Friday, February 3, 2012

AQIDA AT TAHAWIYYA




Akida Ya Tahawiya

sikiliza kwa kiarabu
(Cha Imam Tahawi)

(Akida ya Kiislam: Ahlu Sunnah wal Jama'a)

Kimetungwa na;
Abu Jaafar Ahmed bin Muhammad bin Salama Al-Tahawi. 


Alizaliwa Katika Kijiji cha Tahawiya Mwaka 239, Hijriyyah na akafariki mwaka 321 Hijirriyah.
Kasema Sheikh ,“Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Bwana wa ulimwengu amesema Sheikh Abu Jafar Al-Warraq Al-Tahawi wa Misri, “Huu ni uchambuzi wa imani ya Ahlus-sunnah wal-Jamaah kufuatana na mwangalio wa wana-sheria wa Kiislamu ambao ni Abu Hanifa Al-Numan bin Thabit Al-Kufi (Alifariki 150.  Hijiriya); Abu Yusuf, Yaqub bin Ibrahim, Al-Ansari, Abu Abdallah, Muhammad bin Al-Hassn Al-Shaibani, Mola awe radhi nao.  Hawa wote waliangalia akida ya dini hii  kwa jicho hili hili.  Na hivyo ndivyo ilikuwa imani yao kwa dini ya Mola wao, Mumba wa ulimwengu.
Kwa rehma zake Allah, sisi nasi twasema juu ya Tawhid  ya Allah:

Akida ya Kiislamu

A. TAWHID RUBUBIYYAH

Hii ni itikadi ya kuamini upweke na Allah na kuwa yeye yu pekee katika matendo yake. Kwa maana nyingine ni kuwa Allah ni pekee kafika kuumba vitu vyote, kuvinemesha na kuviweka na kuendelea vikiwa vyenye kuendelea. Yeye pekee ndiye aliye na uhuru wa kutenda atakalo katika habari zote za ulimwenguni na hata baada ya Qiyamah.  Alifanya, anafanya na atafanya bila msaada wa yeyote wala bila kuwa na masaidizi.  

Kasema katika (39:62):
"Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu, na Yeye ndiye Mlinzi juu ya kila kitu". Na amesema katika Surat (Yunus 10:3): "Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenyezi Mungu, ambaye ameziumba mbingu na ardhi kwa siku sita, na ametawala kwenye ufalme wake, anaendesha mambo yote. Hapana mwombezi ila baada ya idhini yake. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi. Basi muabuduni Yeye. Je! Hamkumbuki?"
Hata washirikina ambao walikuwa wanaabudu masanamu walitambu aina hii hii ya Tawhid kuwa Allah yu pekee katika jambo hili la kuumba na kuendesha ulimwengu.  Bali wao walikana hali ya kufufuliwa/ hawakuamini kusimama kwa Qiyamah pamoja na kukubali kwao kuwa Allah yu pekee na uwezo wake huu; hawakuangaliwa hawa kuwa ni Waislamu; kwa sababu walimshirikisha Allah na visivyo kuwa Mungu. Waliabudu vitu vingi zaidi ya Allah na walikataa kukubali siku ya hukumu.
Rububiyyah ni kuwa malezi yote ya ulimwengu yapo mikoni kwa Mwenyezi Mungu Allah (na kwa hilo anastahiki kuabudiwa yeye tu na si kingine kile) Aliye pwekeka.

B.        TAWHID ULUHIYYAH

Aina hii ya Tawhid ilikataliwa kabisa na mushirikina.  Allah anasema: (Saad: 38:4 – 5) "Na walistaajabu kuwajia mwonyaji anaye tokana nao wenyewe, na makafiri wakasema: Huyu ni mchawi, mwongo." 5. "Amewafanya miungu wote kuwa ni Mungu Mmoja tu? Hakika hili ni jambo la ajabu."
Quran imeleta aya nyingi za namna hiyo.  Tawhid hapa inamtaka binadamu aelekeze ibada zake zote kwa Allah, Mwenyezi Mungu, Mola wa ulimwengu tu.  Ni yeye tu ndiye anastahiki kuabudiwa hivyo kuabudu kingine kile kisicho kuwa yeye (Allah) ni ibada ya urongo.  Na kwa uhakika hiyo ndio tafsiri na maelezo ya Lailaha Illallah, yaani hakuna apaswaye kuabudika kwa haki isipokuwa Allah; kama alivyosema:- (Al –Hajj:22:62}

