Swali:
Nini hukmu ya wasiokuwa waislam wanaopigana (alongside) au kushirikiana kwa namna moja au nyingine na muslims katika jihad dhidi ya maadui wa waislam?
Jibu:
Hakuna ubaya kwa asiyekuwa Mwislamu kujitolea au kushirikiana na Waislamu, katika jihadi dhidi ya maadui wa Waislamu – iwapo Waislamu wenyewe hawana mashaka au wasiwasi naye na wakawa
wanahitajia msaada wake. Ama kuhusu thawabu za Jihadi kwa mtu kama huyo, basi malipo yake atayapata duniani na si akhera, kama zinavyosema aya kadhaa za Qur'ani na hadithi za Mtume (SAW) Mwenyezi Mungu, kuhusu mema ya kafiri, anasema:
wanahitajia msaada wake. Ama kuhusu thawabu za Jihadi kwa mtu kama huyo, basi malipo yake atayapata duniani na si akhera, kama zinavyosema aya kadhaa za Qur'ani na hadithi za Mtume (SAW) Mwenyezi Mungu, kuhusu mema ya kafiri, anasema:
: وَقَدِمْنَا إِلَى مَا عَمِلُوا مِنْ عَمَلٍ فَجَعَلْنَاهُ هَبَاء مَّنثُورًا {الفرقان:23}
“ Na tutayaleta yale waliyo yatenda katika vitendo vyao kwa kuyafanya yawe mavumbi yaliyo tawanyika”. [Al-Furqan: 23]
Wakati huo huo, Moja ya Sifa kubwa ya Mwenyezi Mungu ni uadilifu na Mwenyezi Mungu anasema إن الله لايضيع أاجر المحسنين “Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa watenda mema!”
Hali kadhalika, katika Surat al-Zilzalah, Mwenyezi Mungu anasema:
“Itakapo tetemeshwa ardhi mtetemeko wake! Na itakapo tema ardhi mizigo yake! Na mtu akasema: Kuna nini?! Siku hiyo itasimulia (ardhi) maelezo yake. Kwa sababu Mola wake ameifunulia (kufanya hivyo). Siku hiyo watu watatoka kwa mifarakano wakaoneshwa vitendo vyao! Basi anaye tena chembe ya wema, atauona! Na anaye tenda chembe ya ouvu atauona”.
Kwa maana hiyo, hakuna amali ya mwana-adamu ambayo haina malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Ila, wale wataolipwa wema siku ya Qiyama kwa mema yao waliyoyatenda duniani ni wale waliomuamini Mwenyezi Mungu S.W. tu. Wengine, malipo ya mema yao hufanywa hapa hapa duniani.
Mtume S.A.W. amesema:
: إن الله لا يظلم مؤمناً حسنة يعطى بها في الدنيا ويجزى بها في الآخرة، وأما الكافر فيطعم بحسنات ما عمل بها لله في الدنيا حتى إذا أفضى إلى الآخرة لم تكن له حسنة يجزى بها. رواه مسلم
“Mwenyezi Mungu hamdhulumu mu’mini jema lolote; hupewa jema kwa jema hilo duniani na hulipwa jema kwa jema hilo Akhera. Ama kafiri, basi hulipwa, kwa jema alilolifanya, duniani, kiasi kwamba afikapo Akhera huwa hakuna jema kwake yeye kulipwa”. [Muslim]
Na maneno hayo ya Bwana Mtume S.A.W., ndiyo ufafanuzi wa aya zinazosema kuwa Amali njema za makafiri zitageuzwa siku ya Qiyama kuwa vumbi tupu, yaani hazitawafaa huko; kwa sababu Mwenyezi Mungu, S.W. hapokei amali yoyote ile isipokuwa ile ambayo swafi kabisa na imekusudiwa YEYE peke Yake.
Hivyo kafiri anaweza akipenda kusaidia kwa hali au kwa mali vita vya jihad, ila waislamu wanatakiwa kuwa na tahadhari kubwa katika msaada huo maana kafiri huwa ama anasaidia kimasomaso yaani kuonesha kuwa hayuko pamoja na maadui wa waislamu na uwislamu au anasaidia ili kujisaidia mwenyewe -kama wanavyo onekana siku hizi, katika maeneo mbali mbali ya WAislamu.! Msaada wake huo usiwahadae Waislamu wakaanza kumuamini na kumkabidi majukumu makubwa au nyeti na kumuingiza jikoni! Atawamaliza siku moja kama tunavyoona yanayojiri katika nchi nyingi za kiislamu hii leo na hasa Mashariki ya kati!
Wa billah alTawfiq
Dr. A. Shareef
No comments:
Post a Comment