-Bayhaqi, Khatib al-Baghdadi, al-`Uqayli, Ibn `Adiyy, Tabarani, na Ibn Khuzaymah. Kila mmoja kwa njia yake na zote njia zao zinakutana na Musa ibn Hilal al-`Abdiyy , Ubayd Allah Ibn Umar, na wote walipokea kutoka kwa Nafi` na Ibn `Umar.Imam Dhahabi ameiswahihisha na kusema ni Hassan, Al Sakhawi naye ameiswahihisha katika Maqasid al Hasana na Subki ameiswahihisha katika Saadat Al Darayn.Na hivyo tunaona hao wenye kujinasibisha na Salafiyah wanapingana sio tu na Ijmaa bali kupinga Sunnah kwa kisingizio cha kufuata Quraan na Sunnah na Salaf Swaleh.
Amakuhusu kufika na kutoa salaam kwa Mtume Swalallahu aleihi wa salaam , Al'imaam ibnu qudaamah asema katika almughni: mtu akifika pale atakikana akipe kibla mgongo na aelekee katikati ya chumba alichozikwa Mtume s.a.w na aseme السلام عليك أيها النبي ورحمة الله و بركاته , السلام عليك يا نبي الله وخيرته من خلقه , ا...شهد ألا اله إلا الله وحده لا شريك له وان محمدا عبده ورسوله , أشهد أنك قد بلغت رسالات ربك و نصحت لأمتك , ودعوت إلى سبيل ربك بالحكمة و الموعظة الحسنة , وعبدت الله حتى أتاك اليقين , فصلى الله عليك كثيرا كما يحب ربنا ويرضى , اللهمَّ اجزه عنَّا أفضل ما جزيت أحداً من النبيين والمرسلين , وابعثه المقام المحمود الذي وعدته يغبطه به الأولون والآخرون , اللهمَّ صلِّ على محمد وعلى آل محمد كما صليت على إبراهيم وعلى آل إبراهيم إنك حميد مجيد , اللهمَّ إنك قلت وقولك الحق: ((وَلَوْ أَنَّهُمْ إِذْ ظَلَمُوا أَنْفُسَهُمْ جَاءُوكَ فَاسْتَغْفَرُوا اللَّهَ وَاسْتَغْفَرَ لَهُمُ الرَّسُولُ لَوَجَدُوا اللَّهَ تَوَّاباً رَحِيماً)) وقد أتيتك مستغفراً من ذنوبي, مستشفعاً بك إلى ربي؛ فأسألك يا ربِّي أن توجب لي المغفرة كما أوجبتها لمن أتاه في حياته , اللهمَّ اجعله أول الشافعين وانجح السائلين وأكرم الأولين والآخرين , برحمتك يا أرحم الراحمين , ثم يدعوا لوالديه وإخوانه وللمسلمين أجمعين . ثم يتقدم قليلاً ويقول : السلام عليك يا أبا بكر الصديق السلام عليك يا عمر الفاروق , السلام عليكما يا صاحبي رسول الله صلى الله عليه وسلم وضجيعيه ووزيريه ورحمة الله وبركاته اللهمَّ اجزهما عن نبيهما وعن الإسلام خيراً , سلام عليكم بما صبرتم فنعم عقبى الدار , اللهمَّ لا تجعله آخر العهد من قبر نبيك ومن حرم مسجدك يا أرحم الراحمين
Maana yake
Amani iwe juu yako ewe Mtukufu wa daraja na rehema za Mungu na baraka zake pia ziwe juu yako, amani iwe juu yako ewe Mtume wa Mungu na kiumbe wake mbora.... nashuhudia kuwa hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ispokua Allaah peke yake hana mshirika, na nashuhudia kuwa Muhammad ni mja waje na Mtume wake. nashuhudia kuwa wewe umefikisha risala za mola wako na ukawanasihi ummati wako, na ukalingani katika njia ya Mola wako kwa hikma na mawaidha mazuri, na ukamuabudu Allaah mpaka kufariki. basi mola akuswalie kwa wingi kama anavopenda Mola wetu na