Swali:
Je, mtoto mienzi minne hadi mwaka mmoja akikucheulia katika nguo itafaa kusalia?
-----------------------------------------------------------------------------------------
Jibu:
Bismillah;
Kipimo si umri bali ni hali ya kichanga. Kichanga ambacho hakili kitu isipokuwa maziwa tu, basi akikojolea nguo, unatakiwa kuimwagia maji yachuruzike - na siyo lazima kuikosha-. Viovyo hivyo, utafanya hivyo hivyo kwa kichanga kilichokucheulia nguoni. Hivyo, ndivyo alivyokuwa akifanya mtume S.A.W. alikuwa akiletewa
vichanga mara kwa mara ili kuwaombea dua au kuwafugnua vinywa -(yaani kutafuta kitu kama tende hivi), kisha akarambisha kwa kidole chake kichanga hichyo. Mara kadhaa ilitokea kuwa vichanga hivyo, nyakati nyengine humkojolea Mtume S.A.W kwenye nguo yake. Basi Mtume S.A.W. alikuwa akiomba aletewe maji na huyanyunyiza juu ya nguo yake pale alipokojolea kichanga na anakwenda kusali bila ya kuiosha au kuifua nguo yake. Hiyo ni hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Bi Aysha, mke wa Mtume S.A.W na ambayo imo katikata Bulkhari na Muslim.
Maulamaa wamebainisha kuwa kigezo ni kichanga kinacho nyonya tu, kwa dalili kwamba vichanga alivyokuwa akiletewa Mtume ni vile ambavyo bado havijala kitu, vinanyonya tu. Na huo ndio msimamo wa maulamaa wengi sana. Imam Malik hata hivyo, yeye anatofautisha baina ya mkojo wa kichanga cha kiume na kichanga cha kike. Ananyunyiza maji kwenye mkojo wa kichanga cha kiume na kuosha kwenye mkojo wa kichanga cha kike, na ana hadithi kutoka kwa Mtuime S.A.W inayosema: يغسل بول الجارية ويرش بول الصبي Imepokewa na Abu Daud. Hivyo, matapishi ya kichanga ni sawa na mkojo wa kichanga. Ama mkojo wa kichanga kilichoanza kula chakula, basi mkojo wake ni najisi na lazima paoshwe pale alipokojolea kwa kumwagia maji.
Wa billahi al-Tawfiq Dr. A. Shareef Abdulkader.

No comments:
Post a Comment