Friday, February 24, 2012

Swali kuhusu ulazima wa mawalii kwa bi harusi aliyewahi achika...

Swali:

Kuna watu wanasema mwanamke akiolewa kisha akiachika akitaka kuolewa tena basi wale mawalii zake si lazima, eti ni kweli?

Jibu:

Hadithi sahihi inasema: الأيم احق بنفسها من وليها والبكر تستأمر في نفسها وإذنها صماتها )رواه مسلم Mjane ana haki zaidi juu ya nafsi yake kuliko kuwa na walii wake, na Mwanamwari\Bikira huombwa idhini na kunyamaza kwake ndiyo kukubali kwake"



Hadithi nyengine inasema; الثيب أحق بنفسها من وليها Hadithi hizi, na nyenginezo kama hizo, zimepokelewa kwa njia mbali mbali sahihi na hivyo hazina mushkeli wowote kuhusu nani ana kauli ya mwisho kuhusu kuolewa! Mwanamwawi hawezi kuolewa au kuozeshwa mpaka akubali mwenyewe na akinyamaza baada ya kutakiwa idhini basi inamaanisha amekubali. Lakini akisema SITAKI, basi hawezi kuozeshwa kwa nguvu.

Ama mjane, kama ulivyomuelezea hapo juu, idhini yake anayo mwenyewe, kwa maana hiyo anaweza kumpa mamlaka mtu yeyote amtakaye ameuozeshe, awe mtu wa familia au la. Ndiyo maana yake. Maulamaa wengi, kwa msingi huo huo, wanasema kuwa mjane, mtu mzima aliyekwisha balighi na mwenye akili yake timamu na Si mtumwa, anaweza hata kujiozesha yeye mwenyewe mbele ya mashahidi wawili na mfunga ndoa . Yaani siyo lazima achague mwakilishi. Ni Imam Malik peke yake, ndiye anayesema kuwa Walii au mwakilishi ni budi, kwa maana hiyo, mwanamke mjane hawezi kujiozesha mwenyewe, bali anaweza kumteua mtu amtakaye ameuozeshe.

Shafii - ananukuliwa kukubaliana na Mwalimu wake Malik -mwanzoni, lakini baadaye aemungana na maulamaa wengine kwamba Walii au Mwakilishi mwanamume ni SUNA si Faradhi. Yaani, mjane mwenye sifa za kuwa huru kujiamulia, anaweza kujiozesha mwenyewe akipenda!

 Jee, kama mwanamke alizaa nje ya ndoa na hajawahi kuolewa inakuaje?

Huyo SI bikira na SI mjane -kisheria- lakini NI mwanmwari, kwa maana hajaolewa. Hivyo, kijamii ni mwanamwari na hivyo ataingia katika mkumbo wa yule ambaye hajawahi kuolewa.

Wallah 'Alam wa Billah al-Tawfiq
Dr. A. Shareef







No comments:

Post a Comment