Wednesday, February 29, 2012

Swali kuhusu maana ya Shareef/Sharif


Swali:


Nini maana ya Shareef au Mashareef?
Je, kama ni jina mtu yeyote anaweza kumuita mtoto wake Shareef?
Je, hili ni jina tuu kama majina mengine au inamaana nyingine, au ni ukoo?

Majibu:

Sharif linatokana na Sharaf, lenye maana ya heshima au utukufu. Kwahiyo tunaweza kusema Sharif ina maana ya mheshimiwa kwa tafsiri ya moja kwa moja. Kuna usemi wa kiarabu, "Man sharrafa nafsahu fahuwa shareef" wenye maana kuwa anayejiheshimu ataheshimiwa.

Tuesday, February 28, 2012

Uganga, Unajimu, Ukahini, Uchawi, Ramli, Piga Bao...


Kutokana na kuulizwa suala hili la “ Uganga”, “ Unajimu”, “ Utabiri”, “ Ukahini”, “ Uchawi”, “ Urogaji”, “Ramli”, “Piga bao”, na kadhalika, na ubabaishaji unatolewa na baadhi ya watu kuhalalisha au kusema si haramu, inajuzu katika Uislamu na kadhalika, nimeona niongozee hapa baadhi tu ya hadithi za Mtume S.A.W. ambazo zimepokelewa na Maimamu mbali mbali katika vitabu vyao vya Hadithi na kuekewa fafanuzi mbali mbali kwamba yote hayo ni HARAMU na ni mambo yasiyokubaliwa katika Uwislamu; na kwamba majina yoyote yatayotumika au kutumiliwa katika nyanja hizo hayawezi na wala hayataweza kuhalalisha vitendo hivyo.

Sunday, February 26, 2012

Johari za Wanazuoni


~ Aliulizwa swali Sayyid Al Habib Umar bin Hafiz (Allah Amhifadhi): "Tufanyeje tukiona uvivu na ukosefu moyo wa kufanya baadhi ya sunnah na nyiradi?"


Akajibu: "Mjisukume mbele kwa kujitia moyo (matumaini): mjikumbushe malipo ya amali hizo na matokeo yake (faida) katika maisha yajayo.


Ukijiona mvivu wakati mwingine usikate tamaa. Usiwache kufanya (hilo jambo) na usilicheleweshe - jirudi ufanye ulivyokuwa ukifanya, kwa kuwa ki asili, haujakamilika.


Huenda uvivu wako unakufundisha somo kubwa na muhimu. Unaweza ukakuletea/jengea udhoofu na unyenyekevu mbele ya Allah, na unaweza kukuondolea 'ujub rohoni mwako. Hii yaweza kuwa na faida zaidi kwako kuliko kufanya kitendo chenyewe"

Johari za Wanazuoni


"Wengi hufikiri kwa kufanya Ibadah watanyookewa na mambo yao ya kidunia, mtazamo huu si sahihi na Allah hatotulipa kwa hongo za Ibadah hizi! Kuna wengine huingia kwenye dini(kaafa/kiukamilifu)baada ya kushindwa katika dunia. Mtizamo huu na Niyah hii si swahihi kwani hata kwenye dini pia watashindwa kama walivyoshindwa kwenye dunia.


Zuhd sio kuacha kitu ukitamanicho bali kutoa kitu cha thamani ulichonacho na kukipeana. Huku ndio kuwa Zahid kikweli.

Iweje Sayyidina Abubakr Sadiq (RA) asimulie hadithi chache?


Je, Unajua?!


Sayyidina Abu Bakr ndiye Swahaba aliyeishi na Mtume S.A.W. kwa muda mrerfu zaidi kuliko Maswahaba wote wengine. Na ndiye aliyeswahibiana na Mtume S.A.W. kwa muda wa uhai wake wote! Lakini, pamoja na hayo yote, ni hadithi chache sana zilizopokelewa kutoka kwake, akimnukuu Mtume S.A.W. Kwanini?!!!