anavyoridhia, Ewe Mola mpe mjazi zaidi ya unavyo wapa majazi manabii wako na mitume wako, na umpe Maqaam Mahmuud uliyomuahidi ambayo wanamuonea wivu wa kwanza wap na wa mwisho wao, Ewe Mola mswalie Muhammad na aali zake Muhammad kama ulivyomswalia Ibrahim na aali zake Ibrahim hakika wewe ni mwingi wa kusifiwa na mwenye daraja ya juu. ewe Mola hakika umesema, na qawli yako ni haki ( na lau pale walipojidhulumu nafsi zao wangeli kujia, wakamuomba Mwenyezi Mungu msamaha, na Mtume akawaombea msamaha, hapana shaka wangeli mkuta Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba na Mwenye kurehemu ). na hakika nimekujia huku nikiomba msamaha kutokamana na madhambi yangu, nikitaka shufaa kutoka kwako kumuelekea Mola wangu, nakuomba Mola wangu unisamehee kama ulivyo wasamehea waliomjia wakati wa uhai wake. Ewe Mola mjaalie awe wa kwanza wao kuomba shufaa, na mzuri wa wenye kuomba, na mtukufu wa wa mwanzo wao na wa mwisho wao, kwa rehema zako Ewe Mwenye kurehemu zaidi ya wengine.(kasha ikifikia hapa) mtu anawaombea wazazi wake na ndugu zake na waislamu wote. kisha anatangulia kidogo na kusema : amani iwe juu yako Ewe Abubakr As-Swiddyq, amani iwe juu yako Ewe Omar bin Khattwaab, amani iwe juu yenu enyi maswahaba wa Mtume s.a.w na mulozikwa nae na mawaziri wake na rahma za Mwenyezi Mungu na baraka zake. Ewe Mola wajazi kutokamana na Nabii wako na waislamu jaza njema, amani iwe juu yenu kwa sababu ya mulivyo subiri, basi ni mema mno malipo ya nyumba ya akhera. Ewe Mola usijaalie iwe ni mara ya mwisho kuzuru kaburi la Mtume wako na haram ya msikiti wako ewe mwenye kurehemu zaidi wenye kurehemu.

Makala hii imetanguliza kusema kuwa maulamaa wametoa dalili ya maneno yao kutoka kwa Qur'an, hadithi na ijmaaa. dalili ya kutoka kwa Qur'an ni aya ya 64 katika suratun Nisaa, Allaah s.w asema: وَلَوْ أَنَّهُمْ إِذْ ظَلَمُوا أَنْفُسَهُمْ جَاءُوكَ فَاسْ...تَغْفَرُوا اللَّهَ وَاسْتَغْفَرَ لَهُمُ الرَّسُولُ لَوَجَدُوا اللَّهَ تَوَّاباً رَحِيماً ‘’…….yaani na lau pale watakapozidhulumu nafsi zao watakujia wamuombe msamaha Allaah na waombewe msamaha na Mtume basi wangempata Allaah mwingi wa kukubali toba na mwingi wa rehema……’’ Ama kuhusu Ayah hii ya 64 Sura ya 4
وَلَوْ أَنَّهُمْ إِذ ظَّلَمُواْ أَنفُسَهُمْ جَآءُوكَ فَاسْتَغْفَرُواْ اللَّهَ وَاسْتَغْفَرَ لَهُمُ الرَّسُولُ لَوَجَدُواْ اللَّهَ تَوَّاباً رَّحِيماً

Na hatukumtuma Mtume yeyote ila at'iiwe kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na lau pale walipo jidhulumu nafsi zao wangeli kujia, wakamwomba Mwenyezi Mungu msamaha, na Mtume akawaombea msamaha, hapana shaka wangeli mkuta Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba na Mwenye kurehemu.
