Thursday, January 26, 2012

Misingi ya madhehebu ya sunni

Swali:
Nini tofauti kuu za kimsingi katika fiqh ya madhhab ya Hanafi, Maliki, Shafi, na Hanbali?

Jibu:   Misingi ya madhehebu ya imam Abu hanifa:

1: Qur'an.

2: sunnah.

3: Aqwaal za maswahaba.

4: Ijmaa3.


5: Qiyaas.

6: Isti7saan.

7: 3urf.
Misingi ya madhehebu ya imam malik:

1: Qur'an.

2:Sunnah.

3: Ijmaa3.

4:Qiyaas.

5: 3amalu ahlil madina.

6: qawlus swa7aabiy.

7: Isti7saan.

8: saddudh dharaai3.

9: Istis7aab.


Misingi ya madhehebu ya imam Shafii:


1: kufuata qur'an na sunna. Na alikua akisema, "Kila hadith ya Mtume (s.a.w) ndio qawli yangu, hatakama hamjaniskia nikiisema"


2: kufuata haki. Ilikua hakuna kinachomzuia kufuata haki, wala hashughuliki na kufanya taqliid
    ama kufuata vitendo vya wana mji kama vile Imam Abu Hanifa alivokua akichukua vitendo vya
    watu wa iraq na imam malik akichukua vitendo vya watu wa Madina.

3: kutilia umuhimu aqwaal za maswahaba. Alikua akiona maswahaba wakiafiqiana katika jambo
    ni hujja. Ama inapokua qawl ni ya swahaba mmoja na wala hakuna aya wala hadith katika
    mas'ala hayo basi qawl ya huyo swahaba hua ni bora kuliko qiyaas.

4: Qiyaas. Alikua kati katika qiyaas, hakukaza kama Imam Malik wala hakulegeza kama Imam
    Abu Hanifa, na alikua akiipa daraja ya ijtihaad na akisema: al'ijtihaad alqiyaas.

‎5: kuzingatia asli ya vitu. Katika mambo yasokua na dalili alikua achukua asli ya kufaa kwa
    yenye manufaa, na asli ya kutofaa kwa vyenye kudhuru.

6: istis7aab.

7: istiqraa.

8: kichache kilosemwa katika mas'ala.

No comments:

Post a Comment