Sayyidina Abu Bakr al-Siddiq R. A. ndiye mwanamume wa mwanzo kabisa kumuamini Mtume Muhammad S.A.W., mara tu baada ya kupewa utume. Aliambatana na Mtume S.A.W. wakati wote huko Makka, kwa muda wa miaka 13 na ndiye aliyefuatana naye kutoka Makka kwenda Madina. Hivyo, ndiye Swahaba wa mwanzo kabisa miongoni mwa

Swali kuhusu hadithi alizosimulia Bilal (Radhiallau anhu)...


Swali:


Asalam alaikum. Hadithi nyingi nilizoziskia anatajwa swahaba aliemsikia mtume (s.a.w) lakini sijaskia hadithi aliyopokea Bilal bin Rabbah (radhi allaahu anhu)na ndie swahaba aliekua kribu sana na mtume (s.a.w), nisaidieni na mnielimishe jambo hili tafadhalini.

Jibu:

Waalaykum salaam. Sayyidina Bilal (radhi allaahu anhu) amepokea hadithi arobaini na nne (44) na ana musnad yake (musnad Bilaal), na katika hizo kuna nne katika swahihayni.

Saturday, February 25, 2012

Injili ya Barnaba yenye thamani ya mamilioni ya Paundi za Uingereza yavumbuliwa.





  • Vatikan yataka kuiona biblia hiyo
  • Yadaiwa kuwa na umri wa millenia moja na nusu


Biblia ya siri ambayo Yesu (Nabii Isa Aeyhi Salaam) anaaminika kutabiri ujio wa Mtume Muhammad (S.A.W) ulimwenguni imezua utashi wa udadisi kutoka Vatican.

Papa Benedict XVI amedai kutaka kuona kitabu hicho chenye umri wa miaka elfu mia tano (1,500) ambacho wengi wamesema ni Injili ya Barnaba ambacho kilikuwa kimefichwa na serikali ya Uturuki kwa zaidi ya miaka kumi na mbili.

Friday, February 24, 2012

Swali kuhusu vazi la hija (ihram)...

Swali:

Je, Ihram inaruhusiwa kushona au kufunga na pini?


Jibu:


Ihram ni vazi lakuhiji. Vazi la mwanamke linaweza kushonwa kama kanzu na mtandio, kama vile mavazi anayovaa kwa kuswali. Ama mwanamume, bazi lake haliruhusiwi kushonwa. Ni shuka mbili, moja kuvaa chini na ya pili kuvaa juu. Wakati wa wote wa hija, mwanamume hatakiwi kufunika kichwa chake, mpaka baada ya

Swali kuhusu ulazima wa mawalii kwa bi harusi aliyewahi achika...

Swali:

Kuna watu wanasema mwanamke akiolewa kisha akiachika akitaka kuolewa tena basi wale mawalii zake si lazima, eti ni kweli?

Jibu:

Hadithi sahihi inasema: الأيم احق بنفسها من وليها والبكر تستأمر في نفسها وإذنها صماتها )رواه مسلم Mjane ana haki zaidi juu ya nafsi yake kuliko kuwa na walii wake, na Mwanamwari\Bikira huombwa idhini na kunyamaza kwake ndiyo kukubali kwake"

Swali kuhusu Kuapa/Kula yamini...


Maswali:


Je, nini maana ya kuapia (WALLAHI !)
Je, mtu anapoapia hivyo wakati ni kitu cha uongo inakuaje?
Nini hukmu ya mtu anaeapia kwa uongo au kwa maslahi fulani ambayo ni ya uongo!
Je, yafaa kuapia kila mara?

Majibu:

Bismillahi!
Kuapa, au Kula kiapo, au Kula Yamini, katika Uislamu, kunamaanisha “kutoa dhamana kwa mtu mwengine au watu wengine, au kumthibitishia, kwa kutumia Jina la Mwenyezi Mungu au mojawapo wa Sifa Zake, kwamba jambo fulani linaloapiwa – na ambalo halina ushahidi wazi wazi- ni kweli na sahihi kama

Swali: Kuingia msikitini na kusoma Qur'ani kwa mwenye hedhi...


Swali:

Asalam Alaykum warahmatullahi wabarakatuhu,
Jee, mwanamke akiwa kwenye hedhi anaruhusiwa kwenda msikitini au haruhusiwi?
Na jee, anafaa kusoma Quran kimoyoni au haifai?