Ibn Kathir katika Tafsir yake anaelezea kisa maarufu kuhusiana na Ayah hii ambayo kwenye Tafsir iliyochapwa na Darus Salaam inayotegemewa na Masalafiyah/ Answar Sunnah kisa hiki kimeng'olewa kwa makusudi kabisa ya kupotosha umma wa Kiisilamu
وَقَدْ ذَكَرَ جَمَاعَة مِنْهُمْ الشَّيْخ أَبُو مَنْصُور الصَّبَّاغ فِي كِتَابه الشَّامِل الْحِكَايَة الْمَشْهُورَة عَنْ الْعُتْبِيّ قَالَ :
كُنْت جَالِسًا عِنْد قَبْر النَّبِيّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَجَاءَ أَعْرَابِيّ فَقَالَ : السَّلَام عَلَيْك يَا رَسُول اللَّه سَمِعْت اللَّه يَقُول " وَلَوْ أَنَّهُمْ إِذْ ظَلَمُوا أَنْفُسهمْ جَاءُوك فَاسْتَغْفَرُوا اللَّه وَاسْتَغْفَرَ لَهُمْ الرَّسُول لَوَجَدُوا اللَّه تَوَّابًا رَحِيمًا " وَقَدْ جِئْتُك مُسْتَغْفِرًا لِذَنْبِي مُسْتَشْفِعًا بِك إِلَى رَبِّي ثُمَّ أَنْشَأَ يَقُول : يَا خَيْر مَنْ دُفِنَتْ بِالْقَاعِ أَعْظُمه فَطَابَ مِنْ طِيبهنَّ الْقَاع وَالْأَكَم نَفْسِي الْفِدَاء لِقَبْرٍ أَنْتَ سَاكِنه فِيهِ الْعَفَاف وَفِيهِ الْجُود وَالْكَرَم ثُمَّ اِنْصَرَفَ الْأَعْرَابِيّ فَغَلَبَتْنِي عَيْنِي فَرَأَيْت النَّبِيّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَآله وَسَلَّمَ فِي النَّوْم فَقَالَ : يَا عُتْبِيّ الْحَقْ الْأَعْرَابِيّ فَبَشِّرْهُ أَنَّ اللَّه قَدْ غَفَرَ لَهُ
"

Miongoni mwa Masheikhe akiwemo Shaikh Abu Nasrin Al-Sabbagh katika kitabu chake Ash-Shamil, ameelezea kisa hiki mashuhur kutoka kwa Utbi , ambaye anasimulia
Nilikuwa nimekaa karibu na kaburi la Mtume S.A.W alipokuja Bedui(Muarabu) na kuanza kusema...''Asalaam aleika Ya Rasuulu-Allah. ..Nimemsikia Allah akisema ...'' وَلَوْ أَنَّهُمْ إِذْ ظَلَمُوا أَنْفُسهمْ جَاءُوك فَاسْتَغْفَرُوا اللَّه وَاسْتَغْفَرَ لَهُمْ الرَّسُول لَوَجَدُوا اللَّه تَوَّابًا رَحِيمًا " ......Hivyo nimekuja kwako kutaka msamaha wa dhambi zangu na kuomba Shafaa yako kwa Allah , kisha akaanza kusoma mashairi
: يَا خَيْر مَنْ دُفِنَتْ بِالْقَاعِ أَعْظُمه فَطَابَ مِنْ طِيبهنَّ الْقَاع وَالْأَكَم نَفْسِي الْفِدَاء لِقَبْرٍ أَنْتَ سَاكِنه فِيهِ الْعَفَاف وَفِيهِ ا......
Ewe Mbora wa waliolala ardhini(makaburini) mbaye harufu nzuri mpaka mwisho wa mashairi.... .

