Sunday, February 26, 2012

Johari za Wanazuoni


~ Aliulizwa swali Sayyid Al Habib Umar bin Hafiz (Allah Amhifadhi): "Tufanyeje tukiona uvivu na ukosefu moyo wa kufanya baadhi ya sunnah na nyiradi?"


Akajibu: "Mjisukume mbele kwa kujitia moyo (matumaini): mjikumbushe malipo ya amali hizo na matokeo yake (faida) katika maisha yajayo.


Ukijiona mvivu wakati mwingine usikate tamaa. Usiwache kufanya (hilo jambo) na usilicheleweshe - jirudi ufanye ulivyokuwa ukifanya, kwa kuwa ki asili, haujakamilika.


Huenda uvivu wako unakufundisha somo kubwa na muhimu. Unaweza ukakuletea/jengea udhoofu na unyenyekevu mbele ya Allah, na unaweza kukuondolea 'ujub rohoni mwako. Hii yaweza kuwa na faida zaidi kwako kuliko kufanya kitendo chenyewe"

No comments:

Post a Comment