C.        TAWHID – ASMAI WA SIFAT

(Kumpwekesha Allah katika majina yake na sifa zake) maana yake ni kuwa Allah yu pekee katika majina yake na sifa zake.  Na hiyo ni kuamini kuwa majina na sifa za Allah zilivyopokelewa ndani ya kitabu chake Quran na katika Hadith Sharifu za Mtume (SAW) ni kweli na haina budi kuaminiwa kama vilivyo; bila kubadili kwa kupunguza kitu (maana) au kuongeza.  {Hakuna kutafsiri majina yake na sifa zake kwa sura ya binadamu}.  Na hilo ni kuliangana kauli yake ifuatayo.
Ikhalas – 112: 1 – 4
1. Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee. ***
2. Mwenyezi Mungu Mkusudiwa. ***
3. Hakuzaa wala hakuzaliwa. ***
4. Wala hana anaye fanana naye hata mmoja.  ***  
Na pia kasema Allah: (Shura – 42:11):
"Yeye ndiye Muumba mbingu na ardhi, amekujaalieni mke na mume katika nafsi zenu, na katika nyama hoa dume na jike, anakuzidishieni namna hii. Hapana kitu kama mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona"

Na pia kaongeza (A’araf – 7:180):
"Na Mwenyezi Mungu ana majina mazuri kabisa, basi muombeni kwa hayo. Na waacheni wale wanao haribu utakatifu wa majina yake. Hao watakuja lipwa waliyo kuwa wakiyatenda."
Na kisha kasema tena: (Nahl – 16:60):
"Hali ya wasio iamini Akhera ni ovu; na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye sifa tukufu. Naye ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima."
Mfano wa juu kabisa maana yake ni maelezo mazuri sana juu ya Allah ni ile hali kuwa ametakasika na kasoro zo zote.  Hivi ndivyo watu wa Ahlu Sunnah Wal-Jamaah miongoni mwa maswahaba na wale waliokuja baada yao, walivyo kuwa wakiamini.  Walizifahamu sifa za Mwenyezi Mungu kutoka ndani ya Qurani na Sunnah bila kuthibutu kuzitafsiri sifa hizo katika hali za maumbo au maumbi la wanayoyafahamu wao.  Pia walimtakasa Mola wao na hawakuthibutu kumlinganisha Allah na kiumbe chochote.  Mwendo wao wa fungu hili la Tawhid nikulingana na Kitabu na Sunnah; na hali hiyo inafunga mlango wa upinzani katika suali zima hilo.  Wenye kuamini hivyo ndio haswa waliotajwa katika aya ifuatayo na tunaomba Allah aliweke liwe miongoni mwao (Aminah).  Ni yeye tu ndiye mwenye kutegemewa kwa mambo yote na neema zote na dua zote zielekezwe kwake. 

(Tauba: 9:100)
"Na wale walio tangulia, wa kwanza, katika Wahajiri na Ansari, na walio wafuata kwa wema, Mwenyezi Mungu ameridhika nao, na wao wameridhika naye; na amewaandalia Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa."

JUU YA TAWHID
(KUMPWEKESHA ALLAH)

1.                  Allah ni mmoja na wala hana mshirika kabisa.

2.                  Hakuna katika ulimwengu wote kinacholingana na Allah.

3.                  Hakuna kinachoweza kumfikia katika matendo wala kumpita (kumzidi).

4.                  Hakuna apaswaye kuabudiwa isipokuwa yeye Allah.

5.                  Yeye ni mkongwe hana mwanzo, na ni wamilele asiye kuwa na mwisho.

6.                  Hatakufa na wala hatatoweka.

7.                  Hakuna litokealo ulimwenguni isipokuwa kwa utashi wake.

8.                  Hakuna fikra ambayo inaweza kumweleza yeye yuko namna gani.

9.            Hafanani na chochote katika viumbe vyake.

10.              Yuko hai, na wala kifo hakitamfikia.  Yeye ndiye mlinzi, akiwa hana haja kulala (au kupumzika).

11.             Yeye ndiye aliye umba ulimwengu wote; lakini hana shida na ulimwengu huo. Yeye anatoa riziki kwa            walimwengu wote bila ugumu wowote.

12.          Yeye anawaonyesha na kluwapelekea walimwengu umauti/kifo bila kuogopa; na atawatia uhai tena bila taabu au kusumbuka.

13.              Amekuwepo katika Azali akiwa na sifa zake zote.  Amekuwa nazo hizo sifa zote na ataendelea kuwa nazo.  Hizi sifa hazikuongezeka baada ya kuumba viumbe, maana sifa hizo zimekuwepo daima.

14.              Hakuwa muumbaji baada ya kuumba (khaliq) viumbe vyake wala hakuwa mwenye kusimamisha (Al-Bain) baada ya kuusimamisha ulimwengu.

15.              Alikuwa mlezi (Rabb) kabla ya kuwepo chochote cha kulelewa na amekuwa mumbaji …..(khaliq) kabla hajamwumba yeyote.

16.              Ingawa anaitwa mponyeshaji, anastahiki kuwa na sifa hiyo kabla hata ya kuleta ufufuo.  Hali kadhalika anastahiki kuitwa muumbaji hatakama alikuwa hajaumba kitu chochote.

17.              Uwezo wake ni juu ya kila kitu; kila mtu yu muhitaji kwake.  Anaweza kufanya lolote atakalo na wala hahitajii chochote wala lolote.