Baada ya kusoma mashairi hayo akaondoka, Utbi akapitiwa na usingizi akatokewa na mtume katika usingizi , Mtume akamweleza Ewe Utbi mkimbilie yule Bedui na umpe khabari njema kuwa Allah amemsamehe madhambi yake!!!
Kisa hiki kimesimuliwa na maulamaa wakubwa na wa kutegemewa wa Ahlul Sunnah wal Jamaa wakiwemo Imam Nawawi katika kitabu chake Adhkaar, Ibn Qudama na wengine wengi
Mufassiriina walifahamu kua kumjia Mtume s.a.w ni wakati wowote ndio wakawa wanataja kisa cha U’tbiy mashuhuri kilotajwa hata kwa tafsir ya ibnu kathiyr Sheikh tegemezi la Tafsiri ya wale wajiitao Salafiyah ila leo wameihujumu Tafsiri hii kwa kuking’oa kipande hiki miaka ya hivi karibuni na wakijua kuwa wanajidhulumu nafsi zao hawa watu na kuanza kusema mafundisho haya ni shirk?! Ibn Kathir hakuona huyu mtu alikwenda kwenye kaburi la Mtume na kufanya Shirk na akatuletea kisa hiki kwenye Tafsir yake maarufu bila sherhe yoyote kwani kinajitosheleza chenyewena Ibn Kathir hakuona itapelekea watu kufanya shirk na kutoka atika Uisilamu wao?
Kisa hiki hata Qurtubi amekielezea, Angalizo angalieni Tafsiri zote ambazo haziko chini ya ufadhili wa Mamlaka Saudi Arabia na zile zote ambazo kabla Dar-Us Salaam haijaanza kuchapisha vitabu utakuta maandishi haya ya Ibn Kathir na Tafsiri Qurtubi Ila machapisho mapya ya Daru-Salaam na viungo vyake vyote vyenye kueneza mafundisho ya Kisalafiyah kipande hiki hakimo na vitabu vingi vinavyochapishwa na Salafiyah kuna vipande vingi mno vinavyopishana na mitizamo yao mipya vimetolewa hususan miaka ya hivi karibuni baada ya kuanzishwa kwa matbaa yao ya Darusalaam miaka ya tisini, Inshallah tutakuja kulibainisha hili la kuhariri vitabu vya Ahlul Sunnah wal Jamaa tukijaaliwa kwenye makala zijazo .Hii inatufanya kuwa makini sana na vitabu vinavyoenezwa bure kupotosha Aqidah swahihi ya Ahlul Sunnah wal Jamaa na kuletewa Aqidah za Kiyahudi na Kinaswara kwa kisingizio cha kufuata Quraan na Sunnah na watangu wema.
Kisa kingine kimesimuliwa na Bayhaqi..... ..:
Imesimuliwa toka kwa mtunza hazina wa Umar R.A ya kuwa watu walikumbwa na ukame wakati wa utawala wa Sayidna Umar R.A

Alikwenda mmoja katika jamaa kwenye kaburi la Mtume S.A.W na akasema ‘’…..Yaa Rasuwlu –Allah tufanyie uombezi kwa Allah kwa Umma wako, hakika umma wako unaangamia..’’’ ..Baadae Mtume alimtokea yule jamaa katika usingizi na kumpa ujumbe ampelekee Salaam zake Sayidna Umar, na mweleze kuwa itanyesha mvua, mwambie/ mweleze awe mwerevu/atumie hikma...Umar alipopelekewa ujumbe huo , akasema ewe Mola wangu sina nguvu isipokuwa zile ulonipa(Tafsiri inaweza kuwa si nzuri ila mantiqi yake imefahamika)
Ibn Kathir ambaye ni mwanafunzi wa Ibn Taymiyah amesimulia toka kwa Bayhaqi katika kitabu chake al-Bidaya wa al-nihaya na kusema isnaduhu swahih pia katika Kitabu Jami al-Masanid (1/223) - Musnad Umar - amesema kuwa "Isnaduhu Jayyid Qawi:!!!