Jibu:

Bismillah! Mwanamke awe na hedhi asiwe na hedhi, yeye si najsi. Hivyo basi, hakatazwi kuingia msikitini au kupita msikitini iwapo amejidhibiti vya kutosha ili damu isidondoke na kuangukia kwenye msikiti. Hali

Tuesday, February 21, 2012

Hatari Ya Kutoa Fatwa bila ya Ilm.

Imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya watu bila ya ilimu kujichukulia madaraka kwa kutafuta hadithi hapa na pale (siku hizi kupitia google) kisha kupitia vipande vya aya za Qur'an na kujijibia maswali na kufikia uamuzi wa mambo fulani ya kisheria.

Tena hawasiti kuwaambia hata wenzao wanaouliza swali, "Hiyo ni haraaam!" ama "Bid'ah hiyo!" au kinyume chake. Hii ni hatari, kwani wanaweza kujipotosha wenyewe na kuwapotosha wengine na kujitia motoni. Tunao wasomi wa dini waliopitia elimu zinazowaruhusu kutoa fatwa kupitia misingi inayokubalika kisheria.

Hivi leo akitokea mtu akakwambia amesoma kwenye internet dawa ya gonjwa fulani, au amesoma kitabu jinsi ya kuondoa kansa utamuachia mwili wako akutibie? Iweje umruhusu mtu acheze na dini yako katika moyo wako?

Basi Ustadh Mbarak Ahmed anatuletea mada Hatari ya kutoa fatwa bila ya elimu.

Swali kuhusu kusamehe deni la marehemu...


Swali:


Je, kama namdai mtu na akafariki nikamsamehe, baada ya siku chache ndugu zake wakanifata na kuniambia ndugu yao aliacha usia wanilipe deni langu na nikakataa wananilazimisha, Je hapo nifanyeje?

Jibu:

Kama ulimsame deni lako alipokuwa hai kumegeuza deni hilo kuwa sadaka. Umepata thawabu. Watoto wa marehemu walipogundua kuwa kuna deni, bila ya kujuwa kuwa ulishamsamehe baba yao tokea akiwa hai,

Swali kuhusu taarifa ya kuongeza mke ...


Swali:

Ikiwa mume hakumwambia mkewe kama anataka kuoa na baada ya kuoa pia hajamwambia na mwanamke ameshajua kama mumewe kaoa naye hajamuuliza mumewe na hakuna zamu mume kila siku analala kwa mke wa kwanza. Je hali hii inakubalika katika sheria ya kiislam?

Jibu:

Kumuarifu kabla siyo lazima, lakini kufanya uadilifu, ikiwa pamoja na kugawa zamu sawasawa ni LAZIMA, na hiyo inamaanisha kumjulisha baada ya kuoa ni budi. Maana hatoweza kugawa zamu sawasawa pasi na

Swali kuhusu kusoma Qunut alfajir...

Swali:

Asalam aleikum, nini hukumu ya kufanya Kunut kila swala ya asubuhi kama wanavyofanya katika misikiti  mingi ya East Africa (hususan Ma-Shafi)?


Jibu:


Waalaikum salaam. Katika masail yenye kuwatatiza baadhi ya watu ni mas'ala ya Qunut, na ilifika daraja mpaka kupiga wanaoleta qunut wakiwa ndani ya swala na hilo limetokea malindi kenya. Kuna risala naiandaa inshaallaah karibuni itakua tayari, ispokua nitayaashiria kwa mukhtasar hapa kwa kua nimeombwa hilo. Qunuut tunaizungumzia hapa ni ya kila siku katika swala ya alfajiri wala sio ya witri.

Thursday, February 16, 2012

Kongamano ONLINE: Kusherehekea Rahma...

Organization ya SEEKERS GUIDANCE wakishirikiana na CELEBRATE MERCY.COM wanawaletea kongamano moja kwa moja kupitia mtandao (LIVE),



Kumhusu Kipenzi wetu:
Mtume Muhammad (Salallahu alayhi wa salam) 
Mafunzo katika maisha yake ya ndoa


Siku na mida

Friday, February 17th at 9:00 PM EST (New York Time) 
Sunday, February 19th at 8:30 PM EST (New York Time) 
Thursday, February 23 at 8:00 PM EST (New York Time) 
Saturday, February 25 at 2:00 PM EST (New York Time) 
Saturday, February 25 at 8:30 PM EST (New York Time) 
Sunday, February 26 at 12:00 PM EST (New York Time) 

 Wazungumzaji ni pamoja na:

Al Habib Ali Al Jifri
Imama Suhaib Webb
Dr. Tariq Ramadhan
Nouman Ali Khan
Shaykh Yahya Rhodus
Imam Zaid Shakir
Na wengine wengi!