18.              Au ameviumba vitu vyote ili hali anajua anaumba nini na vipi.

19.              Na kila kiumbe alikiwekea kadiri ya mipango, mahitaji yake.

20.              Alipanga mwisho wa kila kiumbe.

21.              Hakuna kilichofichikana kwake hata kabla alikuwa hajaumba viumbe hivyo.  Alijua toka mwanzo kuwa viumbe hivyo vitakuwaje na vina mambile gani na vitenda gani viumbe hivyo vitatenda katika uhai.

22.              Allah anawaamuru waja wake kumwabudu anawamuru waja wake wasimuasi.

23.              Kila kitu katika ulimwengu kimefungamanishwa na utashi wake Allah.  Chochote au lolote atakalo hutokea.  Na lile asilolitaka kutokea basi haliwi asilani.

24.              Allah (Subhanahu wataala) humwongoa amtakaye.  Ana mhifadhi na madhara kila mmoja kutokana huruma zake.  Kwa hali uadilifu na kuwapa usawa viumbe vyake humdhalisha mmoja kwa mwingine au huzunia uongofu wake kwa mja mmoja au mwingine na huwatia viumbe wake katika mitihani jinsi apendavyo.

25.              Watu wote wako chini ya utawala wake hapa duniani; maisha yao yanatawaliwa na huruma zake na ukarimu wake kwa upande mmoja na kwa uadilifu wake kwa upande mwingine.

26.              Yeye yu juu ya kila kitu ambacho kinaweza kushirikishwa kwake na yeye hana walahakuna aliye sawa naye.

27.              Hakuna awezaye kubadilisha yale aliyopanga (qadari yake) na wala amri zake hazicheleweshwi.  Hakuna atakaye  vuruga mipango yake.

28.              Imani yetu kwa Allah ni kamili.  Junaani kuwa kila litokealo ni kutokana na utashi wake.

JUU YA MUHAMMAD (S.A.W)

29.              Bila shaka yoyote Muhammad ni kiumbe kilichotukuka cha Allah; ni mjumbe wake aliye kipenzi kwake na mtume aliye chaguliwa.

30.              Yeye ni mtume wa mwisho, Imam wa wachamungu wote, Sayyid (Mbora) wa mitume yote na hakuna kipenzi zaidi yake kwa Mwenyezi Mungu ulimwenguni.

31.              Madai yoyote ya utume baada ya mtume Muhammad ni uongo na ukafiri.

32.              Muhammad ni mtume aliyetumwa ujume kwa binadamu na majini; na ujumbe wake ni kwa ulimwengu wote ili kuongoza katika haki.

JUU YA QURAN

Hapana shaka kwamba Quran ni kauli ya Allah.  Allah Subhanahu wa taalah, kaleta wahyi huu kwa mtume wake.  Waumini wanashuhudi kuwa (Qurani) ni ukweli mlipu huku wakiamini kuwa ni neon la Allah na siyo kiumbe kama yalivyo viumbe maneno ya viumbe.  Yeyote asikilizaye maneno ya kitabu hiki na akadhmia kuwa ni maneno ya binadamu anafanya kufru.  Allah amemlaani mtu wa namna hiyo na kamwahidi adhabu kali katika moto wa Jahanamu.  Alisema; (74:26) 26. Nitakuja mtia kwenye Moto wa Saqar.

33.              Hilo lilikuwa jibu kwa yule aliyesema juu ya Qurani kuwa ; (74:25). 
            Haya si chochote ila kauli ya binaadamu.
        Tunaamini kuwa Qurani ni neno la Mwenyezi Mungu Bwana wa binadamu wote.
         Maneno yake hayafanani na maneno ya binaadamu.

34.                    Yeyote atakayelinganisha sifa za Allah na sifa za binadamu anafanya kufuru.  Mtu akiwaza sana na akajiepusha na matendo ya kufuru, atatambua kuwa sifa za Allah hazilingani wala hazifanani na zile sifa za binadamu.

35.          Watu wa Peponi watamwona Mola wao kulingana na kauli ya Quran isemaviyo:    Namna gani hali hii itatokea anajua Allah mwenyewe.  Aya hiyo ieleweke kuwa   hayo ni matakwa yake Allah, na ni elimu yake yeye mwenyewe.  Maelezo mazuri juu ya hilo ni hadithi ya mtume, ambayo ni sahihi.  Hapa ni kuwa utashi wetu na matakwa yetu hayana msingi juu ya jambo hili.  Mja yuko salama (na matendo ya) na kufuru iwapo ataweka msingi wa kuangalia vitu kama vilivyo ndani ya kitabu cha Allah na Hadith za mtume (S.A.W).

36.          Yeyote asiyekubaliana na hoja zilizotolewa katika Kitabu na Sunnah hana Uislamu.  Mtu ambaye atakuwa anafanya mambo ya Kiislamu na hana maarifa halisi na wala hajitupi katika kutafuta ukweli katika vyanzo hivyo viwili – (Kitabu na sunnah) atabakia bila kuwa na imani thabiti, ya kuuelewa Uislamu na imani safi juu ya kupwekeka kwa Allah.  Badala yake mtu huyu atakuwa anatapatapa kati ya imani na kufru; kusilimu na kukufuru.  Atakuwa mwenye kubabaika mara huku mara kule.
               Mtu huyu atakuwa si mwenye imani thabiti wala si mtu aliyekufuru na kukataa kuamini moja kwa moja.

