Tuesday, February 21, 2012

Swali kuhusu taarifa ya kuongeza mke ...


Swali:

Ikiwa mume hakumwambia mkewe kama anataka kuoa na baada ya kuoa pia hajamwambia na mwanamke ameshajua kama mumewe kaoa naye hajamuuliza mumewe na hakuna zamu mume kila siku analala kwa mke wa kwanza. Je hali hii inakubalika katika sheria ya kiislam?

Jibu:

Kumuarifu kabla siyo lazima, lakini kufanya uadilifu, ikiwa pamoja na kugawa zamu sawasawa ni LAZIMA, na hiyo inamaanisha kumjulisha baada ya kuoa ni budi. Maana hatoweza kugawa zamu sawasawa pasi na
kumjulisha mke wa mwanzo. Mwenyezi Mungu anasema: وإن خفتم ان لا تعدلوا فواحدة Mkichelea kutokuwa waadilifu basi (kaeni na ) mke mmoja". Mtume (S.A.W) amesema: " من كانت عنده إمرأتان فلم يعدل بينهما جاء يوم القيامة وشقه ساقط" " Mwenye wake wawili na asiwatendee uadilufu basi atakuja siku ya Qiyama akiwa na ubavu ulioporomoka" [Tirmidhi, Nasa'i na Ibn Majah]

Na Bibi Aisha R.A. amesema: Mtume (S.A.W) alikuwa akigawa zamu na akifanya uadilifu (kwa wakeze) na alikuwa akiseama: " اللهم هذا قسمي فيما أملك فلا تلمني فيما تملك ولا أملك" " Ewe Mola! Huu ndio mgao wangu katika kile ambacho ninakimiliki; basi nakuomba usinilaumu katika kile ambacho unakimiliki na mimi sikimiliki" akikusudia MOYO. [Abu Daud, Tirmidhi, Nasai na ibn Majah].

Yaani Mtume (S.A.W) alikuwa muadilifu sawasawa katiak kuwatendea wake zake wote, isipokuwa katika kugawa mapenzi yake! Hapo alikuwa akimuomba Mwenyezi Mungu asimpatilize kwa vile hakuwa na udhibiti wa kugawa mapenzi sawasawa kwa wake wake wote.

Mwenyezi Mungu vile vile anasema: " ولن تستطيعوا أن تعدلوا بين النساء ولو حرصتم فلا نميلوا كل الميل فتذروها كالمعلقة وإن تصلحوا وتتقوا فإن الله كان غفورا رحيما" النساء " ....Na hamtaweza kufanya uadilifu (wa mapenzi) baina ya wanawake, hata mkikakamia.Kwa hivyo, msimili moja kwa moja mkamwacha (mmojawapo) kama aliye gtundikwa. Na mkisikilizana na mkamcha Mwenyezi Mungu basi Mungu ni Mwingi wa maghafira na Mwenye Kurehemu". [al-Nisa' 126]

 Wa billah al-Tawfiq
 Dr. A. Shareef

No comments:

Post a Comment