Swali:
Je ni nini maana ya ALAL BADRI?
Je kuna aina ngapi za ALAL BADRI?
Je ktk dini inaruhusiwa kufanya/kusoma ALAL BADRI?
Jibu:
Jina sahihi ni Ahlul Badr, yaani watu wa Badr. Hawa ni maswahaba (R.A) waliopigana vita vya Badr na kuleta ushindi kwa waislam mwezi wa Ramadhan, tarehe 17, Mwaka 2 (AH). Idadi yao ni kati ya 305
(ibn Sa'd, Tabaqat 2:11) na 319 (Muslim, Sahih, al-Jihad wal-Siyar, al-imdad bil-mala’ika fi ghazwat Badr). Ibn Ishaq asema walikuwa 314 (Sira 1:317). Kati yao walikuwepo muhajirun zaidi ya 60 na Ansar zaidi ya 240 (Bukhari, Sahih, Maghazi, `iddat ashab Badr) Jeshi hilo dogo tu kwa idadi liliwashinda makafiri waliokaribia elfu. Hawa masahaba wote walioshiriki katika vita hiyo mtume Muhammad (S.A.W) amesema ni waja wa peponi.
Ama kuhusu dua Asma ahlul Badr ni ku-tawassul kwa daraja ya Mtume (S.A.W) na waja wema, kwa hakika hao wote ni katika watu wa daraja ya juu na ni watu wa peponi. Wanaopinga Tawassul kwa ujumla watapinga Dua Asma Ahlul Badr, kwa kuwa hii ni Tawassul. Anaombwa Allah kwa kujikurubisha mja wake kupitia Mtume (S.A.W) na daraja ya Maswahaba hawa wema ambao wanatajwa mmoja baada ya mwingine.
Pitia section ya "Video za Kiswahili" tafuta mada ya Tawassul kwa ufafanuzi zaidi.
No comments:
Post a Comment