Tuesday, February 21, 2012

Hatari Ya Kutoa Fatwa bila ya Ilm.

Imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya watu bila ya ilimu kujichukulia madaraka kwa kutafuta hadithi hapa na pale (siku hizi kupitia google) kisha kupitia vipande vya aya za Qur'an na kujijibia maswali na kufikia uamuzi wa mambo fulani ya kisheria.

Tena hawasiti kuwaambia hata wenzao wanaouliza swali, "Hiyo ni haraaam!" ama "Bid'ah hiyo!" au kinyume chake. Hii ni hatari, kwani wanaweza kujipotosha wenyewe na kuwapotosha wengine na kujitia motoni. Tunao wasomi wa dini waliopitia elimu zinazowaruhusu kutoa fatwa kupitia misingi inayokubalika kisheria.

Hivi leo akitokea mtu akakwambia amesoma kwenye internet dawa ya gonjwa fulani, au amesoma kitabu jinsi ya kuondoa kansa utamuachia mwili wako akutibie? Iweje umruhusu mtu acheze na dini yako katika moyo wako?

Basi Ustadh Mbarak Ahmed anatuletea mada Hatari ya kutoa fatwa bila ya elimu.

No comments:

Post a Comment