*Jisajili mapema iwezekanavyo, click hapa.
Utahitaji kujaza JINA, LOCATION, na E-MAIL mahali hapa kuhudhuria mkutano huu online.
Usikose kesho na siku zitakazofuata (tazama ratiba) Inshaa'Allah.



Sunday, February 12, 2012

Maulidi Mlango wa Papa..

Habari tulizopata kuhusiana na yale Maulidi yaloyokuwa yafanyike msikiti wa Mlango wa Papa, Mombasa yamepangwa kufanyika siku ya leo Jumatatu inshaa Allah.

Tunaomba Mungu leo kuwe na amani.
Amin.

Don't settle for mediocrity, aim higher!



"A muslim when he endeavors to do something, he seeks to excell in (perfect) it"

 Bismillahi Rahmani Rahim 
 'Allathee khalaqal Mawta wal Hayaata li-yabluwakum 'ayyukum 'ahsanu 'amalaa: Wahuwal Azeezu-ghafuur"

Swali kuhusu Falaki Na Hukumu Yake...

Swali:

Je, Falaki ni nini na ni nini hukumu yake?

------------------------------------------------------------------------------------------
Jibu:

Swali haliko wazi. Ni vyema mtu akiuliza swali afafanue wazi wazi anauliza kuhusu nini khasa?

Ikiwa swali ni kuhusu Elimu ya Falaki, ambayo kwa Kiingereza ni Astronomy, pamoja na matawi yake mengine, kama vile Astrophysics (Fisikia ya Umbile za Falaki); Astrometry (Fisikia ya Mienendo na Miale ya Sayari); Cosmology (Elimu ya asili na maumbile ya Ombwe\Anga la juu) na kadhalika –mingoni mwake Elimu ya Utabiri wa hali ya hewa; ambayo ni Elimu ya maumbile ya Ulimwengu na Dunia yetu hii – Nyota, Sayari: kama Jua na Mwezi, Mbingu- inayoelezea na kuchambua maumbile ya vitu hivi, mienendo yake, tabia zake na mahusiano yake na kadhalika- basi Elimu hiyo ni halali kabisa. Bali, naweza kusema kuwa, kama zilivyo Elimu nyengine, ni Fardhi Kifaya kwa Waislamu. Yaani, iwapo patatokea kuwa hakuna mtu aliyesomea Elimu hiyo katika Jamii fulani ya Waislamu, basi Waislamu wale watakuwa wamekosea na wanaweza kupata dhambi kwa Mwenyezi Mungu, S.W.

Friday, February 10, 2012

MAWAHABI wazua vurugu msikitini - Mombasa

Inna Lillahi Wa inna Ilayhi Rajiuun


Habari kutoka Mombasa, Kenya zinasema kuwa usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa, kundi la waisilamu wenye kufuata mtizamo wa ki-Wahabi walifika katika msikiti wa Mlango Wa Papa ambamo palikuwa pameandaliwa sherehe za Maulid kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad [Sallallahu aleihi wa sallam]-rehma kwa walimwengu wote, na kuzuia waumini kufanya sherehe hizo.

Ni desturi kuwa kila Alhamisi ya tatu ya mwezi wa Rabi al Awwal husherehekewa Maulid katika msikiti huo, bahati mbaya msikiti huo umekuwa na mvutano baina ya waumini wa Ahlu sunnah wal jama'a wanaochukulia Maulid kama jambo jema (bid'ah njema), na Mawahabi/"Salafi" ambao huona kama kusherehekea mazazi ya Mtume ni uzushi na upotofu. Ndugu mmoja (Jina linahifadhiwa) aliyeshuhudia mvutano huo anaeleza: "Sasa mimi nilipofika baada kuswali isha nilikuta fujo ilikua imeanza. Hawa wahabi walijua leo kuna maulidi kwa hivyo walikuja hapo msikitini kwanza swalat asr kwa singizio kuwa wako na ijtima'a. Basi ilipofika 7:25pm hivi ndio fujo ikaanza. Hawa watu walikua tayari wamejiandaa na mitaimbo, bakora na visu. Wakaanza fujo mara wakajifungia wao peke yao ndani ya msikiti!"