Swali letu je huyu Swahaba alikuwa akifanya Shirk wakati wa Sayidna Umar?Na je Sayidna Umar aliwaachia tu watu wafanye shirk watakavyo kama leo hii tuimbishwaavyo na watu wenye kuwakemea watu wanaotaka kufanya Tawasul na kuomba Dua mbele za qabr la Mtume swalallahu aleihi wa salaam kwa ufaham wa Masalaf?
Hawa watu wanampinga hata mwanachuoni wao wenyewe (Ibn Kathir) na kauli ya inatoka kwa mwanachuoni anayetegemewa na skuli ya wanaojiita Kisalafiya ambaye ni mwanafunzi wa Ibn Taymiyah..Ibn Kathir hakuwahi kusema kuomba kwenye kaburi la Mtume ni shirk wala Sayidna Umar Radhi-allahu anhu hakuwahi kuleta madai haya mageni na hii ni dalili tosha kuwa Masalaf hawakuona Shirk kuomba kupitia kaburi la Mtume (S.A.W) kama inavyodaiwa na watu hawa wapya wenye mrengo mpya wa Kiisilamu ambao umejaa mashaka mrengo huo
wanaopinga mas'ala haya yaani wenye kujiita Masalafiyah husema kuwa kitendo cha kumjia Mtume s.a.w kimekusudiwa katika zama zilopita, yaani wakati alipokua hai kati ya maswahaba zake.. na hii ni kuweka taqyiid bila dalili, Allaah s.w hakusema wakakujia ukiwa hai, kisha fi’il ya jaauka imekuja kwa siyaaq ya shart kama wanavyosema wana lugha, yani imetanguliwa na idh ambayo ni ya sharti, na inavyojulika katika lugha kua fiil ikija katika siyaaq ya sharti hua ina maana ya U’muum, yani kukusanya, kwa hivyo basi inakusanya kila wakati, sawa zama zake ama hizi ama hata zama zitakazokuja bali fiil kuja baada ya shart ndio sampuli kubwa ya u’muum kama alivotaja mwenye irshaad alfuhuul lakusikitisha ni pale Sheykh Uthaymiin alipojitetea na hoja ambayo ni ya ajabu na hoja dhaifu kushinda hata nyumba ya buibui aliposema katika aya imekuja idh na wala haikuja idhaa, na imezoeleka katika lugha ya kiarabu ikija idh hua inakusudiwa wakati uliopita!!!! kama alivyonukuu maneno haya mwenye kitabu فتاوى مهمة لعموم الأمة , na kitendo hiki kinajulisha kua mtu anapotaka kunusuru fikra na mtizamo wake hua hata hatizami kwa uzuri hoja zake! kwani idh katika Qur'an imetumika kwa maana ya zama zitakazokuja (mustakbal) na ni katika aya zaidi ya tatu, kwa mfano: (( وَلَوْ تَرَى إِذْ فَزِعُوا فَلا فَوْتَ)) (سبأ: من الآية51) (( وَلَوْ تَرَى إِذْ وُقِفُوا عَلَى النَّارِ )) (الأنعام: من الآية27) ((وَلَوْ تَرَى إِذِ الظَّالِمُونَ فِي غَمَرَاتِ الْمَوْتِ )) (الأنعام: من الآية93) (( وَلَوْ تَرَى إِذِ الْمُجْرِمُونَ نَاكِسُو رُؤُوسِهِمْ عِنْدَ رَبِّهِمْ)) (السجدة: من الآية12).
