Swali:
Asalam alaikum. Hadithi nyingi nilizoziskia anatajwa swahaba aliemsikia mtume (s.a.w) lakini sijaskia hadithi aliyopokea Bilal bin Rabbah (radhi allaahu anhu)na ndie swahaba aliekua kribu sana na mtume (s.a.w), nisaidieni na mnielimishe jambo hili tafadhalini.
Jibu:
Waalaykum salaam. Sayyidina Bilal (radhi allaahu anhu) amepokea hadithi arobaini na nne (44) na ana musnad yake (musnad Bilaal), na katika hizo kuna nne katika swahihayni.
Nyongeza!
Ukaribu wa Swahaba kwa Mtume (S.A.W) haupimwi kwa idadi ya hadithi alizozipokea kutoka kwake, bali kwa ucha Mungu wake na Imani yake juu ya Mtume (S.A.W) na mafunzo yake. Hakuna aliyekuwa karibu mno na Mtume (S.A.W), kiasi kwamba kila alipo onekana Mtume (S.A.W) basi na yeye huwa akionekana, kama Sayyidina Abu Bakr al-Siddiq (R.A) Na papo idadi ya hadithi alizozipokea Sayyidina Abu Bak kutoka kwa Mtume (S.A.W) ni kidogo sana kulingana na idadi ya hadithi walizopokea Maswahaba wengine. Sayyidina Umar (R.A) alisikika akisema: Sijapata kumuona Mtume asiwe na Abu Bakr! Mtume amesema mengi kuhusu utukufu na ikhlas ya Sayyidina Abu Bak (R.A) Bali Mweanyezi Mungu (S.W) pia amemsifu Abu Bakr kuwa ni Sahib wa Mtume ndani ya Qur'an.
Moja katika hadithi mashuhuri sana ni hii: Abu Sa'id al-Khudriyy (R.A) amesema: Alikaa Mtume (S.A.W) juu ya minbari yake akituwaidh; kwa kusema: "Mwenyezi Mungu amempa khiyari mja wake mmoja baina ya kumpa mazuri yote ya dunia au achukue kile kilicho Kwake; mja huyo (yaani yeye Mtume (S.A.W.) akachagua kilicho mikononi mwa Mwenyezi Mungu." Sayyidina Abu Bakr aliposikia maneno hayo, akielewa nini khassa alichokikusudia Mtume katika maneno hayo, alilia na kulia huku akisema: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Wallahi tumekutanguliza mbele ya baba zetu na mama zetu!". Abu Sa'id anasema: " Abu Bakr ndiye aliye elewa maneno ya Mtume, kwamba kiumbe aliyepewa khiyari ya kuchagua alikuwa Mtume, na sababu ya Mtume kusema hivyo, ni kwamba alikuwa akiwashajiisha maswahaba zake kujitolea katika Uwislamu. " Mtume (S.A.W) baada ya kusikia maneno hayo ya Sayyidina Abu Bakr, alisema; " Hakika mtu wa kutegemewa sana kuliko wote, kwangu mimi, kwa mali yake na usuhuba wake ni Abu Bakr, na lau kama ningekuwa naruhusiwa kuchagua mwandani wangu, basi ningemchagua Abu Bakr kuwa mwandani wangu; lakini UDUGU wa uislamu ndio unaotuunganisha pamoja. Zibeni kila tundu kwenye Msikiti isipokuwa tundu -analotumia- Abu Bakr!. [Muslim].
Abu Bakr alifikia kiwango cha YAQIN katika imani yake, kiasi cha kunukuliwa akisema, baad ya kuulizwa na maswahaba, aseme ni kipi khassa hicho anachokifanya zaidi ya maswahaba wengine? Abu Bakr alijibu: " Sina cha ziada! Naswali kama mnavyo swali. Zaidi, ni kwamba "Lau kama Mwenyezi Mungu (S.W). angelijitokeza mbele yangu nikamuona kwa macho yangu, basi imani yangu juu Yake (S.W) isingezidi hata punje moja!".
Wa bilah al-Tawfiq
No comments:
Post a Comment