37.          Si sawa kumdhania Allah kuwa ana umbo fulani. Njia iliyo salama ni kuamini kuwa sifa zake zote ni sawa bila kuongeza tafsiri yoyote. Kuziangalia sifa za Allah kama ni majina matupu au kumlinganisha Allah ni mtu akitu ni upotovu; Mola wetu yu wa pekee na hakuna kinachofanana naye.

38.          Allah Karim yu juu ya kila kitu, hana mipaka.  Tofauti na vitu vyote tunavyovifahamu Allah hakuzungukwa na mipaka au kitu chochote; hana mwelekeo wa sehemu sita; juu, chini, mbele, nyuma kushoto na kuume.[3]

39.          Miraji – ni safari ya mtume ya usiku kwenda mbinguni ni tukio lakweli.  Mwenyezi Mungu alimchukua mtume Muhammad (SAW) akiwa yu macho katika safari hiyo isiyo ya kawaida.
              
               Miraji

      Hali ya miraji yaani kupaishwa mtume Muhammad (S.A.W) ilitokea kwa nafsi yake, mwili na roho.  Mola karim alimchukua akanifikisha alipotaka afike.  Kasema Allah Karim (53:10 – 11)

            JUU YA KAUTHAR

40.       Ziwa la Kauthar ni kilicha ukweli.  Allah muweza atawapa ruhsa Ummah (wa Muhammad kukata kio kutokana na ziwa hili tukufu.

            JUU YA SHAFA’A

41.       Shafa’a kwa ummah ni jambo la kweli watapata shaf’a ya mtume Muhammad na habari hizi zimewaridi katika hadith nyingi tu.

            JUU YA AHAD YA ADAM

42.       Ahadi aliyochukua Allah kutoka kwa Seyyidna Adam (A.S) na vizazi vyake ni jambo lililotokea kweli.
Angalia: Rejea Aya ya 172 ya A’raf ambayo inasema kama ifuatavyo: 
(7:172 – 173).

JUU YA QADARI

43.       Mwenyezi Mungu toka azali amekuwa akijua ni watu gani wataingia Peponi na nani wataingia moto wa Jahanamu.  Hakuna la kuongezeka wala la kupungua katika elimu hiyo ambayo ni yake tu Allah pekee.

44.       Allah anajua matendo yote ambayo wanayatenda na yale watakayoyatenda.  Matendo ambayo amekadiri wa mjaitakuwa ni rahisi kwake kuyutenda.  Amebahatika yule ambaye gadari imempangia matendo mema na bahati yake mbaya ambaye gadari imempangia kinyume na hivyo.

45.       Qadar ni siri ya Allah juu ya viumbe vyake; siri hiyo haijui yeyote katika viumbe vyake, si malaika wa mitume.  Qadari ukii tafakari sanandivyo utakavyo sononeka sana na hata pengine kuingiwa na ujeuri na kiburi.

Hapo ndipo tunafunzwa kuwa mUislamu ajiepushe sana na kuweza na kuwazua juu ya Qadar.  Mwenyezi Mungu amewaonya waja wake juu ya Qadar kwa kuwaeleza kuwa “Haulizwi (Allah) kwa nini alifanya kile; lakini wao (waja) watauliswa matendo yao”  Kwa mja kuuliza, “ kwa nini Allah alifanya hili?”  maana yake mja huyu ameasi moja ya amri za Quran na yeyote aulizaye hivyo huwa kafanya tendo la kufru.

46.       Ni waja wematu ambao roho zao zimenawirishwa na imani ya Allah, wanaamini sharia kwa vitendo na kwa kuifuata bila kuuliza kamailivyoletwa katika wahyi.  Wacha mungu wanakuwa na tabia hiyo.
            Elimu iko katika mafungu mawili:
(i)                  Elimu ya dhahiri ambayo [(kama vile chain ya kitabu cha Mungu (Quran na sunnah za Mtume S.A.W.)]
(ii)                Elimu ya Ghaibu (Ambayo ni ya Qadar ambayo imefichikana kwa viumbe wote).[4]
Kukataa vitu vilivyopa dhahiri na kudai kuwa mtu anajua vitu vilivyofichikana/kufahamu ghaibu ni ukafiri.  Imani ya mja inakuwa thabiti kwa kukubali elimu ya mja inakuwa thabiti kwa kukubali elimu ya dhahiri na kuachilia mbali bila kutafuta elimu ya ghaibu.

