- Vatikan yataka kuiona biblia hiyo
- Yadaiwa kuwa na umri wa millenia moja na nusu
Biblia ya siri ambayo Yesu (Nabii Isa Aeyhi Salaam) anaaminika kutabiri ujio wa Mtume Muhammad (S.A.W) ulimwenguni imezua utashi wa udadisi kutoka Vatican.
Papa Benedict XVI amedai kutaka kuona kitabu hicho chenye umri wa miaka elfu mia tano (1,500) ambacho wengi wamesema ni Injili ya Barnaba ambacho kilikuwa kimefichwa na serikali ya Uturuki kwa zaidi ya miaka kumi na mbili.
Kitabu hicho cha pauni milioni kumi na nne kilichoandikwa kwa mkono na kwa maandishi ya ki-dhahabu kipo katika lugha ya kwanza ya Yesu (A.S) "Aramaic", kinasemekana kuongelea mafunzo ya awali ya Ukriso na kutabiri ujio wa Mtume (S.A.W)
Nakala ya ukurasa mmoja wa biblia hiyo inafikirika kuwa na thamani ya Pauni milioni na nusu za Uingereza. Katika Injili hiyo, kama imani ya waislam, ipo wazi kuwa Yesu (A.S) ana hadhi ya ki-Utume (ubinadamu) na si Uungu. Pia inapingana na nadharia ya Utatu Mtakatifu, na kusulubiwa kwa Yesu (A.S) na inatabiri kuja kwa Mtume Muhammad (S.A.W)
Katika toleo moja la injili ya Barnaba inasemekana alimwambia kuhani: "Messiah ataitwa nani? Muhammad ni jina lake takatifu" Na katika toleo lingine, Yesu (A.S) amekana kuwa ndiye Messiah, akisema kuwa huyo atakuwa Mu-Ismaili (Ishmaelite), yaani kutoka uzao wa Nabii Ismail (A.S) ambavyo waarabu wamekuwa wakiitwa wakati huo.
Pamoja na habari hizi, baadhi ya watu wanadai buku hilo si la kweli na kuwa labda liliandikwa katika karne ya kumi na sita, kwa kuwa nakala za zamani kabisa zinazojulikana za injili ya Barnabas ni za wakati huo na zipo katika lugha ya Kiitaliano na Kihispania.
Pasta wa madhehebu ya Ki-protestant, İhsan Özbek ameeleza kuwa haitegemewi kuwa ni Injili halisi ya Barnabas kwa kuwa Mtakatifu Barnabas aliishi katika karne ya kwanza tofauti na inavyodaiwa katika toleo hili ambalo linadaiwa kutoka karne ya tano au sita. Ameliambia gazeti la Zaman: "Nakala iliyopo Ankara yaweza kuwa iliandikwa na mmoja wa wafuasi wa mtakatifu Barnaba"
Profesa wa theologia amesema uchunguzi wa kisayansi kwa kutumia miale ndio njia pekee ya kugundua umri halisi wa Buku hilo.
No comments:
Post a Comment