Suala la Salaam kwa Mtume swalallahu aleihi wa Salaam kwa watu waendao Hijjah na kumzuru Mtume S.A.W
Katika vita vya yarmuk kuna kijana alipokua anaenda kupambana na adui wakiroma(Rumi) akamwambia Abu Ubayda: Je huna haja yoyote kwa Mtume s.a.w? Abu Ubayda akalia sana , kisha akamwambia mpe salamu zangu na umwambie tumepata kile alochotuahidi mola wetu na kujua ndio haki. sasa huyu ni swahaba anatuma salamu kwa Mtume S..A.W baada ya kufariki dunia, huyo anaekataa ni nani?!!!! kisha hii ni salamu ya mtu aenda kufa? yaani maiti apewa salamu, vp aliehai isiwezekane?!!Je hali ya mtu iko vipi kaburini kwake?
Ikitokea mtu kamuomba mwenzake kumtolea Salaam kwa Mtume Swalallahu aleihi wa salaam kwenye kaburi lake basin a aseme As-Salamu `alayka ya Rasul Allah min Fulan(Taja jina la alokuagiza/Aliyekuomba kumtolea salaam) ibn Fulan (na Ubini wake) kasha amtolee salaa Sayidna AbubakarAs-Salamu `alayka ya Aba Bakrin safiyya rasulillahi wa thaniyahu fi al-ghari, jazakallahu `an ummat al-nabiyyi khayran, Kisha amtolee salaam Umar kwa kusema, : As-salamu `alayka ya `umara a`azz allahu bika al-islam, jazak allahu `an ummati muhammadin khayran
Kisha arudi kwenye sehemu yake ya mwanzo yaani mbele za Mtume swalallahu aleihi wa Salaam na amuelekee na kumfanya Mtume swalallahu aleihi wa salaam kama wasila wake(fa yatawassalu bihi fi haqqi nafsihi), na afanye kuomba Uombezi kwa Mtume swalallahu aleihi wa Salaam (wa yatashaffa`u bihi ila rabbihi subhanahu wa ta`ala), nah ii yapendeza kusema kama vile alivyosema yule Beudi wa kisa cha Utb kama tulivyokielezea

Nini maana ya Tawassul Kupitia Kwa Waja wema?Je wale wenye kujiitakidi na kufuata Twariqah wanaabudu Makaburi kama inavyodaiwa?
Imam Al Suyutwi anaeleza katika Tarikh al-Khulafa' (Beirut, 1992 Ahmad Faris .UK. 140):
Mwaka wa 17 Hijiriyah , mwaka ambao Sayidna Umar aliupanua msikiti wa Mtume S.A.W
Mwaka huo huo kulikuwa na ukame umetawala Hijaz.Na mwaka huu ukaitwa mwaka wa Ukame
Umar alifanya Maombi ya Mvua kwa kupitia Al-Abbas.

Ibn Sa`d anasimulia kutoka kwa [Swahabi] Niyar al-Aslami ya kuwa `Umar alipokuwa akienda kufanya Dua ya Mvua alitoka akiwa amevaa jubba la Mtume S.A.W
. Ibn `Awn Anasimulia kuwa Umar R.A aliushika mkono wa al-`Abbas's na kuinua juu na huku akisema maneno haya ‘’Ewe Mola tunajikurubisha kwako kupitia Ami yake Mtume Muhammad S.A.W utuondolee ukame na kutuletea Mvua, kasha akamwambia Al Abbas Yaa Abu Fadhl Qum....(simama ufanye kuomba)

Imesimuliwa katika Al-Bukari toka kwa Anas ya kuwa yeyote Yule atakayedhani kuwa Sayidna Umar alitumia Wasila wa Al-Abbass na sio Wasila wa Mtume basi utashi wake una walakini ati kwa kuwa mtume S.A.W amekufa na Al-Abbass yuko hai(Al-Maliki)
