Monday, February 6, 2012

Swali kuhusu waliozini kabla ya kuoana

Swali:

Nini hukmu ya ndoa ya watu waliozini kwanza kwa miaka miwili halafu baadae ndio wakafunga ndoa?

--------------------------------------------------------------------------------------------
Jibu:

Bismillah.
Watapata dhambi za zina zao na watapata thawabu za kuoana na kuhalalisha vitendo vyao VYA BAADA YA NDOA. Zina ni haramu, lakini haiharamishi halali! Huo ndlio msimamo wa maulamaa wengi sana, miongoni mwa Sunni. Ndugu zetu wa madhehebu ya Ibadhi, hata hivyo, wao wanaamini kuwa zina ni pingamizi ya ndoa.

 Wa billah al-Tawfiq Dr. A. Shareef

No comments:

Post a Comment