Taarifa tulizopokea zinaeleza kuwa watu kadhaa wamejeruhiwa katika vurugu hizo, akiwemo mtoto wa aliyekuwa balozi wa Kenya nchini Saudi Arabia.

Akiendelea kutupa ripoti zaidi, Ndugu yetu aliyekuwepo katika tukio amesema: "Watu wamepigana kwa mawe,mimi binafsi nimepigwa mtimbo katika hali ya kufungua mlango waliokua wamejifungia ndani. Alhamdulillah! sikuumia sana, maumivu tu kidogo na alama. Mimi nimeondoka nimecha bado watu wanaendelea, aibu....hata sijui twaelekea wapi jamani."

Mungu atunusuru na fitna, na atuongoze na kutujaalia amani. Amin,

Thursday, February 9, 2012

Prayer For Syria...

The people of Syria are being slaughtered. 
We ask everyone to please change their pictures to this global day of prayer for Syria.

We ask that people spread the word and ask others to join in prayers and qiyams for Syria this Friday, insha Allah.

Please, please spread the word!



Fatwa dhidi ya mauaji Syria...



Fatwa Yatolewa Kupinga Mauaji ya Raia Syria:

  • Yasema kutii amri ya uongozi wa Assad ni makosa na sio sababu ya kukubalika.
Mamia ya wanazuoni kutoka nchi, madhehebu, na makundi mbali mbali ya ki-sunni islam waliokutana mji wa Istanbul Uturuki kwa takriban siku mbili wametoa tamko Jumanne kuamkia Jumatano. Wamesema kwamba haikubaliki kuutumikia utawala wa rais Bashar Al-Assad, na watu waache mara moja kuwa watiifu na waaminifu kwa utawala wa Assad.

Wanazuoni hao akiwemo Dk. Yusuf al-Qaradawi, mkuu wa umoja wa kimataifa wa wanazuoni (Union of Muslim Scholars), Msomi mashuhuri wa kisaudia Salman al-Ouda, na  Mufti wa Misri Dk. Ali Jumaa, wametuma tamko hilo kwa Anadolu Agency (AA).

Katika tamko hilo wamesema wanajeshi huria wa Syria na wanamapinduzi wanapaswa kusaidiwa, balozi mbalimbali zijitowe na kuachana na Syria, na nchi nyingine zitume ujumbe wa kuzipinga na kugomea nchi za Urusi na Uchina kwa kuwa wamekuwa wakikubaliana na kusaidiana na uongozi wa Syria.

Wanazuoni hao wamesema umwagaji damu na mauwaji nchini Syria hayawezi wala kupaswa kusahaulika, na machafuko haya ya Syria ni lawama kwa  wale waliokubaliana nayo, na wale waliokaa kimya, na wale walioshiriki katika kuleta mauaji hayo.

Fatwa hiyo imesema mauaji ya wananchi yanayofanywa na jeshi na "usalama wa taifa" hayakubaliki, na wanajeshi wanapaswa kupinga amri ya kuuwa watu.

Yafahamika kuwa baadhi ya mashehe wa kiislam wa zamani na wa sasa wanapinga tabia ya uasi wa Uongozi wa nchi kutokana na baadhi ya hadithi za Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) kama:

  • The Messenger of Allah said, “You must hear and obey (the ruler) both in your hardship and your ease and with regard to what pleases you and what you dislike and even if you do not get your due”. [Recorded by Muslim]
  • The Messenger of Allah said, “Hear and obey even if a, Abyssinian slave with a head like a raisin is appointed over you”.[Recorded by Bukhari]
  • The Prophet said “Listen and obey, even if the ruler seizes you and beats your back.” [Recorded by Muslim]

Kujibu hoja za wenye mrengo huo (wengi wakiwemo wenye kufuata Salafiyya), raisi wa shirikisho la mashirika mbalimbali ya  kiislam Ulaya, Shakib Bin-Makhlouf amesema uislam unapinga uonevu na dhulma, na wajibu wa msingi wa kiongozi muislam ni kusimamisha uadilifu katika jamii.

