"Wengi hufikiri kwa kufanya Ibadah watanyookewa na mambo yao ya kidunia, mtazamo huu si sahihi na Allah hatotulipa kwa hongo za Ibadah hizi! Kuna wengine huingia kwenye dini(kaafa/kiukamilifu)baada ya kushindwa katika dunia. Mtizamo huu na Niyah hii si swahihi kwani hata kwenye dini pia watashindwa kama walivyoshindwa kwenye dunia.
Zuhd sio kuacha kitu ukitamanicho bali kutoa kitu cha thamani ulichonacho na kukipeana. Huku ndio kuwa Zahid kikweli.
Tukirudi katika mambo ya Kidunia, jitahidi kuitumikia fani yako yoyote ile ya Kidunia ili uweze kuusaidia Uisilamu kuenea kwa nguvu zako ukaribu wako na Allah(Kuwa walii) kuko karibu sana kama ukijitahidi kwenye fani yako na kujiepusha na Haram, Dumu na yalolazimika kwako kidini(Faraidh) na ukithirishe kufanya mambo mengi ya kheri na dumu na Uradi(akisisitizia wird Aam) wako ambao ndio mwambata katika maisha yako yote"
~ Sayidnah Sheikh Muhammad Al-Yaaqoubi As-Shadhuli Hafidhahullah.
No comments:
Post a Comment