Fatwa Yatolewa Kupinga Mauaji ya Raia Syria:
- Yasema kutii amri ya uongozi wa Assad ni makosa na sio sababu ya kukubalika.
Wanazuoni hao akiwemo Dk. Yusuf al-Qaradawi, mkuu wa umoja wa kimataifa wa wanazuoni (Union of Muslim Scholars), Msomi mashuhuri wa kisaudia Salman al-Ouda, na Mufti wa Misri Dk. Ali Jumaa, wametuma tamko hilo kwa Anadolu Agency (AA).
Katika tamko hilo wamesema wanajeshi huria wa Syria na wanamapinduzi wanapaswa kusaidiwa, balozi mbalimbali zijitowe na kuachana na Syria, na nchi nyingine zitume ujumbe wa kuzipinga na kugomea nchi za Urusi na Uchina kwa kuwa wamekuwa wakikubaliana na kusaidiana na uongozi wa Syria.
Wanazuoni hao wamesema umwagaji damu na mauwaji nchini Syria hayawezi wala kupaswa kusahaulika, na machafuko haya ya Syria ni lawama kwa wale waliokubaliana nayo, na wale waliokaa kimya, na wale walioshiriki katika kuleta mauaji hayo.
Fatwa hiyo imesema mauaji ya wananchi yanayofanywa na jeshi na "usalama wa taifa" hayakubaliki, na wanajeshi wanapaswa kupinga amri ya kuuwa watu.
Yafahamika kuwa baadhi ya mashehe wa kiislam wa zamani na wa sasa wanapinga tabia ya uasi wa Uongozi wa nchi kutokana na baadhi ya hadithi za Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) kama:
- The Messenger of Allah said, “You must hear and obey (the ruler) both in your hardship and your ease and with regard to what pleases you and what you dislike and even if you do not get your due”. [Recorded by Muslim]
- The Messenger of Allah said, “Hear and obey even if a, Abyssinian slave with a head like a raisin is appointed over you”.[Recorded by Bukhari]
- The Prophet said “Listen and obey, even if the ruler seizes you and beats your back.” [Recorded by Muslim]
Kujibu hoja za wenye mrengo huo (wengi wakiwemo wenye kufuata Salafiyya), raisi wa shirikisho la mashirika mbalimbali ya kiislam Ulaya, Shakib Bin-Makhlouf amesema uislam unapinga uonevu na dhulma, na wajibu wa msingi wa kiongozi muislam ni kusimamisha uadilifu katika jamii.
"Uongozi wa Assad umevuka mipaka yote myekundu katika kuwatendea raia" akasema. "Kwahiyo viongozi wa dini yawapasa kusimama upande wa raia. Wanastahili zaidi kabisa kufanyiwa hivyo"
Hata wasomi wakubwa kabisa, kama mkuu wa chuo cha Al Ahzar cha Misri, Sheikh Ahmad Al-Tayyeb ameongea kutetea wanaopinga Uongozi wa Yemen, Libya, na Syria. Alinukuliwa akiwaambia wanamapinduzi wa Libya mwezi Juni mwaka jana "Ngome na mamlaka yote hayana thamani sawa na hata tone moja la damu ya muislam"
Katika tamko hilo, wanachuoni hao wanaungana na kukubaliana na watu watakaotaka kulikana jeshi, na kukaribisha kushiriki katika jeshi huria la Syria.
Wamesema wanazuoni hao kuwa Jeshi huria la Syria likae mbali na kutaka kulipiza kisasi, badala yake liweke umbele kulinda na kusaidia wananchi.
Tamko limesema kamati ziundwe Syria nzima kusaidia juhudi za mapinduzi, na poa kamati kama hizo ziandaliwe Uturuki, Jodan, na Lebanon ili kuwapatia watu wa Syria chakula na misaada mingine ya kibinaadamu.
Kuelekea ukingoni mwa mkutano huo pia walishutumiwa na kukemewa uongozi wa Iran na kikundi cha ki-Shia cha Hizbullah cha nchi ya Lebanon.
Maneno ya mwisho yalijumuisha onyo na changamoto kwa viongozi wachache wa dini walio upande wa Assad kusimama imara dhidi ya Assad au kungoja matokeo "katika dunia hii, na akhera"
Hisani ya Tovuti za: World Bulletin, iHaveNet, Ahlu Sunnah Wal jama'h.
No comments:
Post a Comment