47.       Tunaamini kuwap kwa kalamu ya Mwenyezi Mungu na pia kuwepo kwa ubao (lauhu mahfudh) na vitu vingine ambavyo vinahusiana na Qadar ya Allah.  Alichoamua na kupanga Allah kuwa kitokee basi kitatokea hata kama viumber vyote watajaribu kuzuia hilo jambo lisitokee. Hali kadhalika, kama Allah alipanga pasitendeke au kutokea jambo basi halitokei asilani hata kama viumbe vyote vitataka hilo jambo hive.  Mola karim amepanga mambo yote yatakayotokea moja moja hadi kufikia Qiyamah.  Amri ya Allah haiwezi kushindikana; ni lazima itakee.  Hivyo mtu anapofanya kosa basi ajue ni Qadar hiyo na ni Amri ya Mungu, hangeweza kufanya vinginevyo; na atendaye jema basi  ni Qadari ju yake na asingeliweza kufanya vingine.

48.       Basi watu wote wafahamu kuwa lolote litokealo hapa ulimwenguni Allah analijua na  alikuwa na habari nalo kabla halijatokea.  Hakuna awezaye kubadilisha Qadar ama kwa kusitisha, kupunguza kitu au kuongeza.  Na kuamini haya yote ni ishara ya imani thabiti, kwa kuutambua ukweli huu na mtu kuwa anajitambua yeye nafsi yake kwa kumpwekesha Mwenyezi Mungu.
            Allah amesema (25:2)
            Pia kasema Allah (33:38)
            Basi binadamu anajiweka katika mtihani mzito kwa (kuanza) kuleta upinzani juu ya Qadar, na akawa mwenye kudodosa na kutaka kujua mambo ya ghaibu kwa kutumia kupiga mabao au kuangalia nyota na mambo omengine ya kishiri kina ataishi kuwa mwogo tu.

            HABARI ZA ARSHI NA KURSIY

49.       Arshi, kiti chaenzi na kiti cha kursiyu ni vitu vya kweli vipo.

50.       Allah, ametakasika hana haja na Arshi wala kursiyu au kitu kingine kile zaidi ya hivyo.

51.       Allah yuko juu ya kila kitu.  Yeye ndiye anavitawala.  Hakuna kitakacho mshinda au kushingana naye alichilia mbali kumtangulia.

            NAFASI YA NABII IBRAHIMU NA MUSA

52.       Tunaamini kwa moyo wote kuwa Allah, alitoa kauli na kutamka kuwa Seyyidina Ibrahim (A.S) ni khalil o(rafiki) wake na Seyyidina Musa (A.S) ni kalimu Allahi (ali ye zungumza na Mola wake ana kwa ana).

            JUU YA VITABU VYA ALLAH

53.       Tunaviamini vitabu vyote vilivyoletwa na Allah duniani na kupewa mitume wake; manabii na marasuli na tuna toa ushuhuda kuwa vitabu vyote na mituwe wote wukweli.

            NANI MUISLAMU NA NANI MU’MIN

54.       Tunawachukua watu wote wanaoelekea kibla cha ka’aba (Makkah) ni Waislamu na waumini iwapo tu wanakubali sharia ya Mtume Muhammad (S.A.W) na wao wakayasema hayo okwa vinywao na nyoyo zao.

55.       Hatuingii katika mjadala na ukishi juu ya hali ya Allah manani na wala hatubishani katika mambo ya dini.

56.       Hatubishi wala hatupingi ineno wala kalmia au maana ya kutoka Quran tukufu.  Tunashahidia kuwa Quran ni neno la Allah mkarimu. Malaika kiongozi Jibril alieleta Quran kwa Muhammad (S.A.W) Seyyid wa manabii kwa kupitia wahyu.  Hakuna shaka kuwa Quran ni neno la Mwenyezi Mungu.  Maneno ya binadamu hayawezi kulingana na Quran na pia hatuiangalii Quran kama ni kumbe.  Si kiumbe.  Zaidi ya hapo hatupingani na watu wa ummah wa Kiislamu juu ya lolote katika haya.

57.       Hatumkufarishi mUislamu yoyote kwa sababu ya dhambi atakayo tenda labda kama mtu atakuwa ana itikadi kuwa jambo hilo alilotenda si dhambi[5].

58.       Na pia tunaamini kuwa kama mtu atakuwa mUislamu madhambi yake yanaathiri imani yake.  [Imani huongezeka kwa kutenda mema nakupungua kwa kufanya maasi].

59.       Ni tamaa (hope – rujaa’) yetu kuwa Mola atawasamehe wote wale waliokuwa na matendo mema (muhsinina) na atawaingiza Peponi kwa huruma zake.  Hili  hatusemi kuwa bila shaka wataingizwa Peponi bali ni ruja’a yetu.[6]   
            Tunaomba msamaha na maghufira kwa ajili ya wale wote wanafanya makosa maasi japo kuwa tunajua hatima ya mtu asi ni adhabu ya Allah hatuwakatii tama na kuendelea kuwaombea.

60.       Mtu anayekuwa na tabia ya kutojali adhabu ya Allah au mwenye kukata tama juu ya rehma za Mwenyezi ni hatari kwani hayo yanamtoa mtu katika mila ya Kiislamu.  Watu wa Qibla wao ni watu wa katikati (wanatamaa ya kupata pepo na wanakhofu adhabu ya Mola wao) mfasiri.

