Inna Lillahi Wa inna Ilayhi Rajiuun
Habari kutoka Mombasa, Kenya zinasema kuwa usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa, kundi la waisilamu wenye kufuata mtizamo wa ki-Wahabi walifika katika msikiti wa Mlango Wa Papa ambamo palikuwa pameandaliwa sherehe za Maulid kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad [Sallallahu aleihi wa sallam]-rehma kwa walimwengu wote, na kuzuia waumini kufanya sherehe hizo.
Ni desturi kuwa kila Alhamisi ya tatu ya mwezi wa Rabi al Awwal husherehekewa Maulid katika msikiti huo, bahati mbaya msikiti huo umekuwa na mvutano baina ya waumini wa Ahlu sunnah wal jama'a wanaochukulia Maulid kama jambo jema (bid'ah njema), na Mawahabi/"Salafi" ambao huona kama kusherehekea mazazi ya Mtume ni uzushi na upotofu. Ndugu mmoja (Jina linahifadhiwa) aliyeshuhudia mvutano huo anaeleza: "Sasa mimi nilipofika baada kuswali isha nilikuta fujo ilikua imeanza. Hawa wahabi walijua leo kuna maulidi kwa hivyo walikuja hapo msikitini kwanza swalat asr kwa singizio kuwa wako na ijtima'a. Basi ilipofika 7:25pm hivi ndio fujo ikaanza. Hawa watu walikua tayari wamejiandaa na mitaimbo, bakora na visu. Wakaanza fujo mara wakajifungia wao peke yao ndani ya msikiti!"
Taarifa tulizopokea zinaeleza kuwa watu kadhaa wamejeruhiwa katika vurugu hizo, akiwemo mtoto wa aliyekuwa balozi wa Kenya nchini Saudi Arabia.
Akiendelea kutupa ripoti zaidi, Ndugu yetu aliyekuwepo katika tukio amesema: "Watu wamepigana kwa mawe,mimi binafsi nimepigwa mtimbo katika hali ya kufungua mlango waliokua wamejifungia ndani. Alhamdulillah! sikuumia sana, maumivu tu kidogo na alama. Mimi nimeondoka nimecha bado watu wanaendelea, aibu....hata sijui twaelekea wapi jamani."
Mungu atunusuru na fitna, na atuongoze na kutujaalia amani. Amin,
No comments:
Post a Comment