Sunday, February 5, 2012

Swali kuhusu Husuda, na Kijicho (Al Ayn)

Swali: 

Nini maana ya Kijicho na Husuda, na ni nini tofauti zake?
----------------------------------------------------------------------------------------------
Jibu:


Kijicho na Husuda\Hasada, au Jicho na Dege ni hali mbili ambazo zipo na zinatambuliwa na Dini kuwa mambo yanayoweza kuwa na athari mbaya na hivyo tujiepushe na hali hizo. 
روى مسلم في صحيحه عن ابن عباس ، قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : " العين حق ولو كان شئ سابق القدر ، لسبقته العين "
وفي الصحيحين من حديث أبى هريرة ، قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : " العين حق "


Mtume S.A.W. amesema: “ Kijicho\Dege ni haki (kipo\lipo) na lau kama kungelikuweko kitu kinachoweza kwenda kinyume na Qudra (yaani hakipo) basi ingekuwa kijicho”. Muslim na Bukhari.



Husuda\Hasada siyo tu imetajwa wazi wazi ndani ya Qur’ani katika surat al-Falaq lakini pia imetajwa dawa yake (zinguo lake) ndani ya sura hiyo hiyo. 


Aya zifuatazo zinazungumzia Kijicho na Hasada:


" وإن يكاد الذين كفروا ليزلقونك بأبصارهم لما سمعوا الذكر " [ القلم : 51 ] . وقال : " قل أعوذ برب الفلق * من شر ما خلق * ومن شر غاسق إذا وقب * ومن شر النفاثات في العقد * ومن شر حاسد إذا حسد " ،


Kijicho, mara nyingi, ni hisia anayokuwa nayo mtu, juu ya mtu mwengine, mara tu baada ya kumuona kwamba anacho kingi mno; kana kwamba anaona kuwa amependelewa kupewa kitu hicho. Yaweza kuwa ni kuvutiwa bila ya kiasi na sura yake, uzuri wake, umbo lake, mavazi yake na kadhalika; bila ya kuwa na niya ya kumpokonya uzuri huo au sifa hiyo au vazi hilo, bali kumtazama kwa jicho la gere kiasi kutamani na yeye angekuwa na sura kama hiyo au sifa kama hiyo au vazi kama hilo! Yaani anamuona huyo aliyemtazama kwa jicho lake kuwa “ Ahh! Aamepewa kingi mno au kikubwa mno au kizuri mno” na kadhalika. 


Kwa vile jicho lina nguvu kubwa sana – bila ya sisi wenyewe kujuwa- kutokana na nguvu alizoziweka Mwenyezi Mungu ndani ya mboni, basi nguvu hizo zinaweza kutoa aina fulani ya miyale inayokwenda moja kwa moja kudunga kilo ilichokiona na hivyo kuathiri kitu hicho. 


Athari ya kijcho ameielezea Mtume S.A.W. aliposema:


: "إن العين لتجعل الجمل الكبير في القدر والإنسان العظيم في القبر


“Kijicho|Dege humuingiza ngamia mkubwa kwenye chungu na mwamadamu mwenye sifa njema kwenye kaburi” Yaani kijicho kinaweza kupelekea mauti kwa aliyeonuewa kijicho! 


Muono wake huo –kutokana na nguvu fulani alizoziweka Mwenyezi Mungu ndani ya Jicho- unaweza kumuathiri aliyeonwa na jicho hilo; na hivyo mwenye kuona muono huo, kidini, hutakiwa aseme papo hapo: “Mashaallah”. Au Bismillahi Mashaallah! Au Katukuka Mwenyezi Mungu Mtukufu, Anampa amtakaye! Na kadhalika. 


Ziko njia nyengine ambazo Mtume S.A.W. ametufunza kuzifanya kuondoa kijicho. Nitazitaja baadaye. 


Ama Husuda\Hasada ni hisia ya chuki na wivu anayokuwa nayo mtu dhidi ya mtu mwengine,juu ya kitu fulani au hali fulani, kiasi ya kuchukizwa na kupenda kitu hicho au hali hiyo iondoke kwa huyo mtu. Hupendi kumuona fulani ana kitu fulani, au anaishi katika hali fulani, au ana kazi nzuri fulani! Ungependa na unapendad kitu hicho kimtoke na kadhalika. Husuda ni chuki dhidi ya neema aliyokuwa nayo mtu mwengine kiasi kupenda neema hiyo imtoke kabisa! Kana kwamba hastahili kuwa na neema hiyo! 


Kutokana na ufafanuzi huo, tunaweza kusema kuwa: “ Kijicho” ina maana pana zaidi kuliko “ Husuda”; maana kila mwenye kijicho, kwa kutaka au kutokutaka, ana sehemu ya “ husuda”, lakini SI kila mwenye “ Husuda” ana kijicho! Ndiyo maana, kijicho kina athari mbaya zaidi na papo kwa papo, kuliko athari ya husuda, inagawa kwa upande wa dhambi, husuda ina dhambi kubwa zaidi kuliko kijicho. Kwa sababu, mwenye husuda ana nia ya kutaka kuona neema imtoke mtu fulani, hivyo lengo lake ni wazi wazi kuwa ni baya tokea mwanzoni. Kijicho, kwa upande wake, kina athari mbaya ya moja kwa moja na aliyeonewa kijicho, lakini siyo lazima kuwa aliyeona kijicho ana niya au lengo la kuona neema hiyo imtoke huyo aliyemuona nayo. Tatizo lake ni kuona kwamba aliyepwa sifa hiyo au sura hiyo au mali hiyo amepewa nyingi mno, kana kwamba amependelewa! Hivyo basi, anaweza kuwa nia yake SI kutaka kuona neema hiyo imtoke, la. Bali ni kuona kwamba amepewa nyingi mno tu! Ni mfano wa GERE katika jamii zetu. Kumuonea mtu gere ni kuona kuwa hicho alichonacho ni kingi mno na hivyo kupenda na yeye angekuwa nacho kama hicho vile vile. 