61.       Mtu hatoki katika uga na imani mpaka akanushe yote yale yaliyomfanya kuwa mUislamu hapo awali[7].

62.       Imani ya Uislamu inapaswa itamkwe kwa ulimi na ithibatishwe moyoni (Kifuani)[8].(Footnoote)

63.       Amri zote ambazo zimo katika Hadith sahihi za mtume (S.A.W) ni za kweli.

64.       Umuhimu wa Imani ni mmoja.  Waumini wote wako sawa kutokana na misingi ya imani yao ilivyo.  
Hata hivyo tofauti zao zipo katika tofauti zao kulingana na vile wanavyo mwogopa Allah na jinsi wanavyo jiepusha na maovu ya shahawati na tama na jinsi wanavyopendelea mambo mazuri.

65.       Waumini wote ni marafiki ArRahman (Allah), Anayeheshimka miongoni mwao mbele ya Allah ni yule anaye tuna kushikama na Quransana.

66.       Imani ni pamoja na kumwamini Alah na malaika wake; vitabu vyake, mitume wake; kuamini kuwepo siku ya Qiyamah nakuamini Qadar (kuwa mema na mabaya, matamu au machungi vyote vinatoka kwa Allah.

            IMANI JUU YA MITUME

67.       Tunayaamini yote yaliyotajwa hapo juu.  Hatubagui hata mmoja miongoni mwa mitume wa Mwenyezi Mungu.  Tunaamini kuwa mambo yote waliyoyalingania ni ya kweli.

68.       Watu ambao wahirtaki madhambi makubwa makubwa (kabairi) miongoni mwa wafuasi wa mtume Muhammad (S.A.W) hawatobaki katika moto wa Jahanamu milele, iwapo tu walikufa wakiwa na imani ya Tawhid ya Kiislamu nakumpwekesha Allah pamoja na kuwa hawakutubukwa makosa yao.  Watu waaina hiyo wanapokutana na Mola wao kama waumini, watakuwa chini ya utashi wa Allah na maamuzi yake; Akipenda ata wasamehe kwa Rahma zake; kasemavyo: (Nisai – 4:48)
            Lakini kama atataka, atawaadhibu kwa kuwapeleka motoni kulingana na wadilifu wake kwa makosa yao na kasha …… atawatoa kwa huruma zake na shafia za waja wake wema.  Na hapo ndipo atawaacha waingie Peponi.  Hili ni kwa kuwa Allah anawahifadhi wale wanaomtambua na hivyo hawachukuwi kuwa sawana wale wanaomkana ambao wamepoteza mwongoza wake na hawana urafiki naye.
            Ewe Mola! Ambaye anaupenda Uislamu na wafuasi wake!  Tuweke thabiti na imara katika Uislamu mpaka tunakutana nawetukiwa na Imani hii.

69.       Tunakubali kusali nyuma ya kila imamu ama meha mungu au mwenye madhambi ambao ni watu wa Qiblah.  Halikadhalika tunasema wajibu wetu kusalia jeneza la kila mmoja wa watu hao.

70.       Hatusemi au kwa kutangaza huyu ataingia Peponi ya yule ni mtu wa motoni.  Wala haluthubutu kumwita mmoja wao kuwa ni kafiri au mushiriki au mnafiki labda kama tabia hizi ziko wazi wazi katika watu hawa.  Ama yaliyofichikana katika tabia zao tunamwachia Allah.

71.       Hatukubali mauaji ya yeyote miongoni mwa watu wa umati Muhammad (S.A.W) isipokuwa wale ambao wanastahiki kisheria kwa misingi ya shariah.

            JUMUISHO

72.       Hatukubaliani na uasi dhidi ya maimamu na watawala wetu hata kama matendo yao ni maovu.  Hatuwa laani wala hatuwaasi. Tunachukua kuwa utu kwao ni vtii kwa Allah iwapo tu hawamuru katika kutenda madhambi.  Tunawaombea Mola awasamehe.

73.       Sisi tunafuata sunnah (za Mtume) na tunashikanana na jamaah na tunakuwa mbali na mgawanyiko wa ummah au kkuleta vikundi vikundi katika jamaah na umah.
74.       Tunawapenda watu wenye kutendea wenzao vitu vya hakina uadilifu na wanachukia uasi na ukhaini (Khiyana).

75.       Likitokea jambo ambayo hatulifahamu  basi tunasema “Allah A’lamu” yaani Allah mjuzi zaidi.

76.       Ni rahsa kwetu kwa watu kutawadha kwa kupaka maji juu ya khofu (soksi za ngozi); waki wa safarini au hata hawako safarini, kulingana na hadithi.

77.       Hajj na jihad vinapaswa kuendeshwa chini ya watu wenye mamlaka katika umah (Ual – Al – Amri) bila kujah  wao ni wacha mungu au watenda madhambi, nahilo litabaki vivyo hivyo mpaka Qiyamah; hakuna cha kusitisha hivyo wale kubatilisha.

