Saturday, January 19, 2013

MISIKITI YA MADINA WALIYOVUNJA MAWAHABI


Bismillahi Rahmani Rahiim

Ifuatayo ni baadhi ya misikiti iliyovunjwa na Mawahabi katika mji wa Madina.

Masjid Bany Quraydhwa:
Katika mji wa Madina kulikua na msikiti unaojulikana kwa jina ( Masjib bany quraydhwa ), umepewa jina hilo kwasababu Mtume (s.a.w) aliswali sehemu hiyo alipokua amewazunguka Banuu Quraydhwa.

Na ametaja Ibnu Shabah na Ibnu Najjaar na Alhaythamy na wengineo sehemu ya huo msikiti, na kisa cha Mtume (s.a.w) kuswali katika hio sehemu ni mashuhuri kama ilivyo kuja katika hadithi ya Abu Said Alkhudury (r.a.3), kimepokewa na Imam Bukhary na Imam Muslim.



Ametaja Ibnu Shabah na Ibnu Najjaar kua Sayyidna Omar Ibn Abdil'aziz ndie aliujenga huo msikiti wakati alipoku ni waali wa Madina ( 87-91h ), katika sehemu aliyoswali Mtume (s.a.w) alipokua anapigana na Bany Quraydhwa.
Msikiti huu ulibaki kuswaliwa maqarne na maqarne, na umepitia mabadiliko mengi, kila ukidhoofika ulikua unatengenezwa, mpaka kuja kuvunjwa mwezi wa Rabeeul Awwal mwaka wa 1422h, umevunjwa na idara ya waqfu Madina!

Masjid Ali Aluraydhwi:
Katika misikiti ya kitarekhe iliyovunjwa pia katika mji wa Madina ni msikiti wa Imam Ali Aluraydhwi, ulikua unapatikana katika kijiji ambacho kipo nje ya Madina kwa maili nne, aliishi katika kijiji hicho Abul Hasan Ali ibn Ja'far Asswaadiq bin Muhammad Albaaqir (148-210h), na yeye ni mmoja katika wajukuu wa Mtume (s.a.w) na kipande chake, na alikua ni katika maimamu wa ahlussunna rahma za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.

Huyu imam amesifiwa na Ibnul Imaad na Dhahabi na Alyaafi'i kua ni imamu katika elimu, mcha Mungu, mwingi wa ibada na mkarimu. Na alikua ni bwana wa watu wake katika banu Hashim, mpaka akaitwa Abul Ashraaf, na alikua amezikwa katika kijiji hicho.
Ulivunjwa msikiti huu na kufukuliwa kaburi la huyu Imam na wengineo siku ya jumanne na jumatano mwezi wa sita mwaka wa 1423h!

Masjid Alkhalifa Abubakr Asswiddeeq:
Katika sehemu za vita vya khandaq maeneo ya jabali sal3 kulikua na msikiti uliojulikana kama masjid Alkhalifa Abubakr Asswiddeeq (r.a.3), swahaba wa Mtume (s.a.w) Amenukuu alustaadh Ali Hafidh katika kitabu chake ( فصول من تاريخ المدينة المنورة) kua mtume (s.a.w) aliswali hapo.
Na ametaja khabari za huu msikiti mwana tarekhe wa madina Ibn Shabah, ulikua unaswali msikiti huu maqarne na maqarne, kutoka wakati wa dola ya umawy mpaka wakati wa dola ya uthmany, lakini la kushangaza sasa katika sehemu hio kuna mashini ya ATM!
Twahitajia kujuzwa ni katika fiqhi gani yafaa kuvunja msikiti wa waqfu na kuweka sehemu yake mashini ya ATM?!

Masjid Baqee3:
Ndani ya ukuta wa Baqee3 upande wa magharibi mwa kaburi la Sayyidna Aqeel na makaburi ya mama wa waumini kulikua na msikiti wa Baqee3, na ulijulikana pia kwa jina la masjid Ubay bin Ka'b. Amepokea mwana tarekhe wa Madina IBn Shabah kua Mtume (s.a.w) aliswali ndani yake mara nyingi. Ulikua umeharibika msikiti huu mpaka wakawa wafukuaji huja wakahifadhi vyombo vyao hapo, mpaka watawala wa Uthmany walipoamua kuutengeneza na kujenga mihrabu yake ukarudi kua mzuri.

Lakini leo hii upo wapi? mbona hatuoni athari ya huo msikiti baqee3? bila shaka umebomolewa.

Masjid Bilaal: 
Katika maeneo ya jabali linalo julikana kama Abu Qays kulikua na msikiti unaoitwa masjid Bilaal, msikiti huu haupo kwa sasa, bali kunapatikana majumba ya kisasa... subhanallaah! msikiti wa swahaba wavunjwa kwa ajili ya kujenga nyumba ya kisasa!!!

Anaerudi katika kitabu ( تاريخ معالم المدينة ) cha Sayyid Ahmad Alkhayari, na kitabu ( فصول من تاريخ المدينة المنورة ) cha Alustaadh Ali Hafidh na venginevyo katika vitabu vilotungwa kueleza tarekhe ya Madina, atapata majina mengi ya misikiti na majumba, kama nyumba ya Abu Ayyuub Al'answari sehemu aliposhukia Mtume s.a.w alipofika Madina, na sehemu nyenginezo ambazo zilikuepo mpaka zama za karibuni, lakini kwa sasa hazipatikani tena! zimevunjwa kwa madai ya kuzuia shirki! ni kama maulamaa wote walopita sehemu za hijazi kati ya waloenda kusoma na waloenda kutekeleza ibada ya hajj hawakuyaona hayo wala hawakuitisha ya vunjwe! tusishangae hata tukiambiwa hao maulamaa pia walikua na itikadi ya kishirikina kwa kutukuza sehemu hizo.
Hawakutosheka na kuvuja hiyo misikiti! wametaka pia kutia mikono yao katika msikiti wa Mtume s.a.w!!!

Albani katika kitabu chake ( مناسك الحج والعمرة ) chapa ya nne kurasa ya 60-61 asema: katika bid'a ziliopo Madina ni kaburi la Mtume (s.a.w) kubakishwa ndani ya msikiti!!!
Na katika kitabu chake ( تحذير الساجد من اتخاذ القبور مساجد ) ametaka qubba la Mtume (s.a.w) livunjwe.
Naye Muqbil Alwaadi'i katika risala yake ( حكم القبة ) kurasa ya 265: walitaka ndugu zama za Abdulaziz walipoingia Madina walitaka kulivunja qubba, na yaret wangekua wamefanya hilo!!!
Mungu aunusuru ummah na hawa makhawarij na fikra zao potofu.

Imeandaliwa na FTAEA.
Wanatwariqa Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment