Thursday, March 22, 2012

Bukhari, 1:1

Sahih Al Bukhari: (Kitabu#1, Hadithi#1)

Narrated 'Umar bin Al-Khattab:
I heard Allah's Apostle saying, "The reward of deeds depends upon the intentions and every person will get the reward according to what he has intended. So whoever emigrated for worldly benefits or for a woman to marry, his emigration was for what he emigrated for."

حَدَّثَنَا الْحُمَيْدِيُّ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ الزُّبَيْرِ، قَالَ حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، قَالَ حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ سَعِيدٍ الأَنْصَارِيُّ، قَالَ أَخْبَرَنِي مُحَمَّدُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ التَّيْمِيُّ، أَنَّهُ سَمِعَ عَلْقَمَةَ بْنَ وَقَّاصٍ اللَّيْثِيَّ، يَقُولُ سَمِعْتُ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ ـ رضى الله عنه ـ عَلَى الْمِنْبَرِ قَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ " إِنَّمَا الأَعْمَالُ بِالنِّيَّاتِ، وَإِنَّمَا لِكُلِّ امْرِئٍ مَا نَوَى، فَمَنْ كَانَتْ هِجْرَتُهُ إِلَى دُنْيَا يُصِيبُهَا أَوْ إِلَى امْرَأَةٍ يَنْكِحُهَا فَهِجْرَتُهُ إِلَى مَا هَاجَرَ إِلَيْهِ ".

Amesimulia 'Umar bin Al-Khattab (r.a):
Nilimsikia Mtume wa Allah (s.a.w) akisema, "Malipo ya matendo hutegemea nia na kila mja atapata malipo kutokana na alichonuia. Kwa hiyo yeyote aliyehama kwa ajili ya manufaa ya kidunia au kwa ajili ya kuoa mwanamke, basi kuhama kwake ni kwa ajili ya alichokihamia"

8 comments:

  1. Kuna walojaribu kutaka kuidho3ofisha hadithi hii kwakua hakuna alopokea kwa omar ispokua ni 3alqama, na hajapokea kwa 3alqama ispokua muhammad attaymy, na hajaipokea kwa attaymy ispokua yahya al'answary, kisha baada ya hapo ndio ikapokewa na wengi, ametaja abu qasim ibnu mandah watu 340 waloipokea kwa yahya

    ReplyDelete
  2. Hata kama imepokewa na mtu mmoja kwa daraja tatu, haimaanishi sio swahihi, kwani katika masharti ya swahih hakuna sharti la kupokewa na wengi! Na yotesha kujulisha ni swahih kupokewa na imam bukhary katika swahih yake, tena akaipanga kama hadith yakwanza.

    ReplyDelete
  3. Hivi ni dalili gani (kama ipo) inatumika katika madhehebu ya Shafi'i ku-support hoja ya kuwa kutamka nia ni sunnah?

    ReplyDelete
  4. Dalili ni hadithi ya ibnu mas3ud katika s.muslim, Mtume s.a.w alipoenda hajj alitamka nia akasema nawaytu hajjatan wa3umrah, na hajj ni ibada, na katika misingi ya sharia ni qiyaas, so imam shafi amefanya qiyaas kati ya ibada ya hajj na ibada zengine kwa kua zote ni ibada.

    ReplyDelete
  5. a.a mafhumu yangu ni kuwa kilicho nasibishwa hapa ni kila jambo la kheri lilonuiliwa na muislamu ama muumini..ikiwa ni kunuia jambo ili upate thawabu ama uepuke shari..basi ujira utakuwepo ka mola wako..na tabaruku na wenzangu wachangie shukran

    ReplyDelete
  6. Mpangilio wa imam bukhary kuna siri kubwa, ameanza swahih yake hadith hii kwa kua amali zaanza kwa nia, kisha akamalizia kwa hadithi ya mizani kuonesha kua amali zamalizikia katika mizani.

    Ma3ulamaa wanasema hadithi hii ni thuluthi ya dini, kutokamana na mafunzo mengi yaliomo ndani yake, na ndio ikapelekea ba3dhi ya ma3ulamaa kutunga kitabu kizima kusherehesha hadithi hii.

    Ikhlaas ni funzo kubwa tunalolipata katika hadithi hii, tukifanya jambo tufanye kwa ajili ya Allaah s.w, sio kwa kutaka umaarufu ama utajo ama kuonekana mjuzi ama kukimbilia dunia na shahawati zake.

    Hijra ni kutoka kwa jambo kwenda lengine, ama kutoka kwa hali na kwenda kwa hali nyengine, wala sio kugura sehemu tu! Na ndio s.omar r.a.3 akachegua mnasaba wa hijra kuanzia tarehe ya kiislamu, kutuonesha kua mu'min atakikana kila wakati agure tabia zake mbovu na marafiki waba na kila kilishokatazwa katika sharia.

    ReplyDelete
  7. Nikichangiya baada yakupata idhni kwa mashekhe zetu kwanza napenda kusema ya kuwa kawaida aya ikiteremshwa huwa kuna sababunnuzuli na yaeza ikawa hakuna vilevile na hadithi piya huwa na sababulwuruudi yani sababu yakutolewa hadithi na sababu yakutolewa hadithi hi ni kuwa swahaba mmoja alifanya hijra wakati maswahaba watoka makka kuenda madina lakini yeye alikuwa na niya yakumfuwata mwanamke na dhwahiri yake ni kuwa afanya hijra kwa niyya ya hijra basi mtume s.a.w akatowa hathi hi ilio tangulia kutajwa hapo juu. Ama tafseer ya hadithi ime tanguliya illa tu niya namna ilivo tafseeriwa katika madh'hebu ya imamu shaafi3i nikuwa haziswihi amali mpaka kwa niyya kwa madh'hebu ya imam abuhanifa hazikamiliki amali mpaka kwa niyya kwa mashafii3i ni wajibu ni nguzo.

    Nikiongezea katika niya ninini..? na sehemu yake niipii.?wakati wake ni upi?watiya vipi..? makusudio ya niya ni yapi ..?na hukmu yake na fkiri tumeitaja hapo juu...

    ‎1 niya katika lugha nikukusudiya ..nakatika sheriya nikukusudiya kitu pamoja nakutenda ulicho kikusudiya na lau ukatiya niya baada ya mdaa ukfanya kile kitu basii hiyo ni 3azma...2 ama sehemu yaniya ni moyoni kwasababu Allahu s.w.t haangali miili yenu wasuraznu lakini yuwaangaliya nyoyo zenu..nakutemka kwa niyya ya pendekezwa kwani humsaidiya katika kuhudhuriasha moyo wake ...na kama alivo tanguliya shekhe letu mbarak kuwa ime thubutu katika hadithi kujihirisha niya mtume s.a.w katika haajji ..na vilevile ime thubutu mtume s.a.w alinigiya kwa nana 3aaishah akauliza kuna kitu maana je kuna chakula nana 3aaishah akasema laa mtume akasema basi nime funga nana 3aaishah akasikiya hadithi ime pokelewa na imam muslim.Na vile vile hakuna swahaaba yeyote aliekurubiya karibu na mdomo wa Mtume s.a.w akahakikisha kuwa hakutemka niya ya swala wakati akiswal! ...3 wakati wa niyaa ni wakati ukifanya kitendo cha ibada ispokuwa saumu na zaka waeza kutanguliza kwa uzito wa kuzifuatanisha.

    ‎4. ama sampuli ya kutiya niya hutafautiyana namna inavo tafautiyana ibada zake.5 makusudiyo ya niya nikutafautisha 3aadah na ibaadah au nikuzitafautisha ibada bayna faradhi na sunna.

    Wallahu a3lam

    ReplyDelete
  8. http://www.youtube.com/watch?v=Bt_NI8raoFQ&list=PL89AE1D9E52748996&index=19&feature=plpp_video

    Umuhimu wa niya

    ReplyDelete