78.       Tunaamini kuwepo kiraman na katibina (malaika waliopewa kazi ya kuandika lolote asemalo mwanadamu au kutenda) na kama vile Mola aliwaweka kuwa walinzi juu yetu.

79.       Tunaamini kuwepo kiraman na katibina (malaika waliopewa kazi ya kuandika lolote asemalo mwanadamu au kutenda) na kama vile Mola aliwaweka kuwa walinzi juu yetu.

80.       Tunaamini kuwepo adhabu ya kaburi kwa wale wanaostahiki hilo.  Tunaamini kuwa malaika wawili; Munkar na Nakir humwuliza kila mtu huko kaburini kwake juu ya Mwenyezi Mungu, Dini, na Mtume.  Hivyo ni kulingana na Hadithi za Mtume (S.A.W) pamoja na riwaya zilizopokelewa kutoka kwa maswahaba zake (R.A.).

81.       Kaburi  ama linakuwa ni bustani kutoka mabastani ya Peponi au ni shimo katika mashimo ya Motoni/Jahanamu.

82.       Tunaamini kuwa watu wote watafafuliwa na watalipwa kwa matendo yao ya duniani.  Tunamini kuwa matendo yote yatafikishwa siku hiyo kwa Allah, tunaamini kuwepo hisaabu na kusoma kila mmoja taarifa zake, kuwepo na malipo mema kwa matendo mazuri au malipo mazito kwa vitendo viovu.  Tunaamini kuwepo daraja juu ya Jahanamu na mizani (ya matendo).

83.       Vyote pepo na Jahanam tayari vimeshaumbwa na vipo.  Hivi vitu; pepo na moto, havita kuwa na mwisho wala kupotea.  Mwenyezi Mungu aliviumba hivyo kabla hajaumba viumbe vyake na akawaumba wale watakuwa wa Peponi na wale ambao watakuwa wa motoni. Atamwingiza amtakaye Peponi kwa sababu za Rahma zake or kumwingiza motoni kwa uadilifu wake.  Kila mtu anafanya lile ambalo ameandikwa kufanya na kila mtu anaelekea kule alikoandaliwa hatma yake.

84.       Mema na maovu vyote vimekadiriwa kwa ajili ya mwanadamu.  Mambo mema na mambo mabaya yamepangiwa yamfike binadamu. [Mtihani kwa mja ni aina mbili amaanapata neema; ama ashkuru  an akufura au anapata mambo yasiyopendeza katika nafsi yake na hapo ana ashukuru na kusubiri au akufuru – mfasiri].

85.       Uwezo wa kufanya kitu/jambo ni wa aina mbili;

            (i)         Tawfiq:

Ni Rahma kutoka kwa Allah ambayo inamwezesha mtu kufanya kulingana na maamrisho ya Mwenyezi Mungu au akajiepusha na kuacha vitu vilivyokatazwa.  Tawfiq huambalaria na matendo ya mtu.
Rahma zake Allah zinamwezesha mja kutekeleza amri alizopewa na Mola wake na akaacha matendo mawi.  Tawfiq daima imeambalania tendo fulani na haipo Tawfiq kabla ya tendo hilo ambapo mja anapatia katika kutimiza amri na anasubiri kwa kuacha alilokatazwa.  Tawfiq haitmsiani na kiumbe chochote maana hawana uwezo na Tawfiq.
           
(ii)        Uwezo wa afya, na uwezo wa vifaa mbali mbali ama kuwa navyo kama ni fursa au kutumia vinngo ya mwili wake mtu katika kutenda jambo.  Mwanadamu ataulizwa kwa amri ambayo hakuitekeleza iwapo alikuwa na uwezo wa kutima amri hiyo (kama kwa mtu mwenye mali ya kutosha akaacha kutoa zaka, au kwenda hija na mtu mwenye afya njema akaacha kufunga au kwenda kwenye jihadi)
                        Kasema Allah (Baqarah – 2: 286).

86.       Matendo ya watu waliumbwa na Allah lakini wanayachuma wao wenyewe.

87.       Allah amewataka kufanya yale tu wanayo yamudu.  (Hiyo ndiyo maana ya – la hawla wala quata Illa billahi) “Hakuna katikisika wala uwezo wowote isipoku kwa uwezo wake Allah.”  Tunasema hakuna mtu ambaye anaweza akaacha kufanya maova ila kwa uwezo na msada wa Allah.  Hakuna mtu mwenye uwezo wa kutenda jambo jema na utii kwa Allah na kuendelea na hali hiyo isipokuwa kwa tawfiq Allah.

88.       Kila kitu kinatokea kwa ntashi wake Allah.  Elimu yake, maamuzi yake na makadirio yake (Qadari) na utashi wake vimetawala matendo na matukio yote.
Amri za Allah ziko juu ya mambo yote.  Yeye hufanya yale atakayo kufanya; na kamwe hakuna afanyalo bila kufanya uadilifa.
            Amesema (21:23)
89.       Maiti ananufaika kwa matendo yake mazuri na nema aliyoyafanya katika uhai wake kama vile sala na zakah.