"Uongozi wa Assad umevuka mipaka yote myekundu katika kuwatendea raia" akasema. "Kwahiyo viongozi wa dini yawapasa kusimama upande wa raia. Wanastahili zaidi kabisa kufanyiwa hivyo"

Hata wasomi wakubwa kabisa, kama mkuu wa chuo cha Al Ahzar cha Misri, Sheikh Ahmad Al-Tayyeb ameongea kutetea wanaopinga Uongozi wa Yemen, Libya, na Syria. Alinukuliwa akiwaambia wanamapinduzi wa Libya mwezi Juni mwaka jana "Ngome na mamlaka yote hayana thamani sawa na hata tone moja la damu ya muislam"

Katika tamko hilo, wanachuoni hao wanaungana na kukubaliana na watu watakaotaka kulikana  jeshi, na kukaribisha kushiriki katika jeshi huria la Syria.

Wamesema wanazuoni hao kuwa Jeshi huria la Syria likae mbali na kutaka kulipiza kisasi, badala yake liweke umbele kulinda na kusaidia wananchi.

Tamko limesema kamati ziundwe Syria nzima kusaidia juhudi za mapinduzi, na poa kamati kama hizo ziandaliwe Uturuki, Jodan, na Lebanon ili kuwapatia watu wa Syria chakula na misaada mingine ya kibinaadamu.

Kuelekea ukingoni mwa mkutano huo pia walishutumiwa na kukemewa uongozi wa Iran na kikundi cha ki-Shia cha Hizbullah cha nchi ya Lebanon.

Maneno ya mwisho yalijumuisha onyo na changamoto kwa viongozi wachache wa dini walio upande wa Assad kusimama imara dhidi ya Assad au kungoja matokeo "katika dunia hii, na akhera"

Hisani ya Tovuti za: World Bulletin, iHaveNet, Ahlu Sunnah Wal jama'h.




Tuesday, February 7, 2012

Mwaliko Wa Semina



Mahali: University of Nairobi, [Kenyatta National Hospital]

Mzunguzaji: Allama Habib Ali Aljufri

Siku:  Jumanne, 14/2/2012

Muda:  2:00pm hadi 5:00pm


Baada ya Mhadhara  Al Habib atatoa waadhi Masjid Nuur, South C baada ya Maghrib.


Al Habib atawasili Kenya kutokea Abu Dhabi tarehe 13, kisha ataondoka  Nairobi kuelekea Lamu kwenye Maulid ya Riyadha.

Himma Himma! jitahid kuhudhuria 


Kwa maswali na maelekezo zaidi comment hapo chini.

Monday, February 6, 2012

Dalili zilizopo kwenye vitabu vya kutegemewa kuhusu Maulid


Yaa Nabii Salaam Aleika


Swali kuhusu waliozini kabla ya kuoana

Swali:

Nini hukmu ya ndoa ya watu waliozini kwanza kwa miaka miwili halafu baadae ndio wakafunga ndoa?

--------------------------------------------------------------------------------------------
Jibu:

Bismillah.
Watapata dhambi za zina zao na watapata thawabu za kuoana na kuhalalisha vitendo vyao VYA BAADA YA NDOA. Zina ni haramu, lakini haiharamishi halali! Huo ndlio msimamo wa maulamaa wengi sana, miongoni mwa Sunni. Ndugu zetu wa madhehebu ya Ibadhi, hata hivyo, wao wanaamini kuwa zina ni pingamizi ya ndoa.

 Wa billah al-Tawfiq Dr. A. Shareef

Sunday, February 5, 2012

Swali kuhusu Husuda, na Kijicho (Al Ayn)

Swali: 

Nini maana ya Kijicho na Husuda, na ni nini tofauti zake?
----------------------------------------------------------------------------------------------
Jibu:


Kijicho na Husuda\Hasada, au Jicho na Dege ni hali mbili ambazo zipo na zinatambuliwa na Dini kuwa mambo yanayoweza kuwa na athari mbaya na hivyo tujiepushe na hali hizo. 
روى مسلم في صحيحه عن ابن عباس ، قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : " العين حق ولو كان شئ سابق القدر ، لسبقته العين "
وفي الصحيحين من حديث أبى هريرة ، قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : " العين حق "


Mtume S.A.W. amesema: “ Kijicho\Dege ni haki (kipo\lipo) na lau kama kungelikuweko kitu kinachoweza kwenda kinyume na Qudra (yaani hakipo) basi ingekuwa kijicho”. Muslim na Bukhari.

