Friday, February 3, 2012

Uswahihi wa swalat Tasbih



Bismillah Rahman Rahim


Swali limeulizwa kuhusu swalati Tasbih ambayo umaarufu wake watu wengi huifanya mara moja kwa mwaka(ndani ya Ramadhan) au mara moja kwa mwezi au mara moja kwa Wiki.Na miaka ya hivi karibuni kumekuwepo na baadhi ya Waisilamu wenye kuipinga swalah hii tukufu na kusema swala hii ni uzushi(Bidaa) na kumekuwepo na juhudi za makusudi kupiga vita suala hili ikilinganishwa na suala la bidaa.Inshallah kwa Tawfiq yake Allah tuiangalie hii swalah ya Tasbih kutoka katika viunga vyake muhimu(Sunnah/Hadith) na Maulamaa wakubwa wakubwa wamesemaje kuhsu swalah hii



Hadith

 حدثنا عبد الرحمن بن بشر بن الحكم النيسابوري، ثنا موسى بن عبد العزيز، ثناالحكم بن أبان، عن عكرمة، عن ابن عباس : أن رسول اللّه صلى اللّه عليه وسلم قالللعباس بن عبد المطلب : " ياعباس يا عماه ألا أعطيك؟ ألا أمنحك؟ ألا أحبوك؟ ألاأفعل بك عشر خصالٍ إذا أنت فعلت ذلك غفر اللّه لك ذنبك أوله وآخره، قديمهوحديثه، خطأه وعمده، صغيره وكبيره، سره وعلانيته عشر خصالٍ : أن تصلي أربعركعاتٍ تقرأ في كل ركعة فاتحة الكتاب وسورةً، فإِذا فرغت من القراءة في أول ركعةٍوأنت قائمٌ قلت : سبحان اللذه، والحمد للّه، ولا إله إلا اللّه واللّه أكبر خمس عشرةمرةٍ، ثم تركع فتقولها وأنت راكعٌ عشراً، ثم ترفع رأسك من الركوع فتقولها عشراً، ثمتهوي ساجداً فتقولها وأنت ساجدٌ عشراً، ثم ترفع رأسك من السجود فتقولها عشراً، ثمتسجد فتقولها عشراً، ثم ترفع رأسك فتقولها عشراً، فذلك خمسٌ وسبعون في كلِّركعةٍ تفعل ذلك في أربع ركعاتٍ إن استطعت أن تصليها في كلِّ يوم مرةً فافعل، فإِنلم تفعل ففي كلِّ جمعةٍ مرةً، فإِن لم تفعل ففي كلِّ شهر مرة، فإِن لم تفعل ففي كلِّسنةٍ مرةً، فإِن لم تفعل ففي عمرك مرةً ".‏

 Vilevile inapatikana kwa maneno haya

عن ابن عباس رضي الله عنهما أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال للعباس: "يا عماه ألا أعطيك؟ ألا أمنحك؟ ألا أحبوك؟ ألا أفعل بك عشر خصال إذا أنت فعلت ذلك غفر الله لك ذنبك أوله وآخره وقديمه وحديثه وخطأه وعمده، وصغيره وكبيره، وسره وعلانيته، عشر خصال، أن تصلي أربع ركعات تقرأ في كل ركعة فاتحة الكتاب وسورة، فإن فرغت من القرآن قلت: سبحان الله والحمد لله ولا إله إلا الله والله أكبر خمس عشرة مرة، ثم تركع فتقولها وأنت راكع عشرا ، ثم ترفع رأسك من الركوع فتقولها عشراً، ثم تهوي ساجداً فتقولها وأنت ساجد عشراً، ثم ترفع رأسك من السجود فتقولها عشراً، ثم تسجد فتقولها عشراً، ثم ترفع رأسك فتقولها عشراً. فذلك خمس وسبعون في كل ركعة، تفعل ذلك في الأربع ركعات. إن استطعت أن تصليها في كل يوم مرة فافعل، فإن لم تفعل ففي كل جمعة مرة، فإن لم تفعل ففي كل شهر مرة، فإن لم تفعل ففي كل سنة مرة، فإن لم تفعل ففي عمرك مرة".