Mafunzo ya Mtume S.A.W. kuhusu kijicho.


Mojawapo ni zinguo. 


Na zinguo ni kusomea maji baadhi ya sura za Qur’ani, kama Alfatiah, Surat al-Nnas, Surat al-Falaq na Ayat al-Kursiyy na kisha kumnyunyizia aliyesibiwa na kijicho, iwapo mwenye kijicho hicho hajulikani.


Mtume S.A.W. hata hivyo, amesema kwamba yule ambaye akijihisi amemtazama Mwislamu mwenziwe kwa jicho ambalo linaweza kuwa kijicho, basi atawadhe na achukue maji aliyotawadhia kumwagia mwilini (kumuosha) yule ambaye anaamini kuwa huenda akawa amemtazama kwa kijicho. 


Baadhi ya dua za kuondoa au kutibu kijicho (zinguo) zilizopokelewa kutoka kwa Mtume S.A.W.


أعوذ بكلمات الله التامات من شر ما خلق .


ونحو : أعوذ بكلمات الله التامة من كل شيطان وهامة ، ومن كل عين لامة .


ونحو : أعوذ بكلمات الله التامات التي لا يجاورهن بر ولا فاجر ، من شر ما خلق وذرأ وبرأ ، ومن شر ما ينزل من السماء ، ومن شر ما يعرج فيها ، ومن شر ما ذرأ في الأرض ، ومن شر ما يخرج منها ، ومن شر فتن الليل ، والنهار ، ومن شر طوارق الليل إلا طارقاً يطرق بخير يا رحمن .


ومنها : أعوذ بكلمات الله التامة من غضبه وعقابه ، ومن شر عباده ، ومن همزات الشياطين وأن يحضرون .


ومنها : اللهم إني أعوذ بوجهك الكريم ، وكلماتك التامات من شر ما أنت آخذ بناصيته ، اللهم أنت تكشف المأثم والمغرم ، اللهم إنه لا يهزم جندك ، ولا يخلف وعدك ، سبحانك وبحمدك .


ومنها : أعوذ بوجه الله العظيم الذي لا شئ أعظم منه ، وبكلماته التامات التي لا يجاورهن بر لا فاجر ، وأسماء الله الحسنى ، ما علمت منها وما لم أعلم ، من شر ما خلق وذرأ وبرأ ، ومن شر كل ذي شر لا أطيق شره ، ومن شر كل ذي شر أنت آخذ بناصيته ، إن ربي على صراط مستقيم .


ومنها : اللهم أنت ربي لا إله إلا أنت ، عليك توكلت ، وأنت رب العرش العظيم ، ما شاء الله كان ، وما لم يشأ لم يكن ، لا حول ولا قوة إلا بالله ، أعلم أن الله على كل شئ قدير ، وأن الله قد أحاط بكل شئ علماً ، وأحصى كل شئ عدداً ، اللهم إني أعوذ بك من شر نفسي ، وشر الشيطان وشركه ، ومن شر كل دابة أنت آخذ بناصيتها ، إن ربي على صراط مستقيم .


وإن شاء قال : تحصنت بالله الذي لا إله إلا هو ، إلهي وإله كل شئ ، واعتصمت بربي ورب كل شئ ، وتوكلت على الحي الذي لا يموت ، واستدفعت الشر بلا حول ولا قوة إلا بالله ، حسبي الله ونعم الوكيل ، حسبي الرب من العباد ، حسبي الخالق من المخلوق ، حسبي الرازق من المرزوق ، حسبي الذي هو حسبي ، حسبي الذي بيده ملكوت كل شئ ، وهو يجير ولا يجار عليه ،


حسبي الله وكفى ، سمع الله لمن دعا ، ليس وراء الله مرمى ، حسبي الله لا إله إلا هو ، عليه توكلت ، وهو رب العرش العظيم .


Kuna hadithi nyingi zinazokataza husuda na kutaja dhambi za husuda: Miongoni mwa hadithi hizo ni: " Jiepusheni na Hasada\husuda; kwani hada inakula thawabu kama kuni zinavyokula moto" Abu Daud. " Haikai pamoja kwenye tumbo la Mu'umini vumbi la jihadi na mpulizob wa Jahannam (moto) wala hazikai pamoja katika mwili wa mwenye kuamini Imani na Hasada". Ibn Hibban. Hadithi za dhambi za hasada ni nyingi na makatazo yake ni makubwa.


Swali linakuja; Je kipofu anaweza kuwa na athari za kijicho?


Anazo; anaweza kupatwa na kupatisha kijicho. Mwenyezi Mungu akimnyang'anya kiumbe chake macho ya kawaida basi humpa macho ya hisia na hayo yana athari ya macho ya kawaida vile vile. 


Wa Billah al-Tawfiq Dr. A. Shareef 

No comments:

Post a Comment