Tawassul kwa Wanazuoni

Video: Tawassul kwa Wanazuoni
By: Ustadh Mbarak Ahmed.


Hii ni video ya tatu katika mlolongo wa mada ya Tawassul. Tizama "Tawassul katika Qur'ani na Sunna", na "Tawassul katika Sunna" katika section ya "Video za Kiswahili" Juu ya ukurasa wa blog hii. Sasa Ustadh Mbarak Ahmed anatuletea "Tawassul kwa Wanazuoni"

Friday, February 3, 2012

Hukmu ya kusherehekea Mazazi ya Mtume swallahu aleihi wa salaam


Bismillah alRahman alRahiym


Kwa mujibu wa mafunzo ya kiislamu ni muhimu (bali ni wajibu) kuyaelewa mas-ala kabla ya kuyatolea hukumu. Wanachuoni wa Usuul wanasema kuelewa mas-ala ni nusu ya jawabu. Nasi kabla ya kutoa hukumu juu ya mas-ala ya maulidi ni vizuri tukawa na mtazamo sahihi juu ya kadhia nzima kabla hatujatoa hukumu. Quran inatuonya kuwa kusema kuwa hili ni halali na hili

Uswahihi wa swalat Tasbih



Bismillah Rahman Rahim


Swali limeulizwa kuhusu swalati Tasbih ambayo umaarufu wake watu wengi huifanya mara moja kwa mwaka(ndani ya Ramadhan) au mara moja kwa mwezi au mara moja kwa Wiki.Na miaka ya hivi karibuni kumekuwepo na baadhi ya Waisilamu wenye kuipinga swalah hii tukufu na kusema swala hii ni uzushi(Bidaa) na kumekuwepo na juhudi za makusudi kupiga vita suala hili ikilinganishwa na suala la bidaa.Inshallah kwa Tawfiq yake Allah tuiangalie hii swalah ya Tasbih kutoka katika viunga vyake muhimu(Sunnah/Hadith) na Maulamaa wakubwa wakubwa wamesemaje kuhsu swalah hii

Qari Masoud Adam in London




Qari -- Masoud Adam
















Swali kuhusu ndoa ya Mut'ah

Swali:

Je, ndoa ya Mutta inafaa?, naomba maelezo ya ziada.

-----------------------------------------------------------------------------------------------

Jibu:

Naamini unakusudia Ndoa ya Mut’a na si Mutta. Kama ni hivyo, basi ni vyema kuitolea ufafanuzi unaostahili ili ijulakne timbuko lake, sababu zake na msimamo sahihi wa Sharia juu yake.

Neno “Mut’a”, katika lugha ya Kiarabu, linamaanisha : starehe ya muda; Kwa hivyo, “Nikah al-mut’a”

Swali kuhusu mtoto akicheuwa kwenye nguo...

Swali:

Je, mtoto mienzi minne hadi mwaka mmoja akikucheulia katika nguo itafaa kusalia?

-----------------------------------------------------------------------------------------
Jibu:

Bismillah;
Kipimo si umri bali ni hali ya kichanga. Kichanga ambacho hakili kitu isipokuwa maziwa tu, basi akikojolea nguo, unatakiwa kuimwagia maji yachuruzike - na siyo lazima kuikosha-. Viovyo hivyo, utafanya hivyo hivyo kwa kichanga kilichokucheulia nguoni. Hivyo, ndivyo alivyokuwa akifanya mtume S.A.W. alikuwa akiletewa

AQIDA AT TAHAWIYYA




Akida Ya Tahawiya

sikiliza kwa kiarabu
(Cha Imam Tahawi)

(Akida ya Kiislam: Ahlu Sunnah wal Jama'a)

Kimetungwa na;
Abu Jaafar Ahmed bin Muhammad bin Salama Al-Tahawi. 

