Monday, January 30, 2012

Al-Qaswidatu Mudhwariyah Fiy Swalat 3ala Khairul Bariyah



Mawlāya šalli wa sallim dāiman abadan
 'Alā Ĥabībika Khayril khalqi kullihim

Yā Rabbi šalli ‘alāl Mukhtāri min Muđarin
wal Anbiyā wa jamī’ir Rusli mā dhukirū


Wa šalli Rabbi ‘alāl Hādī wa Shī’atihi
wa Šaĥbihi man li ťayyid Dīni qad nasharū

Sunday, January 29, 2012

Sherehe za uhuru Zanzibar, 1963

December 1963, siku ya sherehe za uhuru wa Zanzibar. 

Habib Umar bin Sumayt
  akiwa mstari wa mbele kwa heshima, nyuma (kwenye kiti) ni Qadhi mkuu, Shaykh Abdallah Saleh al-Farsi, ambaye alikuwa  mwanafunzi mkuu wa Habib Umar bin Sumayt.

1962: Jumuiya ya Waislamu Mnazi Mmoja

Picha ya Ukumbusho, iliyopigwa Dar-es-Salaam 1962, mbele ya Jumuiya ya Waislamu Mnazi Moja DSM, kwa ajili ya kuweka jiwe la Msingi la Masjid Kitumbini (Msikiti Mkuu wa Ijumaa DSM), ambapo Habib Umar na ujumbe wake kutoka Zanzibar na Mombasa walkwenda kufanya shguhuli hiyo.

Picha ya pamoja ya mashaykh (1962)

Habib Umar bin Sumayt na Habib Ahmad bin Hussayn Ibn Shaykh Abi Bakr bin Salim walipomtembelea Balozi Abbas Syks, nyumbani kwake 1962, baada ya kuweka jiwe la msingi la Masjid Kitumbini, DSM. 

Baadhi ya majina ya waliomo katika picha hii ni kama ifuatavyo: 1. Shareef Abdulkader al-Juinaydi (DSM), 2.al-'Allamah al-'Arif Billah Habib Ahmad bin Husayn Ibn Shaykh Abi Bakr bin Salim (znz); 3. Balozi Abbas Syks (DSM); 4. al-Allamah al-'Arif Billah Habib Umar bin Ahmad bin Sumayt (znz);5. al-'Allamah al-Fadhil Shaykh Hassan bi 'Amier (znz) Mufti wa Tanganyika; 6. al-'Allamah Habib Hamid Mansab Ibn Shaykh Abi Bakr bin Salim (znz); 7; al-'Allamah Sayyid Ali Badawi (Lamu-znz); 8. al-'Allamah Maallim Sa'id bin Ahmad (Mombasa); 9. al-Akh Muhammad 'Alwi Bu Numay (znz); 10. al-Akh Abdulwahhab (DSM) presidant of Arab Association Tanganyika; 11. Shaykh al-Fadhil Abdulkader Ba'Abbad (DSM). 12. Shaykh Qasim bin Jum'a Darwesh (DSM).

Ma Habaib wakiwa kwa Balozi Abbas Sykes (1962)

Nyota mbili kubwa za ZNZ, al-Habib al-'Allamah al-'Arif billah Sayyyid Ahmad bin Husayn Ibn Shaykh Abi Bakr bin Salim na al-Habib al-'Allama al-'Arif Billah Sayyid Umar bin Abi Bakr bin Sumyat wakiwa nje ya nyumba ya Balozi Abbas Syks (Mkuu wa Mkoa wa DSM, wakati huo-amesimama nyuma yao) walipokwenda kumtembelea nyumbani kwake DSM, baada ya kuweka jiwe la msingi la Msikitu Mkuu wa Ujumaa DSM, 1962.

Habib Umar na Habib Ahmad bin Hussayn walialikwa rasmi na Jumuiya ya Msikiti wa Ijumaa kwendakuwekajiwe la msingi la kuupanua msikiti huo na kuwa Msikiti Mkuu wa Ijumaa.

1965: Mashaykh wakiwa Sharif-Msa, Zanzibar

Mrithi wa Habib Umar bin Sumayt: al-Habib al-‘Allama Hamid Mansab alliyevaa bushti, akiwa katika picha ya pamoja kwenye shamba la Habib Umar bin Sumayt lijulikanalo kwa jina la Sharif-Msa ZNZ 1965. Baadhi ya waliyomo na majina yao, kama ifuatavyo:

1. Maallim Saleh; 2. Habib Umar bin Abdallah Mwinyi Baraka; 3. Habib Ali Badawi; 4. Habib Hamid Mansab Ibn Shaykh Abi Bakr bin Salim; 5.Haabib Abdulwahid bin Muhammad Ibn Shaykh Abi Bakr bin Salim; 6. Habib Ahmad bin Hamid Ibn Shaykh Abi Bakr bin Salim; 7. Habib Ahmad Yaasin Jamalullayl; 8. Sayyid Johari Jamallulayl; 9. Shaykh Ilyas; 10. Habib Muhammad Alwi Bunumayy; 11. Habib Umar bin Alwi Bunumayy.


Saturday, January 28, 2012

Kwanini msikiti wa Makka ukaitwa Masjid Al Haram?


SWALI:


Neno HARAM na HARAAM yana maana tofauti au ni maana moja tu (kinyume cha halali)? Does it mean "Holy/Sacred" also? Na kwanini msikiti wa Makka ukaitwa Masjid Al Haram?
----------------------------------------------------------------------------------------------

JIBU:

Bismillah, wa Sallah Allah ala Rasul Allah!