Swali:
Asalam aleikum, nini hukumu ya kufanya Kunut kila swala ya asubuhi kama wanavyofanya katika misikiti mingi ya East Africa (hususan Ma-Shafi)?
Jibu:
Waalaikum salaam. Katika masail yenye kuwatatiza baadhi ya watu ni mas'ala ya Qunut, na ilifika daraja mpaka kupiga wanaoleta qunut wakiwa ndani ya swala na hilo limetokea malindi kenya. Kuna risala naiandaa inshaallaah karibuni itakua tayari, ispokua nitayaashiria kwa mukhtasar hapa kwa kua nimeombwa hilo. Qunuut tunaizungumzia hapa ni ya kila siku katika swala ya alfajiri wala sio ya witri.
1) Amepokea ibnu 7ibbaan na ibnu khuzayma kutoka kwa anas bin malik (r.a) asema: Mtume (s.a.w)alikua haleti qunut katika swala ya asubuhi ispokua anapowaombea ama anapoapiza watu.
2) Na anapokea Imam Ahmad na Bazzaaq na Daaru qutny na Bayhaqy na Alhakim kutoka kwa huyohuyo Anas (r.a) kuwa Mtume (s.a.w) hakuacha kuleta qunut katika swala ya alfajiri mpaka alipofariki dunia.
3) Na amepokea Alhazimy katika al'i3tibaar kutoka kwa Ibnu Mas3uud (r.a) kuwa Mtume (s.a.w) hakuleta Qunut ispokua mwezi.
Sasa ni vipi tutajumuisha kati ya hizi hadith? Jee alikua haleti kabisa? Ama alileta mwezi kisha akawacha? Ama alileta siko zote mpaka kufariki?
Hadith ya kusema alileta mwezi kisha akawacha (#3) inafasiriwa na hadith ilopokewa na Abu Hanifa katika musnad yake kua Mtume (s.a.w) alileta qunut mwezi akiwaapiza makafiri. So aliposema kisha akawacha means akawacha kuwaapiza makafiri sio akawacha kuleta Qunut.
Ama hadith mbili za kwanza zote zimepokewa kutoka kwa Anas (r.a), ya kwanza yasema alikua haleti ispokua kwa kuombea watu ama kuwaapiza, na yapili yasema alileta daima; tutatanguliza ipi?
Qaa3ida inasema: Almuthbitu muqaddamun 3alan naafy. Siku zote anaethibitisha hutangulizwa kuliko mwenye kukataa. Kwahivyo hadith ya kutowacha mpaka kufariki ndio itakayotangulizwa.
Kwa kuthibiti hilo ndio imam shafi akasema qunut ni sunna katika swala ya alfajiri. Wallaahu a3lam
Pengine wanaopinga hawajafahamu, lakini hoja yao kubwa ni kuwa hadith inayosema hakuacha kuleta ni dhaifu, na hilo tutalieleza kwa mapana na marefu katika risala inshaallaah kuwa hadith ni sahih kabisa na wala hawajakose Imam Bayhaqy na Imam Hakim walipoiswahihisha.
Wabillahi Tawfiq.

No comments:
Post a Comment