Monday, April 2, 2012

Bukhari 1:5



Sahih Al-Bukhari: Kitabu #1, Hadith # 5

Narrated Said bin Jubair:
Ibn 'Abbas in the explanation of the statement of Allah "Move not your tongue concerning (the Quran) to make haste therewith." (75.16) said "Allah's Apostle used to bear the revelation with great trouble and used to move his lips (quickly) with the Inspiration." Ibn 'Abbas moved his lips saying, "I am moving my lips in front of you as Allah's Apostle used to move his." Said moved his lips saying: "I am moving my lips, as I saw Ibn 'Abbas moving his." Ibn 'Abbas added, "So Allah revealed 'Move not your tongue concerning (the Qur'an) to make haste therewith. It is for Us to collect it and to give you (O Muhammad) the ability to recite it (the Quran)' (75.16-17) which means that Allah will make him (the Prophet) remember the portion of the Qur'an which was revealed at that time by heart and recite it. The statement of Allah: 'And when we have recited it to you (O Muhammad through Gabriel) then you follow its (Quran) recital' (75.18) means 'listen to it and be silent.' Then it is for Us (Allah) to make it clear to you' (75.19) means 'Then it is (for Allah) to make you recite it (and its meaning will be clear by itself through your tongue). Afterwards, Allah's Apostle used to listen to Gabriel whenever he came and after his departure he used to recite it as Gabriel had recited it."

حَدَّثَنَا مُوسَى بْنُ إِسْمَاعِيلَ، قَالَ حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، قَالَ حَدَّثَنَا مُوسَى بْنُ أَبِي عَائِشَةَ، قَالَ حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ جُبَيْرٍ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، فِي قَوْلِهِ تَعَالَى {لاَ تُحَرِّكْ بِهِ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِ} قَالَ كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يُعَالِجُ مِنَ التَّنْزِيلِ شِدَّةً، وَكَانَ مِمَّا يُحَرِّكُ شَفَتَيْهِ ـ فَقَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ فَأَنَا أُحَرِّكُهُمَا لَكُمْ كَمَا كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يُحَرِّكُهُمَا. وَقَالَ سَعِيدٌ أَنَا أُحَرِّكُهُمَا كَمَا رَأَيْتُ ابْنَ عَبَّاسٍ يُحَرِّكُهُمَا. فَحَرَّكَ شَفَتَيْهِ ـ فَأَنْزَلَ اللَّهُ تَعَالَى {لاَ تُحَرِّكْ بِهِ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِ* إِنَّ عَلَيْنَا جَمْعَهُ وَقُرْآنَهُ} قَالَ جَمْعُهُ لَهُ فِي صَدْرِكَ، وَتَقْرَأَهُ {فَإِذَا قَرَأْنَاهُ فَاتَّبِعْ قُرْآنَهُ} قَالَ فَاسْتَمِعْ لَهُ وَأَنْصِتْ {ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا بَيَانَهُ} ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا أَنْ تَقْرَأَهُ. فَكَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم بَعْدَ ذَلِكَ إِذَا أَتَاهُ جِبْرِيلُ اسْتَمَعَ، فَإِذَا انْطَلَقَ جِبْرِيلُ قَرَأَهُ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم كَمَا قَرَأَهُ.

Amesimulia Said bin Jubair (r.a):
Ibn 'Abbas (r.a) katika kuelezea kauli ya Allah "Usiutikisie huu wahyi ulimi wako kwa kuufanyia haraka." (Qur'an 75:16) alisema "Mtume wa Allah (s.a.w) alikuwa akipokea wahyi huku akipatwa na shida kali na alikuwa akitikisa midomo yake (haraka) wakati wa ufunuo." Ibn Abbas (r.a) alitikisa midomo yake akisema: "Natikisa midomo yangu kama nilivyomuona Mtume wa Allah (s.a.w) alivyokuwa akitikisa yake." Ibn Abbas (r.a) akaongezea, "Kwa hiyo Allah akaleta (akafunua) 'Usiutikisie huu wahyi ulimi wako kwa kuufanyia haraka. Hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha.' [Qur'an 75:16-17] ambayo yamaanisha kwamba Allah (s.w.t) atamfanya Mtume (s.a.w) akumbuke kwa moyo sehemu ya Qur'an iliyofunuliwa wakati huo na kuisema/soma. Kauli ya Allah: 'Na Tunapo usoma (Ewe Muhammad, kupitia Jibril a.s), basi nawe fuatiliza kusoma kwake.' (75:18) yamaanisha 'usikilize na kuwa kimya'. 'Kisha ni juu Yetu kuubainisha' [75:19] yamaanisha 'Kisha ni juu ya Allah kukufanya uusome (na maana yake itabainika yenyewe kupitia ulimi wako). Baada ya hapo, Mtume wa Allah (s.aw) alikuwa akimsikiliza Jibril (s.a) wakati wowote anapokuja na baada ya kuondoka alikuwa akisema kama ambavyo Jibril (a.s) alivyosema/soma."

No comments:

Post a Comment