maelezo  toka : Sahih Fiqh -hu-Sunna iliyoandikwa na  Abu Malik Kamal Ibn Al-Sayid Salim, Mujaraba wa 2, hadith  nambari 33; ‘Ikrimah anasimulia kutoka kwa  Ibn ‘Abbas kuwa Mtume S.A.W alimweleza  Abbas ibn ‘Abdal-Mutalib: “Ewe  Abbas, Ewe Ami Yangu, Nikueleze jambo jema?, Nikupe zawadi ilo njema kwako? ,Je nikueleze mambo kumi ambayo ukifanya Allah atakusamehe madhambi yako yote uliyofanya mwanzo na mpaka sasa? Madhambi ambayo uliyafanya kwa siri na dhahiri, madhambi uliyofanyanya kwa makusudi na bila kukusudia?Madhambi uliyofanya kwa siri na kwa dhahiri? Mambo hayo kumi ni: Swali Rakaah nne, katika kila swala soma Fatiha na Surah na utakapomaliza kusoma Fatiha na Surah wakati umesimama soma maneno haya: 

Subhanallah Wal hamdullilah walailaha ilallah wa Allahu Akbar  mara kumi na tano, nenda rukuu sema tena Tasbih hiyo mara kumi rudi Itidali sema tena hiyo Tasbih mara kumi , nenda Sijidah soma tena hiyo Tasbih mara kumi Katika Jalsa baina ya sijida soma tena hiyo Tasbih mara kumi nenda tena sijida some tena hiyo Tasbih mara kumi , baada ya Sijida ya pili kaa kitako soma tena hiyo Tasbih mara kumi endelea na Rakaa ya pili. Kwa kuhisabu idadi itakuwa sabiini na tano (kwa kurejea Tasbih hii Subhanallah walhamdullilah wala ilaha illa Allah Allahu Akbar) kwa kila Rakaa. Soma hivyo kwa kila Rakaa kwa rakaa zote nne. Kama hutoweza kuiswali swala hii kila siku , basi ifanye mara moja katika kila Ijumaa, na kama hutoweza kila Ijumaa basi na ifanye mara moja kwa mwaka na kama hutoweza basi ifanye mara moja katika Umri wako.

Hadithi hii tukufu  Imesimuliwa katika Sunan  Abu Daud Hadith nambari 1297, Sunan Ibn Maja Hadith namba 1387, na Al Hakim Hadith namba 1308, Ibn Khuzaimah katika Swahihi yake na At-twabarani.

Kuhusu Hadithi hii al-Mundhiri asema : “Hadith hii imesimuliwa toka kwenye sanadi nyingi ambazo zinakwenda mpaka kwa Maswahaba na sanadi yenye nguvu sana ni ile itokayo kwa Ikrimah.
  
Wanachuoni waliowengi (Jumhur ya Maulamaa) wameiswahihisha hadithi hii kama, Al-Hafidh Abu Bakr al-’Ajari, (mwalimu wake al-Mundhiri), Abu Muhammad ‘Abdurrahim al-Misri,  na  Abu al-Hassan al-Maqdisi.” Ibn alMubarak asema : “Swala ya Tasbih ni Mustahab  na yenye kuppendekezwa sana kwetu na yampasa kila mmoja wetu aifanye  na wala asiiwache"

Allaamah Mundhiri (RA) ameandika  Muhaddithin wengi  ambao wameikubali Hadith hii katika hao ni : Imaam Abu-bakr al-Ajurriy, Imaam Abu Muhammad al-Misriy (Ustaadh wake  Allaamah Mundhiri), Hafiz Abul-Hasan Maqdisi (Ustaadh wake Allaamah Mundhiri), Imaam Abu-Dawud and Imaam Haakim. (Targheeb Mujaraba wa 1 uk. 468)

Allaamah Suyutwi (RA) amewataja muhadithin  wakubwa na mashuhuri mpaka kufikia idadi ya  20 ambao wameikubali uswahihi wake. Mbali na hao walioelezewa  katika hao: Abu-Sa'id al-Sam'aaniy, Khatwib al-Baghdaadiy, Hafidh ibn-Mandah, al-Bayhaqi, al-Subkiy, al-Nawawiy, ibn al-Salah, Abu-Musa al-Madiniy, al-Alaaiy, Siraaj-ud-Din al-Bulqiniy, al-Zarkashiy na wengineo wengi (al-Laalil Masnu'ah Mujaraba wa 2 uk. 40)

Wahadith wafuatao wa Ahlul Sunnah wal Jamaa  wameandika kwa kirefu kuhusu Swalat
Tasbih kwa kuikubali kuwa ni swahihi:

1) Imaam al-Daraaniy (r.a.),
2) Imaam Abu-Musa al-Madiniy (r.a.),
3) Hafidh ibn Mandah (r.a.),
4) Hafidh ibn Naaswirud-Din ad-Dimishqiy (r.a.),
5) 'Allamah al-Suyyuutwi (r.a.)  na  
6) Imaam Ibn Tuluun (r.a.)
7)Al Madni
8)As-Sumaani
9)Al Mundhiri
10)Abaul Hassan al Mundhiri
11)Ibn As-Salaah
12)Ad-Dalami
13)Al-Hakim
14)Al-Alaali
15)Az-Zurkashi
16)Al-Muhaamil
18)Haithami
19)Luknawi(Luknavi)
20)Ibn Abidin

Imaam al-Bayhaqi (RA)anasimulia kuwa  'Swalaat al-Tasbih  ilikuwa ni  katika Ibada 
aipendayo  Abdullah ibn al-Mubaarak na Masalaf Swaleh wengi (Watangu wema) wa maeneo
tofauti duniani na wakati tofauti .Kutokana na ukweli huu swala hii inakuwa ni yenye nguvu 
na kukubaliwa kwake na hawa watangu.' (Shu'ubul Imaam Mujaraba wa1 uk. 427; chapa ya Ilmiyyah)

Maulamaa wa Kishafii  walioikubali ni kama ifuatavyo  Imaam al-Mahalliy, Imaam al-  
Juwaini Imaam-ul-Haramayn, Imaam Ghazzaaliy, Imaam Raafii na wengineo  (al-La-aaliy
Mujaraba wa .2 uk wa .43; al-Adhkaar cha Imaam al-Nawawiy uk wa .242)
Qauli ya Khatwib Baghdaadiy (RA), haina haja/hoja ya kuikataa hii swalat Tasbih. Haafidh ibn Hajar (RA) amegusia qauli toka kwa Imaam Maalik qauli ambayo inaonyesha kuwa inakubalika katika Madh-habu ya Ki-Maliki  ( Futuhaat al-Rabbaaniyyah Mujaraba wa 4 uk wa 321) Qaadhi Iyaad Maaliki (RA)  pia anaikubali swala hii.

Imaam Ahmad ibn Hanbal (RA) ana qauli mbili katika suala hili qauli yake ya zamani na qauli yake mpya kuifuta qauli yenye kuifuta qauli ya zamani , Mwanachuoni wa hadith Hafidh ibn Hajar (RA) anasema Imam Ahmad Ibn Hanbal aliikubali baadae ( kwa qauli mpya) ambayo yaonyesha pia alikuwa akiiswali swala hii (Futuhaat al-Rabbaaniyyah Mujaraba wa .4 uk wa .318, 320)

Imaam Taajuddin Subkiy (RA) na Imam  BadrudDin Zarkashi wao wanasema swala hii ni 
katika masuala ya usuul din  mbali ya kuwa ni masuala ya  wema  yeyote atakayeipinga hatokuwa katika njia swahihi  (Futuhaat Mujaraba wa .4 uk wa .321-322)

Mwanachuoni wa Kislafiya Naswirudini al -Bani pia ameiswahihisha katika kitabu chake Albani Swahihi Sunan Abu Daudi Hadith namba 152. Albani anasema katika Hadith hii twachukua vitu viwili muhimu kwanza yatupasa kuikubali hadith kuwa ni Swahihi hata kama hakuna katika watangu (Salaf) waliwahi kuiswali!! Mbali na hii imesimuliwa kwetu kuwa katika Masalaf kama vile Ibn Mubarak walikuwa wakiswali swala hii.

Suala la pili ni kuwa ni kuiweka katika matendo hadith hii (yaani tuiswali swala hii) ambayo kuna baadhi ya watu wanaiyona Bidaa! Hii itakuwa inatufanya sisi kuhuisha Sunnah ya Mtume
Swalallahu aleihi wa salaam   na atapata ujira bora  toka kwa Allah mpaka siku ya malipo na atakayekuwa akiifanya swala hii na kuirithisha kwa vizazi vijavyo malipo yake hayatokoma mpaka Yaumul qiyama.

Hafidh ibn Hajar al-Asqalaani (RA) anasimulia  kuwa kuna wakati  Muhaddith anaamua kufanya baadhi ya hadith dhaifu , au  kusema hadith ni ya kutunga akitegemea isnadi moja au mbili alizonazo kumuonyesha udhaifu huo, ingawa zinaweza kuwepo sanadi nyingine zenye nguvu zaidi ya hizo ategemeazo ambazo zinaweza kuifanya hadith kuwa hassan au hata kuwa Swahihi (Al nukat Mujaraba wa .2 uk wa .848-850)

Hafidh ibn Hajar (RA) anaendelea na kuielezea kwa mfano wa hadith hizo kama  hadith ya Swalat Tasbih  kuwa imeelezewa kuwa ni Swahihi au hassan na sio dhwaifu. Imaam al-Tirmidhi (RA) Maulamaa wengi ikiwemo  Imaam Abdullah ibn al-Mubaarak (RA), wameikubali swala hii ya tasbih na mazuri yake mengi (Tirmidhi Mujaraba wa .2 uk wa .348; Hadith 481), Targheeb Mujaraba wa .1 uk wa .468)

 Uswahihi wa Hadith

Wanachuoni walioidhoofisha hadith hii ni - Imam Ahmad (Baadaye alibadilisha msimamo
wake juu ya Hadith hiii)


Wanachuoni ambao wameinyamazia kimya ni  - Ibn Khuzaima,Al-Dhaahabi

Wanachuoni walioiswahihisha hadith hii  kuwa  hasan lighairihi  au  swahihi ni  
Muslim  na  Abu Dawud ( kama ilivyohadithiwa na  Al-Munthiri), Al-Hakim, Al-Bayhaqi, Ibn Hajar, na  wanachuoni wa kisasa (Salafiyah)  Ahmad Shakir na Albani wameikubali Hadith hii kuwa ni swahihi.

Hoja za wanawachuoni hawa wa Ahlul Sunnah wal Jamaa na wale wenye msimamo uitwao Salafiyah hususan wamfuatao Sheikh Albani ni kuwa:

1- Ni mustahab kuswali Swalat Tasbih . imepokelewa toka kwa  Ibn Mubarak, kuwa Ma-Shafii 
na wanawachuoni wengine   wamekubaliana kuwa Hadith ni Swahihi

2- Imejuzishwa  kuswaliwa na baadhi ya wanachuoni wa Kihanbali kuswaliwa kwa hoja yao
kuwa hata kama haina darja la uswahihi inajuzu kuiswali Swalat Tasbih kwa sababu inaangukia kwenye mlango wa mambo ya kheri (فضائل الاعمال)

Imam Hanbali aliikana Swalat Tasbih kwa hoja kuwa haipendi kwa kuwa Isnadi yake si
swahihi hii ilikuwa ni hoja Qadiim twaona Imam Ahmad ambaye baadaye alikuwa akiiswali
baada ya kufikiwa na hoja thabit juu ya usahihi wa Hadith hii ya swala ya Tasbih
  
Wanachuoni waliosema kuwa Hadith hii ni dhwaifu ni kama ifuatavyo:
  •  Imam Al-Tirmidhi  (aliongezea kwa kusema kuwa Hadith hii ni Gharib kutokana na Abi Rafi’I , lakini anaendelea kusema kuwa Ibn Mubarakah alikuwa ni mwenye kuiswali swala hii na watu wengi wema na watu wa Ilm walikuwa ni wenye kuifanya swala hii)
  • Ibn Al-A'rabi
  • Ibn Al-Jawzi
  • Ahmad Bin Hanbal (Alibadilisha msimamo wake juu ya uswahihi wa swalat Tasbih mwishoni mwa maisha yake)
  • Al-U'qaili
  • Ibn Taimia
  • Ibn Jawziyah
  • Ibn Khuzaima: (Lakini amesherehesha chini  ya Hadith hii kuwa Hadith hii  ikiwa itakubalika  ni dhwaifu basi haifai kuswaliwa ama ikiwa inakubalika kuwa ni sahihini wajibu kuikubali na kufuata!!!) 
Wanachuoni wa kisasa  walioikataa na kuiita bidaa ni:
  • Shaykh Muqbil (saudi salafiya)
  • Shaykh Bin Baaz (saudi salafiya)
  • Shaykh Uthaymeen (saudi salafiya)
  • Shaykh Yahyaa al Hujuriy(saudi salafiya)
Kutokana na hoja zilizotolewa hapo juu kwa kukubalika na jopo la Maulamaa wa Ahlul Sunnah wal Jamaa na hata wale wenye msimamo wa Kisalafiya kwa kufuata msimamo na mrengo wa Albani, inaonyesha swala hii ya Tasbih haina mgogoro wowote  na tumeona imekubalika kuwa ni Hadith swahihi na yenye mashiko makubwa kabisa.


Shime waisilamu tuisimamishe swala hii hususan katika makuni haya ya mwisho yaliyobaki ,Kuna wale wajiitao Masalafiya wenye kufuata misimamo ya Ibn Taimia na Ibn Qayim Jawziya bado wanashikilia kuwa ni dhaifu na haifai kuswaliwa. Hoja zao ni dhaifu ukilinganisha na hoja za Baadhi ya Masalafiya wenzi wao na Jumhuri nzima ya Ahlul Sunnah wal Jamaa kuhusu msimamo wao juu ya Hadith hii.

Tanbih:

1. Unaweza kuswali wakati wowote ule iwe mchana au usiku , inashauriwa sana kuswaliwa wakati wa Laylatul Qadr(katika masiku ambayo yanakadiriwa kuwa Laylatul Qadr) kutokana na barakah za usiku huu kama ilivyoelezwa ndani ya Quraan Sura ya 97

2. Tasbih iwe na idadi ya  300 katika Rakaa nne kama ilivyo maelekezo kwenye Hadith na uhesabu idadi hiyo ukitumia vidole na usihesabu kwa sauti kubwa hii itabatwilisha swala yako.

 Jambo muhimu la kuzingatia:

Mtazamo huu wa Albani juu ya Swalat Tasbih ni tofauti na mtazamo wa Masalafiya/Answar Sunnah wenye kufuata mrengo wa Ibn Taimia au Usalafiya wa Kisaudia kama vile Sheikh Uthaymin , Sheikh Ibn Baaz ,Al Hujuriy Sheikh Muqbil wao huona suala hili ni Bidaa na yafaa kupigwa vita Na wamechukua dalili toka kwa Ibn Taimia ambaye Ibn Taimia alichukua dalili toka kwa hoja ya zamani ya Imam Ahmad ambayo aliiwacha na kufuata Jamhur ya wanawachuoni kuhusu suala la Swalat Tasbih!

Ifahamike tunapoongelea neno Salaf(tunamaanisha watangu wema yaane karne tatu za mwanzo) na tunapoongelea Salafiyah au Salafiy tunamaanisha kundi linalofuata itikadi iliyoanzishwa na Ibn Taimia na wanafunzi wake(ingawa yeye alibaki kuwa Hanbali) na hususan skuli itokayo Saudia au yenye mahusiano na Saudia, na tunapoongelea Ahlul Sunnah wal Jamaa ni wale wenye kujinasibisha na kufuata Madh-habu ya Kishafi, Maliki, Hanafi na Hanbali hususan wafuatao Aqidatul Ashairah na Maturidi wengine wasema hata Aqidatul Athairah nao ni katika Ahlul Sunnah wal Jamaa. 

No comments:

Post a Comment