Bida'h kwa mujibu wa Ahlu sunnah wal jama'ah

Je, Bid'a ni nini?
Pt 1

-----------------------------------------------------
Je, Bid'a ni nini?
Pt 2

Video: Je bid'a ni nini
By: Ustadh Mbarak Ahmed

Let's talk about Bida'h.

Videos: Bid'ah in the light of Qur'an and Sunnah
By: Allama Dr. Muhammad Tahir ul Qadri


Bida'h...in the light of Qur'an and Sunnah
Pt 1
-----------------------------------------------------


Bida'h...in the light of Qur'an and Sunnah
Pt 2
-----------------------------------------------------


Bida'h in the light of Sunnah
------------------------------------------------------

Wednesday, February 1, 2012

Tawassul Katika Qur'an..







Videos: Tawassul katika Qur'an
By: Sidi Mbarak Ahmed.

LATFIYAH



AUDHUBILLAHI MINASHAITWANI RAJIYM
ALLAHU LATWIFUN BIL IBADAHI YARZUQU MANYASHAAU WA HUWA-L-QAWIYYU-L-AZIYZ
 Soma  YA LATWIYF  Mara 1000 
Kisha Soma Dua hii 

Al-Wadhwifa al-Mashishiyya/Swalat Mashishiyah


A`udhu bi-llahi sh-shaytan ir-rajimi

I seek refuge with Allah from the evil one, the rejected.
Bismi llah ir-rahman ir-rahim
In the name of Allah, the Merciful, the Compassionate
‘allahumma salli wa-sallam bi-jami`i sh-shu’uni fi z-zuhuri wa-l-butini
O Allah, send blessings and peace in all the affairs of the revealed and the hidden,
‘ala man minhu anshaqqati l-‘asraru l-kaminatu fi dhatihi l-`aliyyati zuhuran
Upon the one from whom the secrets, which were hidden in his lofty essence, were cleft apart,
Wa-nfalaqati l-‘anwaru l-muntawiyatu fi sama’i sifatihi s-saniyati buduran
And the lights, which are hidden in the sky of his lofty qualities, dispel the shadows of night as full moons,
Wa-fihi rtaqati l-haqa’iqu minhu ‘ilayhi

Hizbul Bahar Li-Imam Abal Hassan As-Shadhuli(Q.A.S)



The shaykh said concernign Hizbul Bahar:
Wallahi, I did not utter it [Hizbul Bahar] except as it came from Rasulu-Allah S.A.W, from whose instruction I learned it. "Guard it;' he said to me, "for it contains Ismu Allah al Aadhwam (Durrat Asrar wa Tuhfat Abrar)
Bismillah Rahmanir-Rahiym
Allahumma Swali alaa Sayidnaa Muhammad wa Aalaa Aaali Sayidnaa Muhammad
Ya Allah Aaliyu Ya Adhwimu Ya Haleem Yaa Aleeym

حزب النصر Li Imam Abal Hassan As Shadhuli (Q.A.S) Hizb al-Nasr



حزب النصر 
Hizb al-Nasr

اللهم بسطوة جبروت قهرك، وبسرعة إغاثة نصرك، وبغيرتك لانتهاك حرماتك، وحمايتك لمن احتمى بآياتك، Allahumma bisatwati jabarouti qahrika, wa bisorati ighathati nasrika, wa bighayratika li ntihaki horumaika, wa himayatika liman ihtama bi ayatik.
O Allah, by the force of the absolute power with which You triumph, and the quickness of Your succour when You aid to victory, and Your jealousy at the violation of things You have made sacrosanct, and by Your protection of him who seeks safety in Your verses: 

Ruqya kwa matatizo ya majini?

Swali:

Je, kuna dua/ maombi za kuwafukuza majini?

-----------------------------------------------------------------------------------------------
Jibu:

Bismillahi Rahmani Rahiim. Imam Al Nawawi katika Al Adhkar ameeleza kwamba Ibn al Sunni amesimulia kuwa bwana mmoja alimwendea Mtume (Rehema na Amani ziwe juu yake) na kumwambia kuwa kaka yake alikuwa na matatizo ya jini. Mtume (Sallallahu alayhi wa sallam) akamwambia amlete huyo kaka na kisha akamsomea Qur'an kama ifuatavyo: