Wednesday, January 25, 2012



Sayyid Al Habib Umar bin Hafiz (Allah amhifadhi) aliulizwa:

"Tufanyeje tukiona uvivu na ukosefu moyo wa kufanya baadhi ya sunnah na nyiradi?"


Akajibu: "Mjisukume mbele kwa kujitia moyo (matumaini): mjikumbushe malipo ya amali hizo na matokeo yake (faida) katika maisha yajayo.

Ukijiona mvivu wakati mwingine usikate tamaa. Usiwache kufanya (hilo jambo) na usilicheleweshe - jirudi ufanye ulivyokuwa ukifanya, kwa kuwa ki asili, haujakamilika.

Huenda uvivu wako unakufundisha somo kubwa na muhimu. Unaweza ukakuletea/jengea udhoofu na unyenyekevu mbele ya Allah, na unaweza kukuondolea 'ujub rohoni mwako. Hii yaweza kuwa na faida zaidi kwako kuliko kufanya kitendo chenyewe"

No comments:

Post a Comment