Followers of Tariqat Alawiya in East Africa [Wana-twariqa Afrika Mashariki]
As salaamu alaikum! Shukrani na sifa zote ni zake Allah [Subhanahu Wa Ta'allah]; rehma, baraka, na amani za Allah zimfikie kipenzi wetu Mtume Muhammad [Sallalahu alayhi wasallam], ahli zake, swahaba wake, na wanaomfuata. Dhumuni la Blog hii ni kukumbushana, kuelimishana na kusambaza mafunzo ya ilm tasawwuf/tazkiyah, iliyojengeka juu ya msingi wa Qur'an na Sunnah haswa kwa kufuatana na madhehebu ya Imam Shafii.
Search This Blog
Sunday, July 6, 2014
SWAUM KWA MTAZAMO WA WANAVYUONI WA TAZKIYAH
بسم الله و الحمد لله .
Tungependa kuangaziya Ibada ya Funga(Swaum) kwa mtazamo na fikra za Wanavyuoni wa Tazkiyah/Taswawwuf.
Kama wanavyuoni wa Fiqhi,Wanavyuoni wa Tazkiyah/Taswawwufwanakubaliana kuwa funga ya Ramadhani ni lazima na kadhalika ya kafara,deni n.k. na kuna za sunnah kama za Siku sita za Shawwal,Kila jumatatu na alhamisi n.k. kwao wao saum ina vigawanyo.Asema Imam Abu Hamid Muhammad bin Muhammad bin Muhammad Al-Ghazali رحمه الله katika kitabu chake IHYA ULUM DIN "Saumu ni daraja tatu, saumu ya watu wote nayo ni kutokamana na vyenye kufuturisha. saumu ya khaswa nayo ni kuzuiliya viungo visifanye madhambi na saumu ya khaswa wa khaswa nayo ni kulekeza moyo kwa Allah pekee"
wakasema tena "watu wa kawaida hufunga kwa kuwacha mufattwiraat lakini walio juu kwa daraja hufunga kwa kuwacha shahawaat(matamanio ya nafsi) na muharramaat(yaliyoharamishwa)"
Ulamaa wa Tazkiyah, mbali na Fadhwaail mbali mbali za Swaum zilizotajwa na faida za ki-afya wanataja kuwa swaum ina faida za ki-moyo nyingi.
Imam Abdullah bin Alwy bin Muhammad Al-Haddad رحمه الله katika itabu chake maarufu 'annaswaihu diniyah' asema "saumu ndiyo nguzo ya mazoezi ya nafsi na msingi wa mujahadah"
Saum kwao ni mmoja katika misingi ya kuenda kwa Allah. . تقليل الكلام والمنام و الطعا م
و الله أعلم

Saturday, January 19, 2013
MISIKITI YA MADINA WALIYOVUNJA MAWAHABI
Bismillahi Rahmani Rahiim
Ifuatayo ni baadhi ya misikiti iliyovunjwa na Mawahabi katika mji wa Madina.
Masjid Bany Quraydhwa:
Katika mji wa Madina kulikua na msikiti unaojulikana kwa jina ( Masjib bany quraydhwa ), umepewa jina hilo kwasababu Mtume (s.a.w) aliswali sehemu hiyo alipokua amewazunguka Banuu Quraydhwa.
Na ametaja Ibnu Shabah na Ibnu Najjaar na Alhaythamy na wengineo sehemu ya huo msikiti, na kisa cha Mtume (s.a.w) kuswali katika hio sehemu ni mashuhuri kama ilivyo kuja katika hadithi ya Abu Said Alkhudury (r.a.3), kimepokewa na Imam Bukhary na Imam Muslim.
Sunday, January 6, 2013
Kwanini Tunasherehekea Mawlid?
SABABU ISHIRINI NA TANO ZINAZOMFANYA MUISLAMU ASHEREHEKEE MAZAZI YA MTUME (Swalallahu aleihi wa Salaam)
1: Mawlid ni kuonesha kumfurahikia Mtume (Swalallahu aleihi wa salaam), na kufurahikia mazazi ya Mtume swalallahu aleihi wa salaam kulimnufaisha kafiri, jee sisi waislamu?! na hio ni dalili aloitumia Ibnu hajar katika fathul bary v9 p145 aliposema:
وذكر السهيلي أن العباس بن عبد المطلب رضي الله عنه قال : لما مات أبو لهب رأيته في منامي بعد حول في شر حال فقال ما لقيت بعدكم راحة الا أن العذاب يخفف عني كل يوم اثنين قال وذلك أن النبي صلى الله عليه وسلم ولد يوم الإثنين وكانت ثويبة بشرت أبا لهب بمولده فاعتقها .
Thursday, November 1, 2012
Monday, October 29, 2012
Kumzuru Rasul'Allah (s.a.w) na Ku-tawassal kupitia kaburi lake.
Kuzuru Kaburi La Rasul'Allah (S.A.W) na Ku-tawasal kupitia kaburi la Mtume Swalallahu aleihi wa salaam
Kuzuri kaburi la Mtume s.a.w ni katika manduubaat zilotiliwa mkazo zaidi, bali kwa baadhi ya maulamaa ni karibu na wajibu, bali kwa madhehebu ya dhwahiriya ( moja katika madhehebu ya fiqhi ) ni wajib..
ndio tunamuona Imam Nawawi katika almajmuua anasema: واعلم ان زيارة قبر النبي صلى الله عليه وسلم من أهم القربات وانجح المساعي ..., فإذا انصرف الحجاج والمعتمرون من مكة استحب لهم استحبابا مؤكدا ان يتوجهوا لزيارته صلى الله عليه وسلم وينوي الزائر من الزيارة التقرب وشد الرحل والصلاة فيه

Na imam ibnu Qudaamah asema katika almughni : وإذا فرغ من الحج استحب له زيارة قبر النبي صلى الله عليه وسلم وقبر صاحبيه
Subscribe to:
Posts (Atom)