Kutawassal kupitia kwa waja wema ni mwenendo wa maimamu na maulamaa wakubwa wa Ahlul Sunnah wal Jamaa, na sisi hushangazwa sana na hawa ndugu zetu wenye kukataa jambo hili na hata kuliita Ibada za makaburi au kuabudu Masharifu na waja wema ambapo Shekhe wao mkubwa Muhammad ibn Abdil wahhaab amelikubali jambo hili alipotaja katika majmuuul Fatawa qism yatatu kurasa ya 68: anaetaka kuomba aseme :nakuomba kwa Mtume wako ama kwa mitume wako ama kwa waja wako wema, ama akusudie kaburi linalojulikana aw ghayrahu, aombe hapo kwa hilo kaburi, lakini amuombe Allaah na wala asimuombe mwengine!!!Haya ni maneno ya Sheikhe lao Muhammad Abdulwahab mwanzilishi wa harakati hizi tuzionazo za kupinga kila kitu katika Sunnah na misimamo ya Ahlul Sunnah wal Jamaa
Tunasoma kutoka kwa Shaykhul Qurraa ibnul Jazari asema katika kitabu chake alhinul HASWIIN: وجرب استجابة الدعاء عند قبور الصالحين na imejaribiwa na kukubaliwa dua katika makaburi ya wema. Akasema tena katika alkhayraatul hisaan: imam shafi alikua akitawassal kupitia kwa Abu Hanifa, alikua akija katika kaburi lake akimsalimia na akiswali pale.

Na imam dhahabi katika tadhkiratul huffaadh, katika kumueleza swaleh ibn Ahmad attamimy alhamdani alsimsari akasema: hakika dua katika kaburi lake ni yenye kutakabaliwa. haya ni maneno ya imam Dhahabi mwanafunzi wa ibnu taymiyah ambao wenye kufuata mrengo wao huyapinga mambo haya
Na Al-Imam Subki katika Twabaqaat ush -shaafiiyyah katika kumueleza Imam Ibnu fawrak, asema: hakika kaburi la ibnu fawr huko Hiira huombwa Mungu mvua kwa kutawassal nalo, na dua ni yenye kujibiwa katika kaburi lake!

Imam Ibnu Rajab alHanbali asema: amali huzidi daraja na thawabu kwa mambo matatu, utukufu wa zama, utukufu wa sehemu na utukufu wa hali ya mwenye kufanya hio amali. mfano wa yakwanza ni amali katika mwezi wa ramadhani hua na daraja tafauti ...na siku za kawaida ndio faradhi ikawa kama faradhi 70 ama mfano wa yapili ni kuswali Makkah, swala moja pale ni kama swala laki sehemu zengine... na mfano wa yatatu ni amali kutoka kwa ikhlaas si sawa na amali bila ikhlaas. Maulamaa wa Ahlul Sunnah wal Jamaa walipofahamu maana hizi ndipo wakatambua daraja ya sehemu zilozikwa mawalii na waja wema, ndio unapata hapo juu nimeashiria kua wanasema dua katika kaburi la flani ni yenye kukubaliwa kwa hivyo mtu anapokwenda kwa kaburi la walii hua anataka ile utukufu wa sehemu ile kwani dua katika nyumba si sawa na dua katika msikiti na dua katika sehemu chafu si sawa na dua katika nyumba.
Makala hii imetayarishwa na Sidi Mbarak Ahmed Aweis Al-Azhari(Cairo)

Rejea:
al-Adhkar cha Nawawi
al-Adhkar cha Nawawi
Ash-Shifa Qadi Iyad
"al-Ighatha bi adillat al-istighatha cha As-Sayid Hassan ibn Ali al-Saqqaf al-Husayni al-Shafi'I
Muthir Al-Gharam Al-Sakin Ila Ashraf Al-Amakin cha Ibn al-Jawzi
Kwa makala zaidi na Video kwa Kiswahili tafadhali tembelea
http://twariqah.blogspot.co.uk/
Kwa Niaba ya Kikundi cha Vijana wa Kitwariqah Africa Mashariki(Followers of Tariqah Alawiyah East Africa(Facebook group)

No comments:
Post a Comment