90.       Allah karim hupokea ddua za waja wake na huwapatia mahitaji yao.

91.       Allah ana miliki kila kitu.  Yeye hakuna kinachomumiliki.  Hakuna mtu ambaye asihitaji ya kutoka kwa Allah hata kwa kapuo la jicho. Na yule anayejiona kuwa hana jaja wala hahitaji chochote kutoka kwa mungu hata kwa kupuo la jicho anafanya jambo la kufuru na anaangamia.

92.       Mwenyezi Mungu huchukia na kufurahi lakini ghadhabu zake na furaha zake si kama vile vya viumber vyake.

93.       Tunawapenda maswahaba wa mtume (S.A.W) na mapenzi hayo hayazidiani baina ya swahaba kwa swahaba.

Tunawachukia wanaowadharau maswaha  na wale hutoa kauli mbovu juu ya maswahaba.  Tunasema juu yao kwa adabu na taadhima. Kuwapenda maswahaba ni (moja ya) (yaani chuki juu yao) ni kufuru, unafiki na khiyana (uhaini).

94.       Tunaamini kwa Khalifa wa kwanza baada ya Mtume (S.A.W) alikuwa Abu Bakar Al Sadiq kwa sababu yeye nafasi hiyo ililiangana naye zaidi ya maswahaba wote.  …… Baada yake alikuja Omar ibn Al-Khalab, kisha Uthman bin Afan na mwisho Ali ibn AbAbi Talib (R.A) Hawa wanne ni makhalifa waongofu.

95.       Tunashahidika kuwa wale maswahaba kumi walio bashiriwa peop na Mtume (S.A.W) ni watu wa Peponi kwa kauli yake Mtume; Nao ni hawa wafuatao:
            (i)         Abu Bakr                                            
(ii)        Umar ibn Al-khatab                 
            (iii)       Uthman bin Affan                     
            (iv)       AliTalha ibn Ubaidullah
            (v)        Al-Zabeir ibn Al-Wawam
(vi)       Sa’ad ibn Abi Waqqas
(vii)             Said ibn Zaid
(viii)           Abdurahman bin Auf na Talha ibn Abdullah
(ix)              Abuubaida  ibn jariah ambaye  anajulikana Amiri (mwenye kuaminiwa) Ummah.  Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote.

96.       Ameepuka na unafiti yule huwazungumza maswahaba kwa wema wa mtume (S.A.W) kwa wema na pia wake zake mtume (S.A.W) walitwahaika na machafu na watoto wake ambao walitakaswa kutokana na machafu.

97.       Asitajwe miongoni mwa ulamaa’ wa mwanzo na hata wale waliokuja baada yao kati maaifa ya hadithi au fiqih na tarekhe ila kwa adabu. Kusema maovu juu yao ni njia njema wala si adabu ya Kiislamu.

98.       Hakuna walii aliye juu ya mtume yoyote (A.S) Tunasema mtu mmoja/yeyote ni bora zaidi ya mawalii wote.

99.       Tunaamini makarama yali yoonekana kwa mawalii ikiwa kuna mapokezi yenye riwaya sahihi.

100.     Tunamini katika dalili zinatangulia kabla ya kiyamal; kama vile kutokea Dajjal, kushuka kwa Issa bin Maryam kutoka mbinguni, jua kuchomoza kutoka maghribi na kuonekana mnyama kutoka katika ardhi – dabbatu – l – Ardhi.

101.     Hatumwamini mpiga bao yeyote, wala mchawi au yeyote anayedai lolote linalopingana na kitabu cha Allah, Sunnah na Ijma’ ya Ummah.

102.     Tunaamini kuwa ummah lazima uwe katika hali ya pamoja kama jamaah; utengano na vikundi vikundi ni upotoshaji wenye madhara kwa ummah.

103.     Dini ya Mwenyezi Mungu ni moja huko ombinguni na hapa aidhi: Amesema Allah (2:19)  na pia kasema (5:3).

104.     Uislamu ni dini yenye kuwa katikati bila kuridisha sana mambo au kuyapunguza sana.
*      Amri zake si nyepesi sana wala si nzito sana.
*      Dini isiyomfananisha Allah kwa viumbe vyake.
*      Binadamu wako huru kufanya watakalo.
*      Hali ya kutoku kuogop adhabu ya Allah ni hali ya kulata tamaa juu ya Rahma zake.

105.     Hii ndiyo Dini yetu na Imani yetu toka ndani ya nyoyo zetu ikiwa ni wazi wazi kabisa.  Tuna jikinga kwa Allah na mtu yeyote anayeyapinga haya ambayo yameelezwa nasi.  

Tunaaomba Allah Karim atuongoe tuwe tuwe katika njia iliyonyooka hadi tufikie hali ya umauti tukia katika Dini hii.

No comments:

Post a Comment