Friday, February 24, 2012

Swali kuhusu vazi la hija (ihram)...

Swali:

Je, Ihram inaruhusiwa kushona au kufunga na pini?


Jibu:


Ihram ni vazi lakuhiji. Vazi la mwanamke linaweza kushonwa kama kanzu na mtandio, kama vile mavazi anayovaa kwa kuswali. Ama mwanamume, bazi lake haliruhusiwi kushonwa. Ni shuka mbili, moja kuvaa chini na ya pili kuvaa juu. Wakati wa wote wa hija, mwanamume hatakiwi kufunika kichwa chake, mpaka baada ya
kupiga mawe siku ya kwanza (baada ya kutoka Arafa na kulala Muzdalifa). Na mwanamke haruhusiwi kufunika uso wake na viganja vayake vya mikono katika muhula huo vile vile.

Hali kadhalika, mwanamume na mwanamke - akiwa katika hija, basi haruhusiwi kuoga, kukata nywele, kujitia manukato, kufunga ndoa, kua kiwndo chochotekile, na mengi mengine ambayo hapa si mahali pake kuyataja. Kwa ufupi, Ihram - au vazi la hija la mwanamke linaweza kushonwa ama la mwanamume haliruhusiwi kushonwa.

Wa billah al-Tawfiwq
Dr. A. Shareef

No comments:

Post a Comment